Waziri Makamba: Msituhukumu, tupeni muda miradi ikamilike

Waziri Makamba: Msituhukumu, tupeni muda miradi ikamilike

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
82,489
Reaction score
88,633
Alikuwa akijibu maswali katika Program ya Mjadala ya Club House ya Msemaji wa Serikali.

========

makamba.jpg

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema, takribani nusu ya miradi ya kimkakati iliyoainishwa na serikali ipo kwenye sekta ya nishati.

January amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuwaamini na kuwapa Jukumu hilo na akasema hata utamaduni wa kazi katika wizara hiyo umebadilika. Alisema hayo baada ya kujibu maswali katika programu ya mjadala katika Club House ya Msemaji wa Serikali.

"Sisi tunachoomba ni muda na subira, kwasababu kazi hizi matokeo yake yanachukua muda kupatikana na hukumu ya kazi tunayoifanya sasa tungeomba itolewe mbele kidogo na sio sasa," alisema.

January alisema miaka ya nyuma wizara hiyo ilikuwa na sifa mbaya ya rushwa, mikataba mibaya lakini sasa wizara hiyo na taasisi zake wana mipango mahususi kuhakikisha wanazingatia maadili.

Alisema takribani kila siku kuna zabuni inatolewa katika wizara hiyo na takribani watu 30 wanazikosa zabuni hizo kila siku hivyo wanaokosa wanakuwa na hisia kwamba waliopata hawakupata kihalali.

Habari Leo
 
Sijajua kwanini wananchi wanamwandama sana Makamba..! Huyu waziri kijana hana kosa lolote kwasababu yeye mwenyewe kakuta hali ya umeme ni mbaya sana nchini halafu siasa kibao. Imagine eti kufungiwa umeme Tsh 27,000/=?? Pia umeme wa TZ ni mchache mno kuweza kuhudumia watu zaidi ya 65m. Ujenzi wa bwawa utatuondolea hii shida na tutaacha kumlaumu mteule wa Rais ambaye ni waziri kijana Makamba.
 
Sio Wananchi ni sukuma gang na Chadomo wanamuona threats kwao.
 
Jibu lenye busara.....Fanya kazi Waziri. Hakikisha hakuna rushwa katika hiyo wizara. Imekuwa na changamoto miaka nenda miaka Rudi!
 
Back
Top Bottom