Waziri Makamba: Msituhukumu, tupeni muda miradi ikamilike

Waziri Makamba: Msituhukumu, tupeni muda miradi ikamilike

Tafsiri ya kufaidika haipo clear. Anayefaidika huwa haongei sana wala kutumia muda mwingi kuandika. Hutumia muda mwingi kufaidika zaidi. Anayeandika sana na kuongea huwa ni kijakazi na hapo ndio tafsiri ya chawa inapokuja

Viongozi wao wanatumikia jamii ila wafaidika wa kwanza kabisa huwa ni familia, ndio maana jamii kubwa mnabaki kwenda shule kwa kutembea kwa miguu km 5, huku Watoto wao wakipanda ndege kwenda vacation Dubai. Hivyo tulitegemea Watoto wao ndio wawe mstari wa mbele kuwasifia na kuwatukuza, bahati mbaya kabisa kazi hiyo wanayo wengine
Ndio mfumo ulivyo wa Dunia,hata wewe makelele yote ni sababu ya njaa Kali 😄😄
 
Alikuwa akijibu maswali katika Program ya Mjadala ya Club House ya Msemaji wa Serikali.

========

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema, takribani nusu ya miradi ya kimkakati iliyoainishwa na serikali ipo kwenye sekta ya nishati.

January amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuwaamini na kuwapa Jukumu hilo na akasema hata utamaduni wa kazi katika wizara hiyo umebadilika. Alisema hayo baada ya kujibu maswali katika programu ya mjadala katika Club House ya Msemaji wa Serikali.

"Sisi tunachoomba ni muda na subira, kwasababu kazi hizi matokeo yake yanachukua muda kupatikana na hukumu ya kazi tunayoifanya sasa tungeomba itolewe mbele kidogo na sio sasa," alisema.

January alisema miaka ya nyuma wizara hiyo ilikuwa na sifa mbaya ya rushwa, mikataba mibaya lakini sasa wizara hiyo na taasisi zake wana mipango mahususi kuhakikisha wanazingatia maadili.

Alisema takribani kila siku kuna zabuni inatolewa katika wizara hiyo na takribani watu 30 wanazikosa zabuni hizo kila siku hivyo wanaokosa wanakuwa na hisia kwamba waliopata hawakupata kihalali.

Habari Leo
Ile kampuni ya India iliyolamba 70b .kweli makamba alikosa watanzania wa kuufanya hiyo software
 
Huyu kijana sijui kwanini ana kiburi kiasi hiki na kudharau wananchi kutokana na matendo yake yasiyofaa
Itakuwa family background na pengine ni genetic problem ya familia ile maana kama baba alidiriki kusema wazuri hawafi akimnanga mtu aliyetangulia mbele za haki, mtoto atakosaje kuwa na kiburi na dharau kiasi hiki.
 
Ndio mfumo ulivyo wa Dunia,hata wewe makelele yote ni sababu ya njaa Kali [emoji1][emoji1]
Mimi sina njaa, ndio maana sipigi kelele. Wewe mwenye njaa ndio unapiga kelele.

Mimi nina huo uwezo wa kusafiri vacation kwenda Dubai, hata hivyo sipo bongo.

Bottom line hii kazi yako inafaidisha zaidi watoto wao. Ona mlivyogawana majukumu, wewe ni kuandika na kusifia, wao ni bata na vacation Dubai.

Hata kama ndio uzoba sio kwa namna hii
 
Sijajua kwanini wananchi wanamwandama sana Makamba..! Huyu waziri kijana hana kosa lolote kwasababu yeye mwenyewe kakuta hali ya umeme ni mbaya sana nchini halafu siasa kibao. Imagine eti kufungiwa umeme Tsh 27,000/=?? Pia umeme wa TZ ni mchache mno kuweza kuhudumia watu zaidi ya 65m. Ujenzi wa bwawa utatuondolea hii shida na tutaacha kumlaumu mteule wa Rais ambaye ni waziri kijana Makamba.
Ana kosa kubwa sana ambalo hata Mungu aliye hai hatamsamehe abadani, yeye mwenyewe nafsi inamsuta hapo alipo
 
Mimi sina njaa, ndio maana sipigi kelele. Wewe mwenye njaa ndio unapiga kelele.

Mimi nina huo uwezo wa kusafiri vacation kwenda Dubai, hata hivyo sipo bongo.

Bottom line hii kazi yako inafaidisha zaidi watoto wao. Ona mlivyogawana majukumu, wewe ni kuandika na kusifia, wao ni bata na vacation Dubai.

