Waziri Mahiga: Mkataba kusaka walioficha mabilioni Uswisi wasainiwa Tanzania

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,727
2,000
IMG_0447.JPG

Serikali ya Tanzania na Uswisi zimesaini Mkataba utakaowawezesha Makachero wa Tanzania kwenda nchini Uswisi na kufanya uchunguzi katika mabenki ya huko ili kupata taarifa sahihi za walioficha mabilioni toka Tanzania.

Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr Augustine Mahiga na Balozi wa Uswisi nchini Florence Mattli.

Hata hii ni moja ya hatua muhimu ya Serikali awamu ya tano katika kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma.
========================

HUKU kukiwepo na dhana ya kuwa kuna Watanzania wanaotorosha fedha na kuzificha katika mataifa mbalimbali ikiwemo Uswisi, hatua moja muhimu imefanyika katika kukabili suala hilo, baada ya serikali ya nchi hizo mbili, kusaini mkataba muhimu.

HabariLeo Jumapili imebaini kufikiwa kwa makubaliano ya ushirikiano muhimu wa kisheria kwenye masuala ya jinai, unaolenga kuwajengea uwezo makachero wa Tanzania, kuchunguza masuala mbalimbali ya kiuhalifu nchini Uswisi.

Mkataba huo umeenda mbali zaidi, kwa kuweka wazi kuwa kuanzia sasa makachero hao, wanaweza kuchunguza fedha za Watanzania zilizohifadhiwa nchini Uswisi, tofauti na awali ambapo sheria za nchi hiyo zilikuwa zinazuia.

Mkataba huo umesainiwa hivi karibuni wakati wa Maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi. Uswisi ni nchi inayosifiwa kuwa na huduma bora za kibenki huku ikiwa na sheria kali zinazowalinda wateja wake.

Mkataba wa makubaliano hayo, ambao umeleta mwanga katika kukabiliana na usiri wa fedha hizo, ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga na Balozi wa Uswisi nchini, Florence Mattli.

Akizungumza na gazeti katika mahojiano maalumu kuhusu mkataba huo, Balozi Mahiga alisema kuwa katika kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo, Tanzania itanufaika na ruhusa hiyo ya kufuatilia akaunti za fedha Uswisi.

Alisema kuwa kipengele hicho, kimekubaliwa kwenye makubaliano na kwa sasa hakuna tena kikwazo kitakachoizuia Tanzania kuchunguza akaunti hizo.

Alisema kuwa hatua hiyo inatokana na Serikali ya Uswisi pia kuridhishwa na namna ambavyo Tanzania imekuwa ikipambana na vitendo vya rushwa na ufisadi, kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wake chini ya uongozi wa Rais John Magufuli.

Alisema, Uswisi imekuwa ni rafiki mkubwa wa Tanzania tangu enzi na enzi huku ikiisaidia katika uboreshaji wa sekta mbalimbali.

“Kweli hiyo ni hatua nzuri kwa Tanzania hasa kwa kipindi hiki ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikikabiliana na rushwa na kila aina ya ufisadi na kwa hiyo ruhusa hii itasaidia kulinda fedha zetu kutoroshwa,” alisema Balozi Mahiga.

Akijibu swali ni lini serikali itakuwa tayari kupeleka makachero nchini humo, kuchunguza madai ya kuwepo kwa Watanzania walioficha fedha kwenye benki za nchini humo, Balozi Mahiga alisema; “Siwezi kusema ni lini hatua hiyo inaweza kuanza kuchukuliwa kwa kuwa zipo mamlaka zinazohusika na utekelezaji wake, ila ninachoweza kusema ni kuwa hatua iliyofikiwa ni ya msingi kwetu kama nchi.”

Zitto apongeza Mkataba Akitoa maoni yake kuhusu makubaliano hayo, Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT – Wazalendo ), mmoja wa wabunge ambaye amekuwa akilizungumzia suala la ufichwaji wa mabilioni ya fedha nje ya nchi, aliliambia gazeti hili kuwa kipengele hicho kwenye mkataba huo ni kizuri na kitasaidia kupatikana kwa fedha zilizofichwa katika benki za Uswisi.

Alitumia nafasi hiyo kuipongeza serikali kwa uamuzi huo uliofikiwa na kusema ni hatua ya kimafanikio, hasa ikizingatiwa kuwa fedha hizo zinatokana na nguvu za wanyonge, ambapo pia zilipatikana kinyume na sheria. Balozi Mattli, alisema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi, umekuwa ukiimarika zaidi kila siku, na kuwa nchi hiyo itaendelea kuisaidia Tanzania kwa hali na mali.

