Waziri Mahiga: Mkataba kusaka walioficha mabilioni Uswisi wasainiwa Tanzania

cjui wanamtapeli nani??mmh.pesa wanaficha wao hlf eti tumesaini mkataba,ptuuuuu poor CCM
 
Safi sana, asiishie hapo tu, pia asign mkataba na EU pia kuwawezesha makachero kuperuz mihela iliyotumbukizwa huko. Bado hongkong na AUE.
MBONA MAJINA YA WALIOCHOTA PESA ZA ESCROW BANK ILE HAYAJULIKANI KWA NINI MJUE YA NCHI NYINGINE WAKATI YALIYOPO NCHINI MWENU HAMWEZI KUYAJUA? MBONA NCHI INAPATA AIBU NAMNA HII.
 
Mikataba ya kipuuzi hiyo..
Hata hao makachero wakija na find outs za walioficha hizo pesa majina yao mtayaficha na kuyakalia tu.
Kama kweli JPM ameamua kupambana na wizi na ufisadi aanze kushugulika na Lugumi, Escrow na mkataba wa 60Bil za sare za jeshi la polisi.. Hawa tunao humu humu wala sio wa kuwafata Uswiss..
KIKWETE ALIPOKUWA MADARAKANI ALISEMA ANAWAJUA WAUZA UNGA KWA MAJINA YAO......MPAKA ANAONDOKA MADARAKANI ALIOGOPA KUWATAJA......AMINA CHIFUPA (RIP) ALIPOSIMAMA BUNGENI NA KUONYESHA NIA YA DHATI KUWATAJA WAHUSIKA.....YALOMPATA KILA MWENYE AKILI ANAJUA.....HUYU MAGU NI MNAFIKI KAMA KASHINDWA UA NYOKA ALIYEKO CHUMBANI KWAKE ATAWEZA MUUA NYOKA KWENYE CHUMBA CHA JIRANI YAKE....TUMECHOKA NA NGONJERA, MASHAIRI NA SINGELI ZA CCM NA WATAWALA WAKE WAOGA NA WANAFIKI...
 
Kuna watu huwa wanasema tunakwenda kwa matukio. Hii imefanywa ili watu wasahau matukio mengine. Lugumi ilikwenda weeeee ipo wapi? Escrow ilikwenda weeee sasa oko wapi? Kama tumeshindwa kukamata pesa ambazo zilikuwa kwenye mabenki yetu na majumbani hapa Tz unategemea hao wajinga muda wote huo si walishahamisha accounts. Mswizi hana biashara zaidi ya banking na kutengeneza saa sasa unafikiri yeye ale wapi? Pesa za Mobutu zilisharudi? Marais wote wa Nigeria wanasemekana waliwekeza huko je imekuwaje? Mtu pekee aliyeweza kutumia umafia na kunyang'anya watu wakubwa ujiko ni yule mjeshi wa Ghana Rawling aliyeamua kuwaua marais wote wa zamani na kutaifisha mali zao. Baada ya hapo unaona Ghana woga ukawapata sasa hivi ni nchi inasifika kwa utawala bora. Kwetu sisi ni kulindana. Ikiwa mswada wa habari tu umeleta maneno ya kuletwa itakuwa kitu utajiri wa vizazi na vizazi?

Asante kwa mchango mzuri Mkuu ,kwa kuongezea tu ni kuwa jambo ambalo hufanikiwa kwa asilimia mia huwa linafanywa na mfanyaji kwa hiari na kwa nia thabiti...

Serikali hii ya CCM huwa inasukumwa /inalazimishwa kufanya baadhi ya mambo,hili lilishasemwa kwa kipindi kirefu sana ona namna linavyo shughulikiwa.Alie ktk jumba jeupe kakiri yeye mwenyewe kuwa hawezi kufukua Makaburi sababu Nchi itatikisika ...
 
na pia makachero waende dubai kuchunguza pesa za mh. mwenyekiti zilizohamishwa kipindi cha uchaguzi kama ni za halali
 
Hakuna jipya Mahiga mbona munahagaika na USWISI kama mko serious anzieni na wewe na wabunge wenzako muliopewa milioni kumi ili mupitishe muswada wa habari.
 
View attachment 429957

Serikali ya Tanzania na Uswisi zimesaini Mkataba utakaowawezesha Makachero wa Tanzania kwenda nchini Uswisi na kufanya uchunguzi katika mabenki ya huko ili kupata taarifa sahihi za walioficha mabilioni toka Tanzania.

Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr Augustine Mahiga na Balozi wa Uswisi nchini Florence Mattli

Hata hii ni moja ya hatua muhimu ya Serikali awamu ya tano katika kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma.
========================

HUKU kukiwepo na dhana ya kuwa kuna Watanzania wanaotorosha fedha na kuzificha katika mataifa mbalimbali ikiwemo Uswisi, hatua moja muhimu imefanyika katika kukabili suala hilo, baada ya serikali ya nchi hizo mbili, kusaini mkataba muhimu.