Hata kama ndio uzoba sio kwa namna hii
Unakelele na lawama kama zote,dalili ya njaa 😁😁😁😁
 
Unakelele na lawama kama zote,dalili ya njaa [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Mimi njaa nilishaisahau. Mwenye shibe hawezi kila siku kuamka nakuandika thread za kutukuza watu

Serious kabisa mtu yupo vizuri kiuchumi anawezaje kuandika thread kila mara za kusifia wengine, anawezaje kujaza mipichapicha ya kusifia wengine kwenye simu?

Huo muda tu anaupata wapi?
 
Una njaa ndio maana kutwa kucha uko humu kulalamika kama sio njaa ni nini? Umewahi ona mwenye shibe analalamika mtandaoni? 🤣🤣
 
Kiburi na dharau ki vipi ?

kuna mwingine asipodanganywa akaambiwa ukweli anaona kadharauliwa

mwingine ukizungumza nae bila ya kucheka cheka anaona una dharau
Wanmtaka yule msukuma mwnzao aliyekuwa anawapiga fix,maneno mengi
 
Uzalishaji umeme hutegemea mahitaji, kuwa na watu mil 20 sio sababu wawe na umeme mdogo kuliko sisi.

Mahitaji hetu kwa sasa ni megawatt 1500, hiyo ni kwa mujibu wa huyo waziri.

Unataka tuzalishe megawatt 5000, tunakua tunazitumia wapi? Kuvutia wawekezaji wa viwanda vikubwa sio tu kuwa na umeme wa kutosha kuna factor nyingi. Lakini ukweli ni kuwa bado tunapaswa kuendelea kuwa tegemezi kwao kwa wanachozalisha, usifikiri wao ni wajinga watakuletea viwanda vikubwa hapa ili uache kununua kwao
Kwa hiyo watu wengi hawahitaji umeme mwingi? Kama mahitaji ni 1500MW kulikuwa na haja gani ya kuiharibu Selous na kuweka mradi wa umeme wakati tayari tuna 1600MW? Kwa soko tulilo nalo na utulivu wa kisiasa wawekezaji wengi sana wanahitaji kuja hapa ila umeme ndo unaleta shida. Hizo factor unazosema nyingi tumekidhi karibu zote.
 
Sijajua kwanini wananchi wanamwandama sana Makamba..! Huyu waziri kijana hana kosa lolote kwasababu yeye mwenyewe kakuta hali ya umeme ni mbaya sana nchini halafu siasa kibao. Imagine eti kufungiwa umeme Tsh 27,000/=?? Pia umeme wa TZ ni mchache mno kuweza kuhudumia watu zaidi ya 65m. Ujenzi wa bwawa utatuondolea hii shida na tutaacha kumlaumu mteule wa Rais ambaye ni waziri kijana Makamba.
Watu hawakufungiwa? Hata tozo za mwezi hazikuepo
 
Una njaa ndio maana kutwa kucha uko humu kulalamika kama sio njaa ni nini? Umewahi ona mwenye shibe analalamika mtandaoni? [emoji1787][emoji1787]
Mimi silalamiki bali najibu pale napoona hakupo sawa.
 
Kwa hiyo watu wengi hawahitaji umeme mwingi? Kama mahitaji ni 1500MW kulikuwa na haja gani ya kuiharibu Selous na kuweka mradi wa umeme wakati tayari tuna 1600MW? Kwa soko tulilo nalo na utulivu wa kisiasa wawekezaji wengi sana wanahitaji kuja hapa ila umeme ndo unaleta shida. Hizo factor unazosema nyingi tumekidhi karibu zote.
Nimekueleza kwa sasa mahitaji yamesemwa hayo na waziri.

Lengo la kuongeza hayo mengine ni kupunguza utegemezi wa nishati
Kumbuka tulikua tukinunua umeme kutoka kwa wazalishaji iptl. Pia hata sasa.umeme mwingi tunaotumia tunanunua kutoka kwa wawekezaji wa kwenye gesi.

Kuvutia wawekezaji ni sawa, Ila haimaanishi wawekezaji wakubwa wa viwanda watakuja hapo kwako alafu uache kuwategemea wao. Hata uvutie wawekezaji kiasi gani bado hawatakuja kuzalisha kwa wingi nchini kwako, unapaswa kulinua hili.
Labda kama ni kwa ajili yetu sisi wenyewe watanzania tuanze kuwekeza na kuzalisha
 
Back
Top Bottom