Chanzo: Habari Leo
 
eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
13,730
2,000
Safi sana, asiishie hapo tu, pia asign mkataba na EU pia kuwawezesha makachero kuperuz mihela iliyotumbukizwa huko. Bado hongkong na AUE.
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,372
2,000
Umekurupuka toka wapi wewe?mtu mwenye sifa ya hili jina ...nyabhingi...hakurupuki na kutoa maoni ya kijiweni kama wewe
Between the lines namaanisha huyu mwizi hawezi kukamata mwizi...hapambani na mafisadi papa huyu mtu,anaishia kwa vidagaa tu,lugumi na escrow hata kuvitaja anaogopa,nyinyi mnaamini blah blah zake!!zitto alishatoaga majina ya watu walioficha pesa nje,aanze na hayo!!!!
 
mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,856
2,000
Wanazuga wana vyombo vya usalama kibao...wanasubiria hadi ZZK awatonye
 
Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
11,559
2,000
-Mafisadi mashenzi mapuuzi sana mwafikiri yatakuwa hayajazihamisha?/
•vipo visiwa hapo uingereza
•dubai
• kapo kakisiwa huko latin amerika hasa haka kakisiwa ndiko kabaya sana hawatai fununu zozote/
Yupo jamaa yetu ana mji mkubwa tu marekani/ maekari,...nisije nikalia bure.../ wilimmporha ..jibu / gete gete.. wewe ...
 
niah

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
6,548
2,000
Safi sana, asiishie hapo tu, pia asign mkataba na EU pia kuwawezesha makachero kuperuz mihela iliyotumbukizwa huko. Bado hongkong na AUE.
Kuna watu huwa wanasema tunakwenda kwa matukio. Hii imefanywa ili watu wasahau matukio mengine. Lugumi ilikwenda weeeee ipo wapi? Escrow ilikwenda weeee sasa oko wapi? Kama tumeshindwa kukamata pesa ambazo zilikuwa kwenye mabenki yetu na majumbani hapa Tz unategemea hao wajinga muda wote huo si walishahamisha accounts. Mswizi hana biashara zaidi ya banking na kutengeneza saa sasa unafikiri yeye ale wapi? Pesa za Mobutu zilisharudi? Marais wote wa Nigeria wanasemekana waliwekeza huko je imekuwaje? Mtu pekee aliyeweza kutumia umafia na kunyang'anya watu wakubwa ujiko ni yule mjeshi wa Ghana Rawling aliyeamua kuwaua marais wote wa zamani na kutaifisha mali zao. Baada ya hapo unaona Ghana woga ukawapata sasa hivi ni nchi inasifika kwa utawala bora. Kwetu sisi ni kulindana. Ikiwa mswada wa habari tu umeleta maneno ya kuletwa itakuwa kitu utajiri wa vizazi na vizazi?
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
9,083
2,000
Mikataba ya kipuuzi hiyo..
Hata hao makachero wakija na find outs za walioficha hizo pesa majina yao mtayaficha na kuyakalia tu.
Kama kweli JPM ameamua kupambana na wizi na ufisadi aanze kushugulika na Lugumi, Escrow na mkataba wa 60Bil za sare za jeshi la polisi.. Hawa tunao humu humu wala sio wa kuwafata Uswiss..
 
Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
26,737
2,000
Najiuliza Hii Serikali Ya Viwanda

Inataka Kumdanganya Nani ?Kuhusu Huko Kusainiwa Mkataba Wa Ajabu Kuwahi Kutokea Nchini.
Jumanne Pondamali Mensah Ameshasema Hana Mpango Wowote Wa Kufukua Makaburi Yoyote Ya Wafu
Maana Hataweza Kuyafukia Tena.

Viini Macho Nchini Vitaisha Lini Eti Waziri Naye Kasaini Mkataba Kama Msomi Mbobezi Kwenye Huo Mkataba
Watanzani Tumeligwa Wapi ?
Yaani Utadhani Tupo Kwa Mganga Kila Kitu Tawire Mganga,Makachero Huku Tunaambiwa Makaburi Hayafukuliwi Kamwe
 
avogadro

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
4,130
2,000
Kimenuka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! lakini hawakufanya poa kutangaza !!!!!!!!!!!!! mwizi huwa anaviziwa na kukamatwa kimya kimya!!!!!!!!!!!!!!! ukimpa taarifa anahamisha visibiti.
 
TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
4,618
2,000
View attachment 429957

Serikali ya Tanzania na Uswisi zimesaini Mkataba utakaowawezesha Makachero wa Tanzania kwenda nchini Uswisi na kufanya uchunguzi katika mabenki ya huko ili kupata taarifa sahihi za walioficha mabilioni toka Tanzania.

Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr Augustine Mahiga na Balozi wa Uswisi nchini Florence Mattli

Hata hii ni moja ya hatua muhimu ya Serikali awamu ya tano katika kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma.
========================

HUKU kukiwepo na dhana ya kuwa kuna Watanzania wanaotorosha fedha na kuzificha katika mataifa mbalimbali ikiwemo Uswisi, hatua moja muhimu imefanyika katika kukabili suala hilo, baada ya serikali ya nchi hizo mbili, kusaini mkataba muhimu.

HabariLeo Jumapili imebaini kufikiwa kwa makubaliano ya ushirikiano muhimu wa kisheria kwenye masuala ya jinai, unaolenga kuwajengea uwezo makachero wa Tanzania, kuchunguza masuala mbalimbali ya kiuhalifu nchini Uswisi.

Mkataba huo umeenda mbali zaidi, kwa kuweka wazi kuwa kuanzia sasa makachero hao, wanaweza kuchunguza fedha za Watanzania zilizohifadhiwa nchini Uswisi, tofauti na awali ambapo sheria za nchi hiyo zilikuwa zinazuia.

Mkataba huo umesainiwa hivi karibuni wakati wa Maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi. Uswisi ni nchi inayosifiwa kuwa na huduma bora za kibenki huku ikiwa na sheria kali zinazowalinda wateja wake.

Mkataba wa makubaliano hayo, ambao umeleta mwanga katika kukabiliana na usiri wa fedha hizo, ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga na Balozi wa Uswisi nchini, Florence Mattli.

Akizungumza na gazeti katika mahojiano maalumu kuhusu mkataba huo, Balozi Mahiga alisema kuwa katika kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo, Tanzania itanufaika na ruhusa hiyo ya kufuatilia akaunti za fedha Uswisi.

Alisema kuwa kipengele hicho, kimekubaliwa kwenye makubaliano na kwa sasa hakuna tena kikwazo kitakachoizuia Tanzania kuchunguza akaunti hizo.

Alisema kuwa hatua hiyo inatokana na Serikali ya Uswisi pia kuridhishwa na namna ambavyo Tanzania imekuwa ikipambana na vitendo vya rushwa na ufisadi, kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wake chini ya uongozi wa Rais John Magufuli.

Alisema, Uswisi imekuwa ni rafiki mkubwa wa Tanzania tangu enzi na enzi huku ikiisaidia katika uboreshaji wa sekta mbalimbali.

“Kweli hiyo ni hatua nzuri kwa Tanzania hasa kwa kipindi hiki ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikikabiliana na rushwa na kila aina ya ufisadi na kwa hiyo ruhusa hii itasaidia kulinda fedha zetu kutoroshwa,” alisema Balozi Mahiga.

Akijibu swali ni lini serikali itakuwa tayari kupeleka makachero nchini humo, kuchunguza madai ya kuwepo kwa Watanzania walioficha fedha kwenye benki za nchini humo, Balozi Mahiga alisema; “Siwezi kusema ni lini hatua hiyo inaweza kuanza kuchukuliwa kwa kuwa zipo mamlaka zinazohusika na utekelezaji wake, ila ninachoweza kusema ni kuwa hatua iliyofikiwa ni ya msingi kwetu kama nchi.”

Zitto apongeza Mkataba Akitoa maoni yake kuhusu makubaliano hayo, Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT – Wazalendo ), mmoja wa wabunge ambaye amekuwa akilizungumzia suala la ufichwaji wa mabilioni ya fedha nje ya nchi, aliliambia gazeti hili kuwa kipengele hicho kwenye mkataba huo ni kizuri na kitasaidia kupatikana kwa fedha zilizofichwa katika benki za Uswisi.

Alitumia nafasi hiyo kuipongeza serikali kwa uamuzi huo uliofikiwa na kusema ni hatua ya kimafanikio, hasa ikizingatiwa kuwa fedha hizo zinatokana na nguvu za wanyonge, ambapo pia zilipatikana kinyume na sheria. Balozi Mattli, alisema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi, umekuwa ukiimarika zaidi kila siku, na kuwa nchi hiyo itaendelea kuisaidia Tanzania kwa hali na mali.

Chanzo: Habari Leo
Vigogo wote leo wanaharisha... Big up Magu. Big up Mahinga
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom