Waziri Lukuvi badala ya kuwatishia Watanzania wa hali chini kichumi wawezeshe, si kila aliyepewa kiwanja ni fisadi au ana kipato kama wewe

Ndicho nilichouliza - walipokuwa wakigawa viwanja kwa nini hawakutuuliza kipato chetu ili ijulikane ni wanene tu waliotakiwa kugawiwa hivyo viwanja?
Ndo ujue hili linch lina vichwa mbovu.
Kimara-mbez-kibaha zilivunja nyumba za miaka ya 60, je hawakujua kuwa watu wamejenga barabarani? Ilipofika zamu ya mwanza oooooh hawa wasivunjiwe walinipigia kura mfuuuuu
 
Lengo la mh lukuvi sio kupora viwanja vya wananchi wanyonge sema sisi tunalichukulia kisiasa. Ilikuwa ni kawaida kwa watendaji wasio waaminifu wa wizara ya ardhi kujimilikisha viwanja ili waviuze kwa faida. Inaingia akilini mtu kapimia kiwanja, simu anayo anuani anayo eti anashindwa kufuata hati ya kiwanja chake wiizarani? Waziri amegundua ziwanja vingi vinamirikiwa na watendaji. Kwahiyo serikali inashindwa kukusanya kodi, maana hati za viwanja zipo wizarani. Na ndiyo maana akasema mwenye kiwanja amcho akijajengwa basi ajenge japo hata banda na kufanya usafi kwenye kiwanja. Na viwanja ambavyo wenyewe hawajajitokeza basi wapewe watu wengine ili serikali ikusanye kodi.
 
Tatizo sio Lukuvi ila sheria inataka uendeleze ndani ya miaka miwili. Ili kuepukana na hayo unaweka hata chumba kimoja au unazungusha ukuta.
 
Lengo la mh lukuvi sio kupora viwanja vya wananchi wanyonge sema sisi tunalichukulia kisiasa. Ilikuwa ni kawaida kwa watendaji wasio waaminifu wa wizara ya ardhi kujimilikisha viwanja ili waviuze kwa faida. Inaingia akilini mtu kapimia kiwanja, simu anayo anuani anayo eti anashindwa kufuata hati ya kiwanja chake wiizarani? Waziri amegundua ziwanja vingi vinamirikiwa na watendaji. Kwahiyo serikali inashindwa kukusanya kodi, maana hati za viwanja zipo wizarani. Na ndiyo maana akasema mwenye kiwanja amcho akijajengwa basi ajenge japo hata banda na kufanya usafi kwenye kiwanja. Na viwanja ambavyo wenyewe hawajajitokeza basi wapewe watu wengine ili serikali ikusanye kodi.
Mkuu, kodi ya kiwanja inatozwa hata kama hujakiendeleza!
 
Mkuu, kodi ya kiwanja inatozwa hata kama hujakiendeleza!
Tofautisha kodi ya jengo na koti ya ardhi, kodi yakiwanja kikishapimwa tu, inabidi utoe kodi ya ardhi na ndiyo maana waziri anasisitiza kupima ardhi ili serikali ipate kodi, sio maamuzi ya waziri hiyo ni kwa mujibu Wa sheria
 
Ukimiliki ardhi inabidi ulipie na ndiyo maana waziri anasisitiza kurasimisha ardhi, mila kipande cha ardhi kilichopimwa kitalipiwa kwa ukubwa wake hata makazi holela wanalazimishwa kupima viwanja vyao, ili serikali ikusanye modi.
 