HabariLeo Jumapili imebaini kufikiwa kwa makubaliano ya ushirikiano muhimu wa kisheria kwenye masuala ya jinai, unaolenga kuwajengea uwezo makachero wa Tanzania, kuchunguza masuala mbalimbali ya kiuhalifu nchini Uswisi.

Mkataba huo umeenda mbali zaidi, kwa kuweka wazi kuwa kuanzia sasa makachero hao, wanaweza kuchunguza fedha za Watanzania zilizohifadhiwa nchini Uswisi, tofauti na awali ambapo sheria za nchi hiyo zilikuwa zinazuia.

Mkataba huo umesainiwa hivi karibuni wakati wa Maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi. Uswisi ni nchi inayosifiwa kuwa na huduma bora za kibenki huku ikiwa na sheria kali zinazowalinda wateja wake.

Mkataba wa makubaliano hayo, ambao umeleta mwanga katika kukabiliana na usiri wa fedha hizo, ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga na Balozi wa Uswisi nchini, Florence Mattli.

Akizungumza na gazeti katika mahojiano maalumu kuhusu mkataba huo, Balozi Mahiga alisema kuwa katika kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo, Tanzania itanufaika na ruhusa hiyo ya kufuatilia akaunti za fedha Uswisi.

Alisema kuwa kipengele hicho, kimekubaliwa kwenye makubaliano na kwa sasa hakuna tena kikwazo kitakachoizuia Tanzania kuchunguza akaunti hizo.

Alisema kuwa hatua hiyo inatokana na Serikali ya Uswisi pia kuridhishwa na namna ambavyo Tanzania imekuwa ikipambana na vitendo vya rushwa na ufisadi, kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wake chini ya uongozi wa Rais John Magufuli.

Alisema, Uswisi imekuwa ni rafiki mkubwa wa Tanzania tangu enzi na enzi huku ikiisaidia katika uboreshaji wa sekta mbalimbali.

“Kweli hiyo ni hatua nzuri kwa Tanzania hasa kwa kipindi hiki ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikikabiliana na rushwa na kila aina ya ufisadi na kwa hiyo ruhusa hii itasaidia kulinda fedha zetu kutoroshwa,” alisema Balozi Mahiga.

Akijibu swali ni lini serikali itakuwa tayari kupeleka makachero nchini humo, kuchunguza madai ya kuwepo kwa Watanzania walioficha fedha kwenye benki za nchini humo, Balozi Mahiga alisema; “Siwezi kusema ni lini hatua hiyo inaweza kuanza kuchukuliwa kwa kuwa zipo mamlaka zinazohusika na utekelezaji wake, ila ninachoweza kusema ni kuwa hatua iliyofikiwa ni ya msingi kwetu kama nchi.”

Zitto apongeza Mkataba Akitoa maoni yake kuhusu makubaliano hayo, Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT – Wazalendo ), mmoja wa wabunge ambaye amekuwa akilizungumzia suala la ufichwaji wa mabilioni ya fedha nje ya nchi, aliliambia gazeti hili kuwa kipengele hicho kwenye mkataba huo ni kizuri na kitasaidia kupatikana kwa fedha zilizofichwa katika benki za Uswisi.

Alitumia nafasi hiyo kuipongeza serikali kwa uamuzi huo uliofikiwa na kusema ni hatua ya kimafanikio, hasa ikizingatiwa kuwa fedha hizo zinatokana na nguvu za wanyonge, ambapo pia zilipatikana kinyume na sheria. Balozi Mattli, alisema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi, umekuwa ukiimarika zaidi kila siku, na kuwa nchi hiyo itaendelea kuisaidia Tanzania kwa hali na mali.

Chanzo: Habari Leo
Make Tanzania to be the Great again,come oooooon Tanzania.
 
Kuna watu huwa wanasema tunakwenda kwa matukio. Hii imefanywa ili watu wasahau matukio mengine. Lugumi ilikwenda weeeee ipo wapi? Escrow ilikwenda weeee sasa oko wapi? Kama tumeshindwa kukamata pesa ambazo zilikuwa kwenye mabenki yetu na majumbani hapa Tz unategemea hao wajinga muda wote huo si walishahamisha accounts. Mswizi hana biashara zaidi ya banking na kutengeneza saa sasa unafikiri yeye ale wapi? Pesa za Mobutu zilisharudi? Marais wote wa Nigeria wanasemekana waliwekeza huko je imekuwaje? Mtu pekee aliyeweza kutumia umafia na kunyang'anya watu wakubwa ujiko ni yule mjeshi wa Ghana Rawling aliyeamua kuwaua marais wote wa zamani na kutaifisha mali zao. Baada ya hapo unaona Ghana woga ukawapata sasa hivi ni nchi inasifika kwa utawala bora. Kwetu sisi ni kulindana. Ikiwa mswada wa habari tu umeleta maneno ya kuletwa itakuwa kitu utajiri wa vizazi na vizazi?
Yeye kashasema hafukui makaburi sasa hii mikataba nadhani itakuwa ni kwa hawa wapya watakaoficha hela huko nje

Assume vijana waende huko uswisi wakutane na salio la baba Riziii watagusa kitu au?

