kitako cha sufuria
Member
- Nov 1, 2016
- 78
- 24
Tusaini pia na mkataba wa kuwawezesha makachero wetu kwenda ile nchi kuangalia kama mv dar es salaam ilikuwa mpya au mtumba na kurudishiwa chetu kama ni mtumba.
Tusaini pia na mkataba wa kuwawezesha makachero wetu kwenda ile nchi kuangalia kama mv dar es salaam ilikuwa mpya au mtumba na kurudishiwa chetu kama ni mtumba.
hili ni zao la elimu yetu mbovuNina amini Tanzania tunaweza kulinda na kutetea maslahi yetu huko nje. Je unafikiri hatuna makachero mahili wa kuweza kufanya kazi ya kusaka pesa zetu huko uswisi?. Hivi hakuna watanzania wowote wanaofanya kazi katika mashirika makubwa ya kikachero huko ulaya na marekani?. Hivi ni mara ya kwanza tanzania kufuatilia pesa huko ng'ambo? hujawahi kusikia kwamba account flani flani miaka ya 90 huko huko uswisi ziliwahi kufungwa kwa maslahi ya Taifa ni nani aliyefanikisha?
Tutunze maneno haya tutakuja kumbushana. Nasisitiza si kila kitu unaweza kubeza kwa sababu tu uko UKAWA.CCM, CUF Chadema nk. Tuwape muda serikali hii ni makini na inajua nini inafanya. Mimi ninafikiri tunajishaua tu hatukuambiwa kwamba kuna mkataba wanaingia na nchi ya uswisi ila sisi kwa mtazamo wetu mbaya tunajitoa ufahamu kwamba hichi ni kiini macho kivipi? Tushikamane na muda utafika nchi hii itakuwa na neema na uchumi mzuri zaidi Afrika na dunia nzima.
Nadhani za stanbic Bank zipo ktk track ktk ufuatiliaji,Za Escrow nakumbuka Bunge lilitoa maazimio.Na za Uswisi taratibu kwa mashirikiano ya Serikali zote mbili tutafika pazuri tuNASISITIZA, TAMBUA ZILIZOFICHWA HAPO STANBIC BANK KUTOKA ESCROW KWANZA. HUWEZI KUSHINDWA KUJUA ZA NYUMBANI UKAJUA ZILIZO NJE YA NCHI, VIPIIIII? AU MAIGIZO?
hapana bwana ila kama ni jina la Rais anaitwa Dr John Joseph Pombe Magufuli na kama ni chama chake ni Chama Cha Mapinduzi,nchi huru na una uhuru wa kutoa maoni yako katika kujenga nchi,kumbuka bado tuna safari ndefu sana katika kufikia maendeleo ya kweli.tulia wewe umeshalishwa sumu kaa chini ikumalize
Salama chifu.Chief, salama lakini?
Mimi pia nimeona hiyo taarifa lakini kwa uelewa wangu ni kwamba kutakuwa na ushirikiano kwenye "administrative na key organizational changes" ili kuwezesha ufanisi kwenye ushirikiano.
Sasa hii administrative na key organizational changes inamaanisha kwamba kutakuwa na vitengo maalum upande wa Tanzania na Switzerland ambavyo vitashirikiana kwenye utekelezaji au administrative issues kama hiyo ya suala la fedha ambazo kama zipo ndani ya benki za huko wao Switzerland watawajibika kusaidia kufahamu ziliingiaje.
Kwa hiyo ushirikiano ni kwenye sheria, forensic accounting na auditing na pale wanapohitaji msaada kama kutoa notice basi wanazungumza na wizara ya fedha.
Hivyo haijalishi ni lini fedha zisizo halali ziliingia kwenye mabenki nchini humo lakini makubaliano ya leo hayakuja tu.
Makubaliano ya leo yalianza na mazungumzo mwezi March mwaka jana na unaweza kusoma hapo chini sehemu yake:
"Approved by the Federal Council on 13 March 2015, the memorandum of understanding is intended in particular to support the Tanzanian government in its efforts to combat corruption. These efforts are also in the interests of a clean Swiss financial centre. The memorandum does not create any new rights or obligations with regard to international mutual assistance in criminal matters, but it does introduce some key administrative and organisational changes to ensure efficient cooperation. In particular, in the future the central authorities of both states (in Switzerland's case the Federal Office of Justice) will be able to deal with each other directly and support each other in the drafting of requests for legal assistance. The appendix to the memorandum also includes model requests which satisfy the formal requirements of both states."