Serikali ipi, hii ya Raisi Magufuli ambayo ukipatwa na janga la tetemeko wanakuambia imekula kwako?
Uzuri wa serijali hii hifanyi kazi kwa mazoea. Inaikiliza . Amen naawaambia hili litafanyiwa kazi. Mh. Lukuvi anafuata sheria , nadhani wotye tunajua unatakiwa kujenga ndani ya miaka mitatu huenda wengine hawajui hili! Lakini kwa kuanzai hapo miaka nmitatu ni michache mno ingeweka miaka 5 - 10. Aidha Hongerha saana Mh. Lukuvi unaFANYA kazi kubwa sana! Ila kwa hili nikushauri unavyozungumzia kuzungushia ukuta nadhani hujafanya mahesabu ya haraka haraka. Ni alot of money kwa mwananchi wa kawaida! Nashauri
1. Watu waambiwe wazungushie viwanja vyao kwa alama za miti au nguzo. ) hii iwe mpaka June 2020.
2. Kuanza kujenga- Ndani ya miaka 3 kuanzia sasa mtu aanze kujenga polepole.
Huu mradi ni wa mwaka 2002 kama sikosei hivyo ni miaka 17. Naelewa Mh. Lukuvi anawatafuta hasa wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi waliojilundikia viwanja bila kuvijenga. Naomba kuwasilisha.
 
Kwa hili usiwe na wasiwasi. Njia zimechongwa. Maji bwelele. Ila walionavyo waangaliwe kwanza wapewe muda as WaTZ tulikuwa tumezoea kuhshi kimazoea! Kiwanja miaka 20 hujakidevelop na aje huyo atakaekusemesha atakion cha mtema kuni. Watu wapewe muda ili wajue sasa sheria zinafanya kazi wasibweteke kama zamani!
 
Kila wakati Lukuvi anapenda kutoa tishio kwa Watanzania waliopewa viwanja na serikali kuwa watanyang'anywa kwa kuwa hawana uwezo wa kujenga. Yaani Lukuvi anachosema ni kwamba, hawakustahili kupewa hivyo viwanja kwa kuwa wao hali yao ya kuichumi iko chini na hawana uwezo wa kujenga haraka.

Ugawaji wa viwanja ulikuwa mpango wa serikali na wengi wa waliofaidika na mpango huu walikuwa watu wa kawaida kabisa ambao wanapambana na ugumu wa maisha ya kila siku. Wengi ni wafanyakazi wa serikali au mashirika ya umma wakitarajia watakapopata mafao ya kustaafu watajenga nyumba zao kwenye viwanja hivyo. Hakuna mtu mwenye kiwanja asiyependa kujenga nyumba, hilo liko wazi.

Lakini ajabu ni kwamba Lukuvi hafikirii hilo hata kidogo. Yeye anachojua kila mtu aliyepewa kiwanja ni fisadi mmoja ambaye ana mamilioni ya fedha kaweka mahali na sasa hataki tu kujenga nyumba kwenye kwanja alichopewa na serikali. Kuna wakati hata nafikiria kwamba Lukuvi anafikiri kwamba fedha anazopata kama mshahara na marupurupu kama waziri basi ndivyo ilivyo kwa Watanzania wote - na kwa kuwa yeye ana uwezo wa kujenga nyumba wakati wowote haelewi kwa nini Watanzania waliopewa viwanja washindwe kufanya hivyo.

Msimamo huu wa Lukuvi ni upofu wa hali halisi ya uchumi ya Watanzania kwa kuwa asilmia kubwa sana ya Watanzania, na hata hao waliopewa viwanja wanahangaika kulipa ada za shule za watoto, kulipia kodi ya nyumba, na hata chakula na mavazi. Hali hii imezidi kuwa ngumu katika awamu hii ya tano ambayo Lukuvi ni sehemu yake. Lukuvi haoni hilo, anachotaka ni Watanzania hao waache kuhangaikia ada na chakula ili wajenge hizo nyumba haraka sana. Kwanza tumuulize Lukuvi, je kwa upande wa serikali, imeshapeleka miundo mbinu kama barabara, maji na umeme katika maeneo haya, au bado viwanja hivi viko porini na serikali inachoona ni kibanzi katika macho ya waliogawiwa viwanja!

