Waziri Mabula: Hatuhitaji miji iliyojaa fremu za maduka. Mipango miji izingatiwe

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,997
50,715
Hongera Waziri Kwa kukuona hili,na Ili kuweza kusimamia vizuri master plan za Miji Serikali Ianzishe Wakala au Mamlaka ya Kusimamia Upangaji Miji na Ardhi yaani Town Planning and Land Administration Authority..


Kiukweli Miji yetu inatia aibu na hasira sana yaani utadhani sisi sio binadamu wenye utashi tunaishi hovyo hovyo kama Wanyama..

Kwa nini mnashindwa kupanga Miji na kupima Ardhi Kwa Ajili ya Matumizi Bora? Tunazidiwa Hadi na Burundi,Somalia,Malawi nk..

Ccm muwe na aibu , hatuwezi kuendelea Kwa utaratibu huu wa Ujenzi wa hivyo hovyo..

Mgombea atayeweka ajenda hii mbele ndio nitampa kura yangu..
 
Umeongea point sana mkuu ... tatizo hutasikia mwana siasa Toka ccm akizungumzia hili suala

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi hili jambo Lina maslahi gani kwao?

Mfano kwani kuchukua makazi ya slums Kwa kujenga na kuwapa watu floors za Juu huku Serikali ilichukua za chini Kwa Ajili ya biashara Kuna shida gani? Au mnagwana na wenye maeneo Kwa kulipa mdogo mdogo Kuna shida?

Kupima maeneo ya watu na kuyawekea master plan kwamba uendelezaji uzingatie Mpango Mji Kuna shida? Maana shamba linapimwa na linaachwa ila any kind of uendelezaji lazima ufuate ramani Kuna shida hapo?

Sijawahi waelewa ccm Kwa hili kiukweli na wananikera sana,to be honest kama hakuna atakayekuja na idea hii Wala sitokusumbua hata kuwasikiliza.

Haiwezekani binadamu tuwe tunaishi kama mifugo,Ngorongoro wanahamisha watu huku wanashindwa nini?
 
Uwepo wa fremu nyingi ni matokeo ya uchumi wa uchuuzi na ukosefu wa ajira za viwandani matokeo yake vijana nguvu kazi wanakwenda kuwa wachuuzi wa bidhaa za wachina.

Taifa linatakiwa lijikite kwenye uchumi wa viwanda vikubwa na vidogo na sio uchuuzi.
 
uwepo wa fremu nyingi ni matokeo ya uchumi wa uchuuzi na ukosefu wa ajira za viwandani matokeo yake vijana nguvu kazi wanakwenda kuwa wachuuzi wa bidhaa za wachina.

Taifa linatakiwa lijikite kwenye uchumi wa viwanda vikubwa na vidogo na sio uchuuzi.
Viwanda vizingatie mipango Miji sio kujengwa hovyo hovyo kwenye makazi ya watu nk Kwa visingizio vya uchumi wa viwanda..
 
Kama waziri aonyeshe KWA mfano na sio kwa maneno. Kama wizara wanazidiwa hadi na kampuni binafsi za kuuza viwanja kwa kupanga mji. Ilitakiwa ardhi yote ipimwe, ramani uwepo ukitaka kiwanja unachagua.
Watangulize miundombinu kwanza KISHA watu ndio wafuate na sio miundombinu ndio ifuate watu.
 
[mention]mosekjng [/mention] usikubali jamaa kasema unashida ya kisaikolojia yaani kwa ufupi kasema wewe ni mwehu hebu mjibu na wewe, ukikubali utakua boya sana
 
Back
Top Bottom