Hivyo inaonekana hili suala lilizimwa ghafla mwaka jana na baada ya Swistzerland kuona juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kupambana na rushwa na mambo mengine ya kudhibiti fedha, ndiyo wakaamua kujikumbusha hii kitu ya mwaka jana.
Hata hivyo Switzerland wamekuwa wakitoa ushirikiano na nchi kadhaa katika kufahamu kama wananchi wanalipa kodi kabla ya kuweka fedha huko.
Mwaka jana mwezi wa 11, raia wa Ugiriki walichunguzwa katika taarifa hiyo hapo chini:
Nchi zingine kama Uingereza nao wamekubaliana tangu mwaka 2013 na Switzerland kushirikiana kwenye masuala ya kodi kufahamu wale raia ambao wanakwepa kodi nchini Uingereza na kuweka fedha zao huko Uswiss.
Mwaka huohuo Marekani nayo ilikubaliana na Uswiss kuwezesha kufuatiliwa wale awote ambao wameficha fedha huko katika habari hii:
Switzerland And United States Reach Agreement On Swiss Bank
Last Updated: October 18 2013
Mwaka 2010 Ujerumani nao walitaka orodha ya wakwepa kodi ambao wameficha fedha zao Geneva:
Swiss Bank Data Offered to Germany
Pressure Rises About Secret Accounts
Kesi hizi na zingine nyingi tu zipo arounbd tokea mwaka huohuo wa 2005 ambao umekuwepo huko Uswiss na ungeweza kufahamu kinachoendelea khasa masuala haya ya fedha za kutumwa kutoka nje.
Na katikati ya mwaka huu Jumuiya ya Ulaya walizungumza na Panama ili kutaka kushirikiana kwenye masuala khasa ya data sharing kuona ni watu wangapi khasa na thamani ya fedha walizo nazo huko Uswiss baada ya ile orodha ndeefu kutoka na TAKUKURU wanayo nakala..
Pia katikati ya mwaka tulisikia jinsi wachunguzi kutoka Marekani walivyoivamia FIFA mjini Geneva na kuwakamata baadhi ya maofisa wake baada ya kuchunguza accounts zao ambazo zikituna kwa muda mrefu sana.
Tumeshuhudia Sepp Blatter na Platini waliachia ngazi kutoka kwenye taasisi hiyo kubwa duniani yote hiyo ni baada ya makubaliano hayahaya ya hiki tunachokiona kikifanywa na nguli wa diplomasia Dr Mahiga na waswiss.
Ukiangalia msururu huo wa kesi hizo utaona kwamba zote zinalingana kwenye administyrative issues na hiyo ndiyo key.
Hivyo kwa Tanzania ni hatua kubwa sana na serikali ya awamu ya tano inasogea kidogokidogo kuelekea kuwatambua wale ambao waliiba fedha au kufanya ufisadi na wameficha hizo fedha huko Uswiss.
Kama Serikali ya tz inadhani au inafikiri kuna Nchi itakubali mabilioni yaondolewe kizembe kwenye mabenki yao basi watakua wanaota ndoto za mchana, actually watakua wanaota ndoto nyevu. Tanzania lazma waweke kitu kingine mezani ili situation iwe win win. Mahiga awe makini asije kua kama Membe ambaye alishindwa kuweka offer nzuri mezani kwenye suala la chenchi ya rada tukaishia kupewa vitabu.View attachment 430265
Serikali ya Tanzania na Uswisi zimesaini Mkataba utakaowawezesha Makachero wa Tanzania kwenda nchini Uswisi na kufanya uchunguzi katika mabenki ya huko ili kupata taarifa sahihi za walioficha mabilioni toka Tanzania.
Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr Augustine Mahiga na Balozi wa Uswisi nchini Florence Mattli.
Hata hii ni moja ya hatua muhimu ya Serikali awamu ya tano katika kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma.