Ukweli ni kwamba watu wenye hela, huenda wengine ya ufisadi au mambo mengine, au vigogo kama Lukuvi mwenyewe, walishajenga siku nyingi sana. Na sasa labda Lukuvi atuambie, wakati serikali ikitekeleza mradi huu wa kugawa viwanja, nani hasa waliokuwa walengwa wa kupwa viwanja? Je walikuwa ni Watanzania mafisadi au wenye kipato kikubwa kama cha Lukuvi? Je yule mfanyakazi wa kawaida wa serikali anaesubiri mafao ili ajenge, hakustahili kupata kiwanja?

Kama Lukuvi angekuwa na uwezo mzuri wa kuona uhalisi wa mambo kama kiongozi wa wananchi ambao serikali ilitaka kuwasaidia kuwa na nyumba za kisasa, jambo ambalo angefanya badala ya kufoka watu watanyang'anywa viwanja kufikia December 2019, ni kuanzisha mpango wa mikopo nafuu ili watu wajenge. Tena mikopo hiyo isiwe na riba na itolewe kwa kutumia collateral ambayo ni mafao yaliyopo mifuko ya hifadhi. Ikibidi, taasisi hizo za hifadhi ya jamii ndio zitoe mikopo hiyo ya kujengea nyumba isiyo na riba. Benki kwa sasa zinatoza riba hadi 25%, Mtanzania gani wa kipato cha kawaida anaweza kukopa huko ili ajenge?

Lukuvi, asisahau yeye na viongozi wenzake awamu ya tano ni viongozi wa wananchi wote, wenye kipato kikubwa na kidogo. Anapaswa kupima mwenyewe kama ni halali kuwanyanganya viwanja wananchi wasio na uwezo wa kujenga ili kuwapa wananchi wenye uwezo wa kifedha, badala ya kuwawezesha ili waweze kujenga nyumba za kisasa.

Lukuvi hapaswi kuwapigia kelele za kuwanyang'anya wananchi viwanja wakati hujafanya lolote kuwasiaidia kujenga katika hivyo viwanja. Inafanya tutilie shaka lengo lake hasa hapa yeye na viongozi wenzake kuhusu hivyo viwanja. Usikute wanataka kuwanyang'anya wananchi hivyo viwanja ili wagawane kama walivyogawana nyumba za serikali huko nyuma!

UMENENA SAHIHI KABISA. NAAMINI MH. LUKUVI ATAUSOMA NA KUUTENDEA KAZI UJUMBE HUU MURUA, IKIZINGATIWA WAMEKUWA WAKIJINASIBU KUWA HII NI "SERIKALI SIKIVU".
 
Uzuri wa serijali hii hifanyi kazi kwa mazoea. Inaikiliza . Amen naawaambia hili litafanyiwa kazi. Mh. Lukuvi anafuata sheria , nadhani wotye tunajua unatakiwa kujenga ndani ya miaka mitatu huenda wengine hawajui hili! Lakini kwa kuanzai hapo miaka nmitatu ni michache mno ingeweka miaka 5 - 10. Aidha Hongerha saana Mh. Lukuvi unaFANYA kazi kubwa sana! Ila kwa hili nikushauri unavyozungumzia kuzungushia ukuta nadhani hujafanya mahesabu ya haraka haraka. Ni alot of money kwa mwananchi wa kawaida! Nashauri
1. Watu waambiwe wazungushie viwanja vyao kwa alama za miti au nguzo. ) hii iwe mpaka June 2020.
2. Kuanza kujenga- Ndani ya miaka 3 kuanzia sasa mtu aanze kujenga polepole.
Huu mradi ni wa mwaka 2002 kama sikosei hivyo ni miaka 17. Naelewa Mh. Lukuvi anawatafuta hasa wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi waliojilundikia viwanja bila kuvijenga. Naomba kuwasilisha.
Hilo la kuwatafuta watumishi wasio waadilifu ndilo lengo lake kuu, watendaji walikuwa wanapima kisha wanajimilikisha akitokea mteja wanauza. Sasa hili la kumiliki kiwanja na kitambulisho cha taifa chupi zinawabana.
 
Back
Top Bottom