illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Kuna mgogoro mkubwa sana wa ardhi ambao unafukuta kwa zaidi ya miaka kumi sasa maeneo ya Kivule kata ya Msongola mtaa wa Mbondole. Kesi iko mahakama kuu divisheni ya ardhi, mlalamikaji anaitwa Sufiani Mbwambo ambaye anadai anamiliki takribani hekari 400 ambazo kwa sasa zote zina wakazi takribani kaya 20,000.
Hukumu ya kesi hii ni tarehe sita ambapo wiki iliyopita niliona wakitangaza kwenye taarifa ya habari Star TV na mijadala mingi imekuwa ikijadiwa kwenye majukwaa mbali mbali.
Binafsi nina kaeneo kangu kule hivyo kunifanya niwe na maslahi binafsi na kesi hii ambapo nilikwenda mpaka ofisi za manispaa nikaelekezwa kwa Municipal surveyor ili kupata taarifa za ndani, huyu bwana nilipomgusia tu hilo suala alinikwepa ilinibidi nimtafute boss wake ambaye aliniwekea miadi tukutane.
Tuliongee hili suala, tulifanikiwa kumpata municipal surveyor ambaye alionekana kutetea upande wa mlalamikaji ndipo badae nikaja kugundua hata mahakamani wanapokwenda huyu surveyor ndiye shahidi namba moja wa mlalamikaji, likanishtua kidogo ukweli nilioubaini ni kwamba mwenyekiti wa serikali za mtaa ameshirikiana na watendaji hawa wa manispaa wasio waaminifu kuipika hii kesi ambapo kila mwezi tunachangishwa fedha kwa ajili ya kuendesha kesi, kukodi wanasheria.
mpaka sasa tumechanga zaidi ya milioni 200 kwa miaka kumi iliyopita ukienda kwa mwenyekiti ama manispaa wanakwambia toa hela tukuunganishe na Sufiani Mbwambo ili eneo lako alitoe kwenye kesi, eneo lenyewe lina mchoro wa mpango mji namba TP NO ILA/MISC/70/62005.
Naona ni kama kuna mazingaombwe tunachezewa tunachangishwa hela mtu mmoja anasema anamiliki hekari 400 na siyo mwekezaji na Dar es salaam hakuna shamba bali maeneo yote ni makazi ya watu.
Hata hiyo mahakama sijui kwanini ina prolong hili jambo!! Wahusika tusaidieni maana kama haki haitatendeka sioni mwisho mwema.