========================
HUKU kukiwepo na dhana ya kuwa kuna Watanzania wanaotorosha fedha na kuzificha katika mataifa mbalimbali ikiwemo Uswisi, hatua moja muhimu imefanyika katika kukabili suala hilo, baada ya serikali ya nchi hizo mbili, kusaini mkataba muhimu.
HabariLeo Jumapili imebaini kufikiwa kwa makubaliano ya ushirikiano muhimu wa kisheria kwenye masuala ya jinai, unaolenga kuwajengea uwezo makachero wa Tanzania, kuchunguza masuala mbalimbali ya kiuhalifu nchini Uswisi.
Mkataba huo umeenda mbali zaidi, kwa kuweka wazi kuwa kuanzia sasa makachero hao, wanaweza kuchunguza fedha za Watanzania zilizohifadhiwa nchini Uswisi, tofauti na awali ambapo sheria za nchi hiyo zilikuwa zinazuia.
Mkataba huo umesainiwa hivi karibuni wakati wa Maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi. Uswisi ni nchi inayosifiwa kuwa na huduma bora za kibenki huku ikiwa na sheria kali zinazowalinda wateja wake.
Mkataba wa makubaliano hayo, ambao umeleta mwanga katika kukabiliana na usiri wa fedha hizo, ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga na Balozi wa Uswisi nchini, Florence Mattli.
Akizungumza na gazeti katika mahojiano maalumu kuhusu mkataba huo, Balozi Mahiga alisema kuwa katika kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo, Tanzania itanufaika na ruhusa hiyo ya kufuatilia akaunti za fedha Uswisi.
Alisema kuwa kipengele hicho, kimekubaliwa kwenye makubaliano na kwa sasa hakuna tena kikwazo kitakachoizuia Tanzania kuchunguza akaunti hizo.
Alisema kuwa hatua hiyo inatokana na Serikali ya Uswisi pia kuridhishwa na namna ambavyo Tanzania imekuwa ikipambana na vitendo vya rushwa na ufisadi, kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wake chini ya uongozi wa Rais John Magufuli.
Alisema, Uswisi imekuwa ni rafiki mkubwa wa Tanzania tangu enzi na enzi huku ikiisaidia katika uboreshaji wa sekta mbalimbali.
“Kweli hiyo ni hatua nzuri kwa Tanzania hasa kwa kipindi hiki ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikikabiliana na rushwa na kila aina ya ufisadi na kwa hiyo ruhusa hii itasaidia kulinda fedha zetu kutoroshwa,” alisema Balozi Mahiga.
Akijibu swali ni lini serikali itakuwa tayari kupeleka makachero nchini humo, kuchunguza madai ya kuwepo kwa Watanzania walioficha fedha kwenye benki za nchini humo, Balozi Mahiga alisema; “Siwezi kusema ni lini hatua hiyo inaweza kuanza kuchukuliwa kwa kuwa zipo mamlaka zinazohusika na utekelezaji wake, ila ninachoweza kusema ni kuwa hatua iliyofikiwa ni ya msingi kwetu kama nchi.”
Zitto apongeza Mkataba Akitoa maoni yake kuhusu makubaliano hayo, Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT – Wazalendo ), mmoja wa wabunge ambaye amekuwa akilizungumzia suala la ufichwaji wa mabilioni ya fedha nje ya nchi, aliliambia gazeti hili kuwa kipengele hicho kwenye mkataba huo ni kizuri na kitasaidia kupatikana kwa fedha zilizofichwa katika benki za Uswisi.
Alitumia nafasi hiyo kuipongeza serikali kwa uamuzi huo uliofikiwa na kusema ni hatua ya kimafanikio, hasa ikizingatiwa kuwa fedha hizo zinatokana na nguvu za wanyonge, ambapo pia zilipatikana kinyume na sheria. Balozi Mattli, alisema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi, umekuwa ukiimarika zaidi kila siku, na kuwa nchi hiyo itaendelea kuisaidia Tanzania kwa hali na mali.
