Waziri Makamba: Msituhukumu, tupeni muda miradi ikamilike

Sijajua kwanini wananchi wanamwandama sana Makamba..! Huyu waziri kijana hana kosa lolote kwasababu yeye mwenyewe kakuta hali ya umeme ni mbaya sana nchini halafu siasa kibao. Imagine eti kufungiwa umeme Tsh 27,000/=?? Pia umeme wa TZ ni mchache mno kuweza kuhudumia watu zaidi ya 65m. Ujenzi wa bwawa utatuondolea hii shida na tutaacha kumlaumu mteule wa Rais ambaye ni waziri kijana Makamba.
Ni chuki tu mkuu,huwa nashindwa pia kuelewa kwa nini anachukiwa kias hicho. Angalau hizo chuki wangeelekeza kwenye mzizi mkuu wa matatizo ambao ni CCM yenyewe tungefika mbali sana.
 
Mimi sio chawa
Uchawa ni kama komwe, halifichiki.

Ubaya wa hizi kazi huwa wanafanya watu ambao ni hopeless. Hii kazi ya hizi huwezi kukuta inafanywa na mdogo wake makamba, au abdul mtoto wa mama samia

Kuna mmoja mwaka jana nilimkuta pale mwenge kavaa t-shirt ya picha ya raisi akawa anabishana na wenzake pale hadi wanataka kupigana. nilimuuliza unafikiri kwa nini wewe ndio unafanya hayo na sio mtoto wa mama samia? Wajinga waliwao
 
Ingekja hivyo basi kusingekua na individual cases. Maana hata anayeiba au kula pesa ya serikali tu gesema sio yeye ni CCM

Yapo makosa ya CCM na yapo makosa ya individuals ndio maana walioshtakiwa wanashtakiwa kama individuals, huwezi fanya mambo ya kijinga alafu usingiziwe sio wewe bali ni ccm
 
Mpelekeni mahakamani.
 
Mpelekeni mahakamani.
Nimpeleke ili iwe nini? Mimi nimekujibu uliposema tatizo ni CCM.

Makonda afanye ujinga wake tumuache yeye tuilaumu ccm? Musiba adaiwe pesa kwa ujinga wake, tumuache tuilaumu ccm?
 
Wewe Tsh 27,500/= ukipewa utafanyi nini cha maendeleo? Inatosha hata kioo cha simu yako?
Serikali inakusanya Kodi na hurudisha huduma kwa jamii. moja ya huduma ndio hiyo ya umeme

Tanesco haipati faida kwa watu kulipia kuunganisha umeme, inapata faida kwa watu kununua umeme na kutumia.

Ni kama watu wanavyotumia barabara, ingekua hivyo hata kutembea kwenye lami iliyojengwa na serikali ilipaswa kulipia.
 
Kalemani yeye alikuwa anautoa wapi umeme? Makamba hafai ni mwizi
Kina Kalemani na serikali ya jiwe waliosema tunaidai Barrick trilioni 495? Hao walikuwa ni waongo waliokubuhu. Umeme haujawahi kutosha nchi hii. Hadi August 2022 Tanzania yenye watu zaidi ya milioni 60 ilikiwa ina umeme wa megawatts 1600 tu wakati Zimbabwe yenye watu chini ya 20m ikiwa na 2240MW na Zambia ya watu 20m ikiwa na 3450MW. Na Tanzania ni kubwa kieneo kuliko hizo nchi. Nchi haiwezi kuwa na viwanda kwa umeme mdogo uliopo. Suala la umeme litapata tiba baada ya bwawa kukamilika. Kwa upande bado naona hata pamoja na bwawa bado umeme hautatosha. Angalau tungekuwa na 5000MW mambo yangeenda kwa kasi sana kiuchumi.
 
Serikali inakusanya Kodi na hurudisha huduma kwa jamii. moja ya huduma ndio hiyo ya umeme

Tanesco haipati faida kwa watu kulipia kuunganisha umeme, inapata faida kwa watu kununua umeme na kutumia.

Ni kama watu wanavyotumia barabara, ingekua hivyo hata kutembea kwenye lami iliyojengwa na serikali ilipaswa kulipia.
Wewe unaongea tu siasa huna unalojua
 
Tupunguze makasiriko na kufuata mkumbo, tufanye uchunguzi wa kina na kufuatilia mambo katika uhalisia wake ni hapo tu ndio tutajua mbivu na mbichi.

Makamba piga kazi kwa nafasi uliyonayo, ipo siku watanzania wataelewa.
 
Kina Kalemani na serikali ya jiwe waliosema tunaidai Barrick trilioni 495? Hao walikuwa ni waongo waliokubuhu. Umeme haujawahi kutosha nchi hii. Hadi August 2022 Tanzania yenye watu zaidi ya milioni 60 ilikiwa ina umeme wa megawatts 1600 tu wakati Zimbabwe yenye watu chini ya 20m ikiwa na 2240MW na Zambia ya watu 20m ikiwa na 3450MW. Na Tanzania ni kubwa kieneo kuliko hizo nchi. Nchi haiwezi kuwa na viwanda kwa umeme mdogo uliopo. Suala la umeme litapata tiba baada ya bwawa kukamilika. Kwa upande bado naona hata pamoja na bwawa bado umeme hautatosha. Angalau tungekuwa na 5000MW mambo yangeenda kwa kasi sana kiuchumi.
Uzalishaji umeme hutegemea mahitaji, kuwa na watu mil 20 sio sababu wawe na umeme mdogo kuliko sisi.

Mahitaji hetu kwa sasa ni megawatt 1500, hiyo ni kwa mujibu wa huyo waziri.

Unataka tuzalishe megawatt 5000, tunakua tunazitumia wapi? Kuvutia wawekezaji wa viwanda vikubwa sio tu kuwa na umeme wa kutosha kuna factor nyingi. Lakini ukweli ni kuwa bado tunapaswa kuendelea kuwa tegemezi kwao kwa wanachozalisha, usifikiri wao ni wajinga watakuletea viwanda vikubwa hapa ili uache kununua kwao
 
Wewe unaongea tu siasa huna unalojua
Hakuna nalojua? Ndio uzuri wa jf, nyuma ya keyboard kila mtu mbabe

Sikngei siasa, siasa unayo wewe ambaye bata jina tu umeamua kubadili na kuweka la mwanasiasa, Jambo ambalo hata mtoto wake hawezi kufanya
 
Uchawa ni kama komwe, halifichiki.

Ubaya wa hizi kazi huwa wanafanya watu ambao ni hopeless. Hii kazi ya hizi huwezi kukuta inafanywa na mdogo wake makamba, au abdul mtoto wa mama samia

Kuna mmoja mwaka jana nilimkuta pale mwenge kavaa t-shirt ya picha ya raisi akawa anabishana na wenzake pale hadi wanataka kupigana. nilimuuliza unafikiri kwa nini wewe ndio unafanya hayo na sio mtoto wa mama samia? Wajinga waliwao
Uchawa ni upi? Au inakuaje? Kama ku deal na nyie wapotoshaji basi Niko tayari kuwa chawa Hadi kufa ilimradi niweke rekodi sawa.
 
Mimi nimejaribu kuweka sawa tafsiri ya uchawa.

Pia nimesema hapo kazi kama hizi hazifanywi na Watoto wao au wadogo zao bali hufanywa na watu ambao ni hopeless.
 
Hopeless hawezi fanya kazi ambayo hanufaiki nayo.

Pili Watoto wao hawawezi fanya hivyo maana baba zao hawatumikii familia Bali jamii.
 
Alikuwa akijibu maswali katika Program ya Mjadala ya Club House ya Msemaji wa Serikali.

========

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema, takribani nusu ya miradi ya kimkakati iliyoainishwa na serikali ipo kwenye sekta ya nishati.

January amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuwaamini na kuwapa Jukumu hilo na akasema hata utamaduni wa kazi katika wizara hiyo umebadilika. Alisema hayo baada ya kujibu maswali katika programu ya mjadala katika Club House ya Msemaji wa Serikali.

"Sisi tunachoomba ni muda na subira, kwasababu kazi hizi matokeo yake yanachukua muda kupatikana na hukumu ya kazi tunayoifanya sasa tungeomba itolewe mbele kidogo na sio sasa," alisema.

January alisema miaka ya nyuma wizara hiyo ilikuwa na sifa mbaya ya rushwa, mikataba mibaya lakini sasa wizara hiyo na taasisi zake wana mipango mahususi kuhakikisha wanazingatia maadili.

Alisema takribani kila siku kuna zabuni inatolewa katika wizara hiyo na takribani watu 30 wanazikosa zabuni hizo kila siku hivyo wanaokosa wanakuwa na hisia kwamba waliopata hawakupata kihalali.

Habari Leo
Go brother we have faith in you 🙏💪
 
Apewe muda zidi kuharibu, pathetic
 
Hopeless hawezi fanya kazi ambayo hanufaiki nayo.

Pili Watoto wao hawawezi fanya hivyo maana baba zao hawatumikii familia Bali jamii.
Tafsiri ya kufaidika haipo clear. Anayefaidika huwa haongei sana wala kutumia muda mwingi kuandika. Hutumia muda mwingi kufaidika zaidi. Anayeandika sana na kuongea huwa ni kijakazi na hapo ndio tafsiri ya chawa inapokuja

Viongozi wao wanatumikia jamii ila wafaidika wa kwanza kabisa huwa ni familia, ndio maana jamii kubwa mnabaki kwenda shule kwa kutembea kwa miguu km 5, huku Watoto wao wakipanda ndege kwenda vacation Dubai. Hivyo tulitegemea Watoto wao ndio wawe mstari wa mbele kuwasifia na kuwatukuza, bahati mbaya kabisa kazi hiyo wanayo wengine
 
Back
Top Bottom