Hata akikuta za Dewji, sidhani kama hao uswisi wanapendaga ujinga
 
Pia wakaangalie na yule jamaa ambaye alikufa na kuzikwa marekani na familia yake tu kama alikufa kweli,au alikufa mtu mwingine akazikwa kwa jina la huyu aliyekimbilia kule,na wakikuta maiti wafanya sijui mnaiitaje wenyewe mlio soma me sijaui wathibitishe maiti kama ndiyo yenyewe!
 
Between the lines namaanisha huyu mwizi hawezi kukamata mwizi...hapambani na mafisadi papa huyu mtu,anaishia kwa vidagaa tu,lugumi na escrow hata kuvitaja anaogopa,nyinyi mnaamini blah blah zake!!zitto alishatoaga majina ya watu walioficha pesa nje,aanze na hayo!!!!
Hayo majina aliyoyataja yapo wapi hebu tutajie kama wewe ulishawahi kuyaona au kuyasikia. Kila siku alikuwa anatishia nyau wala hajawahi kuyataja.... :D:D:D:D
 
View attachment 429957

Serikali ya Tanzania na Uswisi zimesaini Mkataba utakaowawezesha Makachero wa Tanzania kwenda nchini Uswisi na kufanya uchunguzi katika mabenki ya huko ili kupata taarifa sahihi za walioficha mabilioni toka Tanzania.

Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr Augustine Mahiga na Balozi wa Uswisi nchini Florence Mattli

Hata hii ni moja ya hatua muhimu ya Serikali awamu ya tano katika kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma.
========================

HUKU kukiwepo na dhana ya kuwa kuna Watanzania wanaotorosha fedha na kuzificha katika mataifa mbalimbali ikiwemo Uswisi, hatua moja muhimu imefanyika katika kukabili suala hilo, baada ya serikali ya nchi hizo mbili, kusaini mkataba muhimu.

HabariLeo Jumapili imebaini kufikiwa kwa makubaliano ya ushirikiano muhimu wa kisheria kwenye masuala ya jinai, unaolenga kuwajengea uwezo makachero wa Tanzania, kuchunguza masuala mbalimbali ya kiuhalifu nchini Uswisi.

Mkataba huo umeenda mbali zaidi, kwa kuweka wazi kuwa kuanzia sasa makachero hao, wanaweza kuchunguza fedha za Watanzania zilizohifadhiwa nchini Uswisi, tofauti na awali ambapo sheria za nchi hiyo zilikuwa zinazuia.

Mkataba huo umesainiwa hivi karibuni wakati wa Maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi. Uswisi ni nchi inayosifiwa kuwa na huduma bora za kibenki huku ikiwa na sheria kali zinazowalinda wateja wake.

Mkataba wa makubaliano hayo, ambao umeleta mwanga katika kukabiliana na usiri wa fedha hizo, ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga na Balozi wa Uswisi nchini, Florence Mattli.

Akizungumza na gazeti katika mahojiano maalumu kuhusu mkataba huo, Balozi Mahiga alisema kuwa katika kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo, Tanzania itanufaika na ruhusa hiyo ya kufuatilia akaunti za fedha Uswisi.

Alisema kuwa kipengele hicho, kimekubaliwa kwenye makubaliano na kwa sasa hakuna tena kikwazo kitakachoizuia Tanzania kuchunguza akaunti hizo.

Alisema kuwa hatua hiyo inatokana na Serikali ya Uswisi pia kuridhishwa na namna ambavyo Tanzania imekuwa ikipambana na vitendo vya rushwa na ufisadi, kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wake chini ya uongozi wa Rais John Magufuli.

Alisema, Uswisi imekuwa ni rafiki mkubwa wa Tanzania tangu enzi na enzi huku ikiisaidia katika uboreshaji wa sekta mbalimbali.

“Kweli hiyo ni hatua nzuri kwa Tanzania hasa kwa kipindi hiki ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikikabiliana na rushwa na kila aina ya ufisadi na kwa hiyo ruhusa hii itasaidia kulinda fedha zetu kutoroshwa,” alisema Balozi Mahiga.

