Mamlaka za Mji wa Songwe zimelala, hakuna mikakati ya kupanga Mji, Wananchi wanajenga kiholela

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Mimi ni Mwenyeji wa Mkoa wa Songwe, mkoa mpya kuanzishwa wenye miaka takribani 7 tangia kuanzishwa kwake.

Hoja yangu ni kuwa tangu kuanzishwa kwa mkoa huu sijaona harakati zozote za wahusika yaani Serikali (Mipango Miji) kufanya upimaji wa eneo ambalo litakuwa ni makao makuu ya mkoa yaani kuwa na Master plan, hata utambuzi wa kimipaka wa eneo sina uhakika kama umefanyika.

Hali hiyo imesababisha Wananchi kuendelea na ujenzi holela, kama hali hii itaendelea kuwa hivi basi bila shaka huko mbeleni Wananchi watakutana na bomoabomoa au Serikali itatumia gharama kubwa kulipa Wananchi fidia pale itakapotaka kufanya maendeleo au miradi kwa jumla.

Ikiwa kama wana Master Plan inaweza kuokoa changamoto hiyo pamoja na gharama zinazoweza kujitokeza, pia inarudisha nyuma juhudi za maendeleo kwa kuwa Wananchi wanakuwa na wasiwasi katika kuanzisha miradi ya maendeleo kwa hofu kwamba miradi hiyo inaweza kuondolewa huko mbeleni.

Kwa kutambua kuwa mikoa mingi hapa Tanzania ilipangiliwa kipindi cha Ukoloni na kufanyiwa marekebisho baada ya Ukoloni.

Je, baada ya miaka zaidi ya 60 ya Uhuru, Serikali haioni haja ya kufanya mipangilio mizuri na ya kisasa ya Miji na Vijiji vyetu ili kuonesha kuwa Afrika hususani Tanzania tumestaharabika vya kutosha?

Ukienda kwenye nchi za wenzetu unakuta hadi sehemu za Vijijini zimepangiliwa vizuri. Tunaweza tusiwe na miundombinu mizuri kama wao lakini Je, hata suala la kupangalia vizuri matumizi ya ardhi yetu linatushinda?

Maafisa Mipango Miji na Vijiji wanafanya kazi gani? Wanafunzi na wataalam wanao hitimu kwenye vyuo vyetu wanafanya kazi gani?

Je, Serikali haioni kuwa ikipangilia vizuri Miji na Vijiji vyetu itaokoa gharama kubwa za ulipaji wa fidia pale itakapohitaji matumizi ya maeneo ambayo tayari yameshakaliwa na Wananchi?

Mwisho kabisa napenda kuwashauri, Afisa Mipango Miji Mkoa wa Songwe, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Kamishina wa Ardhi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Jerry Slaa), kuhusu hili kuwa wafanye upimaji na utambuzi wa kimipaka wa eneo ambalo ndiyo makao makuu ya Mkoa wa Songwe, sambamba na kuandaa Master Plan ya eneo hilo kwa manufaa ya Wanasongwe na Taifa kwa jumla.
 
Wewe umeandikaje heading Yako? Harafu Vwawa haijengwi hovyo hovyo bila Mpango kama Tunduma na Mlowo
Nilikuwa najaribu kuelezea kosa lililofanywa na mwandishi wa mada hii kama ambavyo wewe umeuliza kuhusu uwepo wa mji wa Songwe. Ukiangalia hapo juu utagundua hilo. Asante.
 
Hivi watendaji wa Kijiji na wenyeviti wa Kijiji na maDiwani kazi yao kubwa hasa ni nini?
 
Hivi kwanini hawapimi viwanja ntu akitaka anaend ardhi tuu anapata kuliko sasa mpaka mzee maiko akukatie shamba lake.
 
Back
Top Bottom