Waziri Magufuli amelidanganya Bunge

Waziri Magufuli amelidanganya Bunge

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,506
Nipo hapa nikisikiliza hotuba ya Bajeti ya wizara ya Ujenzi inayosomwa na Waziri John Magufuli. katika hotuba yake ameliambia Bunge sasa hivi kuwa UJENZI WA BARABARA YA LAMI KUANZIA TABATA DAMPO HADI KIGOGO UNAENDELEA.

Jamani mimi ni mtumiaji wa kila siku wa barabara hii ya Tabata Dampo Kigogo nikitokea Tabata Segerea kuelekea Mjini kwenye shughuli zangu. Mara ya mwisho nimepita leo hii jioni. ukweli ni kwamba WAZIRI AMELIDANGANYA BUNGE na hakuna hata dalili za kuwepo kwa ujenzi wa barabara ya lami zaidi ya kuharibika vibaya kwa barabara hiyo.

Nawaomba wabunge wa dar es salaam kusimama kidete kupinga uongo huu wa Magufuli ambao hauna faida kwa wananchi. Mnyika na Mbunge wa Kinondoni Idd Azan tafadhalini hakikisheni mnamwambia ukweli Magufuli kuwa amewadanganya wananchi na taifa lote kwa ujumba.
 
Mkuu Mwana Mpotevu, mimi hushangazwa tu pale viongozi wa Serikali na CCM wanaposema ukweli.Uongo nimeshazoea.Halafu wanakuwa 'wakavu' kweli kweli. Na hushangaa mara zisizozidi tano kwa mwaka

kwakweli inauma sana mtu unapodanganywa huku ukijua kuwa unadanganywa. Wanachokifanya akina Magufuli kutudanganya namna hii sio vizuri hata kidogo
 
Nipo hapa nikisikiliza hotuba ya Bajeti ya wizara ya Ujenzi inayosomwa na Waziri John Magufuli. katika hotuba yake ameliambia Bunge sasa hivi kuwa UJENZI WA BARABARA YA LAMI KUANZIA TABATA DAMPO HADI KIGOGO UNAENDELEA.

Jamani mimi ni mtumiaji wa kila siku wa barabara hii ya Tabata Dampo Kigogo nikitokea Tabata Segerea kuelekea Mjini kwenye shughuli zangu. Mara ya mwisho nimepita leo hii jioni. ukweli ni kwamba WAZIRI AMELIDANGANYA BUNGE na hakuna hata dalili za kuwepo kwa ujenzi wa barabara ya lami zaidi ya kuharibika vibaya kwa barabara hiyo.

Nawaomba wabunge wa dar es salaam kusimama kidete kupinga uongo huu wa Magufuli ambao hauna faida kwa wananchi. Mnyika na Mbunge wa Kinondoni Idd Azan tafadhalini hakikisheni mnamwambia ukweli Magufuli kuwa amewadanganya wananchi na taifa lote kwa ujumba.

mbona anasifiwa sana ka jembe la ukweli na mnamtaka awe rais
 
Kwa propaganda na kupanda chuki haujambo.

kweli mkuu. ile barabara leo jioni kabla hajaenda bungeni si tulimuona Magufuli mwenyewe kashika koleo kuimalizia? isingekuwa kwenda bungeni kusoma budget yake, pengine angekuwa keshaimalizia kabisa.
 
Hiyo barabara ni mbaya sana
cc
magufuli

Ni kweli kabisa nashukuru nawe unajua kuwa barabara hii ni mbaya sana. Tatizo Waziri anayeitwa Jembe anatudanganya anasema eti inaendelea kuwekewa lami hivi sasa na kuwa kazi ilishaanza tangu mwaka jana. Hivi kweli tunadanganywa kweupe namna hii????
 
Yani makufuli ni moja ya wanasiasa wanaofanya siasa yepesi sana
Eti mtu kama makufuli naye anandoto za kuja kuwa rais wa nchi hii
Siku ikitokea hivyo nabadili uraia nachukuwa wa somalia
 
Yani makufuli ni moja ya wanasiasa wanaofanya siasa yepesi sana
Eti mtu kama makufuli naye anandoto za kuja kuwa rais wa nchi hii
Siku ikitokea hivyo nabadili uraia nachukuwa wa somalia

Nachukua maelezo yako haya kwa uangalifu mkubwa sana
 
Huo ni uongo uliopitiliza, kabla mvua hazijaanza kuna mkandarasi alikua anaweka kifusi, alikua anafanya kazi chini ya kiwango bahati yake mvua ikaanza na nazani ndo amepata kisingizio, kwa vyovyote atasema alishamaliza kazi ila mafuriko ndo yakaharibu...
 
Mbunge wa Segerea Dr.Makongoro Mahanga(Bila kuhoji Authenticity ya Ph.D yake hiyo) ameonyesha jinsi asivyokuwa Muwakilishi sahihi wa Jimbo la Segerea kwa kukaa kimya na kumuangalia Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli akidanganya kuhusu ujenzi wa barabara ya Tabata Dampo kuelekea Kigogo

Magufuli anasema ujenzi unaendelea wakati ukweli ni kuwa hakuna Ujenzi wowote unaoendelea na Barabara hiyo huwa ninaitumia

Waziri Magufuli aliyejijengea aura ya kuwa Waziri Mchapakazi mwenye uwezo wa kumeza na kutema Takwimu anadanganya bila aibu?

Je,katika Takwimu zote alizowahi kutoa ,tutaweza vipi kuziamini ?Inawezekana ameshadanganya sana kwa staili hii na ukizingatia Watanzania wengi sisi ni waoga wa Takwimu au Tarakimu

Mbunge wa Segerea amekaa kimya wakati uongo na upotoshaji huu ukiendelea

Ni matarajio yangu kuwa sasa Magufuli ataomba Radhi kwa Uongo huu ndani ya Bunge na kwa wananchi wa Jimbo la Segerea

Si vyema kuleta excuse kuwa waziri kadanganywa na wasaidizi wake.Maana kama this is the case basi credibility yake ipo mashakani na reliability ya Hoja na Takwimu zake anazotoa Bungeni ni ya kutiliwa mashaka

Aluta Continua,Victory Ascerta....!
 
Yani makufuli ni moja ya wanasiasa wanaofanya siasa yepesi sana
Eti mtu kama makufuli naye anandoto za kuja kuwa rais wa nchi hii
Siku ikitokea hivyo nabadili uraia nachukuwa wa somalia

Kitendo chako cha kumbagua Magufuli nami nasema haitakuja tokea mchaga akawa president wa Tangayika na Tanzania
 
Wengine hatukusikia jamani, vipi barabara za Tabora amesemaje? Ile ya Nzega - Tabora na ile ya Tabora-Itigi?
 
Kitendo chako cha kumbagua Magufuli nami nasema haitakuja tokea mchaga akawa president wa Tangayika na Tanzania

Uwezo wako wa kufikiri ni finyu sana
Unaongea ukabila karne hii sio kosa lako
Mchaga ndio mtu amekuwa akileta changamoto kwenye siasa za tz toka tunapata uhuru
Na mpaka leo fanya tathimini ni wachaga wangapi wapo kwenye siasa na wanaifanya ccm hailali
Si niya yangu kukupa uwezo wa mchaga kwenye siasa za tanzania
Ila nimejaribu kukutoa kwenye ujinga uliyotawala akili yako kuhusu wachaga
Jifunze kujenga hoja au kujibu bila kuhusisha ukabila na udini ili tuweze kukuamini kile unachokisimamia usiwe na damu ya nape utafeli mkuu
 
Back
Top Bottom