Akijibu swali ni lini serikali itakuwa tayari kupeleka makachero nchini humo, kuchunguza madai ya kuwepo kwa Watanzania walioficha fedha kwenye benki za nchini humo, Balozi Mahiga alisema; “Siwezi kusema ni lini hatua hiyo inaweza kuanza kuchukuliwa kwa kuwa zipo mamlaka zinazohusika na utekelezaji wake, ila ninachoweza kusema ni kuwa hatua iliyofikiwa ni ya msingi kwetu kama nchi.”

Zitto apongeza Mkataba Akitoa maoni yake kuhusu makubaliano hayo, Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT – Wazalendo ), mmoja wa wabunge ambaye amekuwa akilizungumzia suala la ufichwaji wa mabilioni ya fedha nje ya nchi, aliliambia gazeti hili kuwa kipengele hicho kwenye mkataba huo ni kizuri na kitasaidia kupatikana kwa fedha zilizofichwa katika benki za Uswisi.

Alitumia nafasi hiyo kuipongeza serikali kwa uamuzi huo uliofikiwa na kusema ni hatua ya kimafanikio, hasa ikizingatiwa kuwa fedha hizo zinatokana na nguvu za wanyonge, ambapo pia zilipatikana kinyume na sheria. Balozi Mattli, alisema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi, umekuwa ukiimarika zaidi kila siku, na kuwa nchi hiyo itaendelea kuisaidia Tanzania kwa hali na mali.

Chanzo: Habari Leo
Ile orodha tulipewa na mh ZZK, imetupa somo ni kwa kiasi gani wanasiasa wanavyopenda kutuandaa kuamini ktk alinacha...wengi tukitegemea majina ya wale ambao wanasiasa hao hao wakitwambia ni mafisadi, lkn duh....orodha ilijumuisha mpaka watanzania wenye kuishi na kufanya mambo halali na fedha zao halali ughaibuni
 
tupongeze kwa step moja, tusubiri utekelezaji wake. swiss imekuwa kikwazo kwa miongo kadhaa kwa sheria zao za usiri wa wateja, ikumbukwe wateja wao wengi ni viongozi, wanasiasa na wafanyabiashara toka africa wamepata hela kwa njia zisizo halali, rais abacha wa nigeria alificha hela na hakuwahi kuzitoa hadi mauti yakamkuta. hilo ni tatizo lingine linalohitaji mjadala mpana 'as to why african leaders hide their money in swiss' ni kivipi serikali itanufaika na hiyo treaty tusubiri tuone. sasa waongeze wigo na kusign na nchi zingine ili wakose pa kuzipeleka
 
Pia nafikiri huyo mwandishi wa Habari Leo kashindwa kutafsiri vizuri juu ya kilichokubaliwa. Habari kamili inapatikana katika tovuti ya Ubalozi wa Uswisi Tanzania.
Katika hiyo taarifa, kuna hili limeandikwa:

"The memorandum does not create any new right or obligations with regard to international mutual assistance in criminal matters, but it does introduce some key administrative and organizational changes to ensure efficient cooperation."

Soma habari yote hapa chini:

Switzerland and Tanzania Sign Agreement on Mutual Legal Assistance in Criminal Matters
Media release, 21.10.2016

As Switzerland and Tanzania mark 50 years of diplomatic relations today, the two countries are planning to work more closely together in the fight against international crime. A Memorandum of Understanding on international mutual assistance in criminal matters was signed by Hon. Dr. Augustine Mahiga, Minister for Foreign Affairs, East Africa Regional and International Cooperation and Swiss Ambassador to Tanzania H.E. Florence Tinguely Mattli.
cq5dam.thumbnail.588.368.png

Minister Mahiga Mahiga and Ambassador Tinguely Mattli shake hands after signing the agreement © FDFA
Switzerland is committed nationally and internationally to fight against illicit financial flows, like money laundering and terrorist financing. The Memorandum of Understanding signed today is intended to support the Tanzanian government in its efforts to combat corruption. The memorandum does not create any new right or obligations with regard to international mutual assistance in criminal matters, but it does introduce some key administrative and organizational changes to ensure efficient cooperation. In particular, central authorities of both states will be able to deal with each other directly and support each other in the drafting of requests for legal assistance in future. The appendix to the memorandum also includes model requests which satisfy the formal requirements of both states.

In her remarks, Ambassador Tinguely Mattli said the MoU marks the starting point into a new era of bilateral cooperation between Switzerland and Tanzania. “Switzerland is willing to support the Government of Tanzania in its fight against corruption, which is key for economic development. By signing this important agreement today as we celebrate 50 years of bilateral cooperation, we decide to further strengthen our ties of friendship, cooperation and mutual confidence.”

Source: News
 
Back
Top Bottom