Chanzo: Habari Leo
Huu sasa ni Uchochezi wa wazi wazi. Qwi Qwi Qwi Qwi......Mkataba wa Australia kuchunguza Simba Trust
Mazito hayo tena,nadhani Dr Mahiga ni Diplomat mzoefu sana ktk medani hizo za kijasusi he knows what is doing! Na hili suala ni multi sectoral,ondoa shaka, let's give them time na tusubiri matokeo.Kama Serikali ya tz inadhani au inafikiri kuna Nchi itakubali mabilioni yaondolewe kizembe kwenye mabenki yao basi watakua wanaota ndoto za mchana, actually watakua wanaota ndoto nyevu. Tanzania lazma waweke kitu kingine mezani ili situation iwe win win. Mahiga awe makini asije kua kama Membe ambaye alishindwa kuweka offer nzuri mezani kwenye suala la chenchi ya rada tukaishia kupewa vitabu.
baba alishasema anaanzia alipopakuta hayo yaliyopita kufa nayo wewe. kama ni makaburi kachimbue wewe mikono c unayoBetween the lines namaanisha huyu mwizi hawezi kukamata mwizi...hapambani na mafisadi papa huyu mtu,anaishia kwa vidagaa tu,lugumi na escrow hata kuvitaja anaogopa,nyinyi mnaamini blah blah zake!!zitto alishatoaga majina ya watu walioficha pesa nje,aanze na hayo!!!!
Mbona richmond wanalipwa hadi kesho,mbona escrow tunalipia na juzi tumeshindwa kesi na januari majizi tanesco yanapandisha bei ya umeme kulipa deni...unaongea ujinga gani wewe!!!!?baba alishasema anaanzia alipopakuta hayo yaliyopita kufa nayo wewe. kama ni makaburi kachimbue wewe mikono c unayo
Yap, mimi nampa worning tu. Tujifunze kwa Iran. Mabilioni ya serikali ya Irani yalikuwa freezed marekani kutokana na vikwazo. Baada ya vikwazo Irani ikajua kabisa there is no way US akakubali pesa yoote iondoke hivi hivi so akaamua kununua ndege 400. So na sisi tuwe makini na mikakati yetu.Mazito hayo tena,nadhani Dr Mahiga ni Diplomat mzoefu sana ktk medani hizo za kijasusi he knows what is doing! Na hili suala ni multi sectoral,ondoa shaka, let's give them time na tusubiri matokeo.
OK I know that about Iran,na kwa Dr Mahiga hopeful precaution zote zitakuwa zimeangaliwa kwa umakini sana leading to reach the desired target ktk makubaliano yaliyowekwa.Yap, mimi nampa worning tu. Tujifunze kwa Iran. Mabilioni ya serikali ya Irani yalikuwa freezed marekani kutokana na vikwazo. Baada ya vikwazo Irani ikajua kabisa there is no way US akakubali pesa yoote iondoke hivi hivi so akaamua kununua ndege 400. So na sisi tuwe makini na mikakati yetu.
wewe acha ushamba hukumu za mahakama huwezi ingilia. hayo maden yalishatolewa hukumu na tanzania lazima kulipa. basi kama ndo hivyo na deni la taifa lisilipwe maana hajakopa makugufuli. mbona ulisemi na hilo.Mbona richmond wanalipwa hadi kesho,mbona escrow tunalipia na juzi tumeshindwa kesi na januari majizi tanesco yanapandisha bei ya umeme kulipa deni...unaongea ujinga gani wewe!!!!?
tunalipia pesa iliyoibiwa wazi na magu anajua hilo,swala sio mahakama swala tunalazimika kulipia hela zilizopigwa na maccmwewe acha ushamba hukumu za mahakama huwezi ingilia. hayo maden yalishatolewa hukumu na tanzania lazima kulipa. basi kama ndo hivyo na deni la taifa lisilipwe maana hajakopa makugufuli. mbona ulisemi na hilo.
ata kama zimeibiwa maamuzi ya mahakama lazima yafatwe. magufuli kaingia hukumu tayari ishatolewa, sasa we unataka akatae maamuzi ya mahakamawewe acha ushamba hukumu za mahakama huwezi ingilia. hayo maden yalishatolewa hukumu na tanzania lazima kulipa. basi kama ndo hivyo na deni la taifa lisilipwe maana hajakopa makugufuli. mbona ulisemi na hilo.