Waziri Lukuvi badala ya kuwatishia Watanzania wa hali chini kichumi wawezeshe, si kila aliyepewa kiwanja ni fisadi au ana kipato kama wewe

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,929
2,000
Kila wakati Lukuvi anapenda kutoa tishio kwa Watanzania waliopewa viwanja na serikali kuwa watanyang'anywa kwa kuwa hawana uwezo wa kujenga. Yaani Lukuvi anachosema ni kwamba, hawakustahili kupewa hivyo viwanja kwa kuwa wao hali yao ya kuichumi iko chini na hawana uwezo wa kujenga haraka.

Ugawaji wa viwanja ulikuwa mpango wa serikali na wengi wa waliofaidika na mpango huu walikuwa watu wa kawaida kabisa ambao wanapambana na ugumu wa maisha ya kila siku. Wengi ni wafanyakazi wa serikali au mashirika ya umma wakitarajia watakapopata mafao ya kustaafu watajenga nyumba zao kwenye viwanja hivyo. Hakuna mtu mwenye kiwanja asiyependa kujenga nyumba, hilo liko wazi.

Lakini ajabu ni kwamba Lukuvi hafikirii hilo hata kidogo. Yeye anachojua kila mtu aliyepewa kiwanja ni fisadi mmoja ambaye ana mamilioni ya fedha kaweka mahali na sasa hataki tu kujenga nyumba kwenye kwanja alichopewa na serikali. Kuna wakati hata nafikiria kwamba Lukuvi anafikiri kwamba fedha anazopata kama mshahara na marupurupu kama waziri basi ndivyo ilivyo kwa Watanzania wote - na kwa kuwa yeye ana uwezo wa kujenga nyumba wakati wowote haelewi kwa nini Watanzania waliopewa viwanja washindwe kufanya hivyo.

Msimamo huu wa Lukuvi ni upofu wa hali halisi ya uchumi ya Watanzania kwa kuwa asilmia kubwa sana ya Watanzania, na hata hao waliopewa viwanja wanahangaika kulipa ada za shule za watoto, kulipia kodi ya nyumba, na hata chakula na mavazi. Hali hii imezidi kuwa ngumu katika awamu hii ya tano ambayo Lukuvi ni sehemu yake. Lukuvi haoni hilo, anachotaka ni Watanzania hao waache kuhangaikia ada na chakula ili wajenge hizo nyumba haraka sana. Kwanza tumuulize Lukuvi, je kwa upande wa serikali, imeshapeleka miundo mbinu kama barabara, maji na umeme katika maeneo haya, au bado viwanja hivi viko porini na serikali inachoona ni kibanzi katika macho ya waliogawiwa viwanja!

Ukweli ni kwamba watu wenye hela, huenda wengine ya ufisadi au mambo mengine, au vigogo kama Lukuvi mwenyewe, walishajenga siku nyingi sana. Na sasa labda Lukuvi atuambie, wakati serikali ikitekeleza mradi huu wa kugawa viwanja, nani hasa waliokuwa walengwa wa kupewa viwanja? Je walikuwa ni Watanzania mafisadi au wenye kipato kikubwa kama cha Lukuvi? Je yule mfanyakazi wa kawaida wa serikali anaesubiri mafao ili ajenge, hakustahili kupata kiwanja?

Kama Lukuvi angekuwa na uwezo mzuri wa kuona uhalisi wa mambo kama kiongozi wa wananchi ambao serikali ilitaka kuwasaidia kuwa na nyumba za kisasa, jambo ambalo angefanya badala ya kufoka watu watanyang'anywa viwanja kufikia December 2019, ni kuanzisha mpango wa mikopo nafuu ili watu wajenge. Tena mikopo hiyo isiwe na riba na itolewe kwa kutumia collateral ambayo ni mafao yaliyopo mifuko ya hifadhi. Ikibidi, taasisi hizo za hifadhi ya jamii ndio zitoe mikopo hiyo ya kujengea nyumba isiyo na riba. Benki kwa sasa zinatoza riba hadi 25%, Mtanzania gani wa kipato cha kawaida anaweza kukopa huko ili ajenge?

Lukuvi, asisahau yeye na viongozi wenzake awamu ya tano ni viongozi wa wananchi wote, wenye kipato kikubwa na kidogo. Anapaswa kupima mwenyewe kama ni halali kuwanyanganya viwanja wananchi wasio na uwezo wa kujenga ili kuwapa wananchi wenye uwezo wa kifedha, badala ya kuwawezesha ili waweze kujenga nyumba za kisasa.

Lukuvi hapaswi kuwapigia kelele za kuwanyang'anya wananchi viwanja wakati hujafanya lolote kuwasiaidia kujenga katika hivyo viwanja. Inafanya tutilie shaka lengo lake hasa hapa yeye na viongozi wenzake kuhusu hivyo viwanja. Usikute wanataka kuwanyang'anya wananchi hivyo viwanja ili wagawane kama walivyogawana nyumba za serikali huko nyuma!
 
Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,885
2,000
Mkuu una hoja ya msingi sana, nyumba haijengwi kwa siku moja, kuna wafanyakazi wana dunduliza kwa mwaka anapata pesa ya kununua mifuko 20 ya cement na mabati 10 anayawekeza duka la vifaa vya ujenzi, baada ya miaka mitano anaenda kuchukua mifuko yake 100 na mabati 50.

Mtu kama huyo ukimwambia ajenge kwa mwaka mmoja ni kumuonea, inawezekana hata hicho kiwanja alikipata kwa kukopa na bado anadaiwa, ukimnyang'anya kiwanja ni kumtia umasikini zaidi,
 
CHLOVEK

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
536
1,000
Historia ya Mh. Lukuvi inaonyesha kuwa alitokea unyongeni sana, na wapo waliomsaidia kufika hapo alipofika. Cha ajabu sasa badala ya kutumia uzoefu na uwezo alioupata kuwasaidia wanyonge kuinuka, yeye amebaki kuwatisha kama walivyofanya wakoloni. Nchi za wenzetu real estate ndio huwa wanajenga nyumba, wafanyakazi wanachukua morgage wanakwenda kuishi kwenye hizo nyumba huku wakikatwa kidogo kidogo kutoka kwenye mishahara yao.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,929
2,000
Mkuu una hoja msingi sana, nyumba haijengwi kwa siku moja, kuna wafanyakazi wana dunduliza kwa mwaka anapata pesa ya kununua mifuko 20 ya cement na mabati 10 anayawekeza duka la vifaa vya ujenzi, baada ya miaka mitano anaenda kuchukua mifuko yake 100 na mabati 50.

Mtu kama huyo ukimwambia ajenge kwa mwaka mmoja ni kumuonea, inawezekana hata hicho kiwanja alikipata kwa kukopa na bado anadaiwa, ukimnyang'anya kiwanja ni kumtia umasikini zaidi,
Shukurani Mkuu. Na huenda ilikuwa rahisi kufanya hivyo huko nyuma, maana katika awamu hii kuna watu walirudi kuomba hela walizodunduliza kwenye maduka ya vifaa vya ujenzi!
 
celinawetu

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
1,215
2,000
Syo kweli kuwa waliopewa ni watu wa kawaida,kwani wale watu wa kawaida waliomba na wengi waliomba ili wajenge, mfano ukienda Mbweni na Bunju maeneo ya low density ndo yamekuwa mapori na hayo ndo waligawana mafisadi wa ardhi kushirikiana na majizi serikalini.

Lukuvi kaza buti baba siku ya kuwafutia basi tukumbuke sisi walala hoi tuje tuvinunue hata kwa mkopo.
Baba hongera sana mkombozi wa wanyonge kwa busara na hekima zako mungu akuwekee mkono wake udumu ktk kweli na haki
 
celinawetu

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
1,215
2,000
Historia ya Mh. Lukuvi inaonyesha kuwa alitokea unyongeni sana, na wapo waliomsaidia kufika hapo alipofika. Cha ajabu sasa badala ya kutumia uzoefu na uwezo alioupata kuwasaidia wanyonge kuinuka, yeye amebaki kuwatisha kama walivyofanya wakoloni. Nchi za wenzetu real estate ndio huwa wanajenga nyumba, wafanyakazi wanachukua morgage wanakwenda kuishi kwenye hizo nyumba huku wakikatwa kidogo kidogo kutoka kwenye mishahara yao.

Ishu ni kuhodhi viwanja bila kuendeleza wakati wanyonge hawana pa kuishi.
Lukuvi baba shika hivyo hivyo hadi wa PUU
 
celinawetu

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
1,215
2,000
Mkuu una hoja ya msingi sana, nyumba haijengwi kwa siku moja, kuna wafanyakazi wana dunduliza kwa mwaka anapata pesa ya kununua mifuko 20 ya cement na mabati 10 anayawekeza duka la vifaa vya ujenzi, baada ya miaka mitano anaenda kuchukua mifuko yake 100 na mabati 50.

Mtu kama huyo ukimwambia ajenge kwa mwaka mmoja ni kumuonea, inawezekana hata hicho kiwanja alikipata kwa kukopa na bado anadaiwa, ukimnyang'anya kiwanja ni kumtia umasikini zaidi,

Viwanja vya mbweni,bunju vimegawiwa tangu 2000+ sasa yapata miaka ishirini, huko kuwekeza kidogokidogo ili ujenge unataka kujenga nini..
Usiachie baba minya kwa nguvu zaidi wasiponyoke
 
eliakeem

JF-Expert Member
May 29, 2009
9,824
2,000
Mleta mada umetaja mambo mazuri ambayo yanaweza kusaidia wananchi kuweza kujipatia makazi. Hata nchi zilizoendelea ni serikali na wadau wengine, lakani kwa kuongozwa na sera na sheria walizojiwekea. Nyumba za madaraja na matumizi tofauti tofauti zinajengwa na real estate developers, Real Estate Investment Trust (REIT) etc ambao huzigawa kwa wafanyakazi kwa udhamini (guarantee) wa muajiri au serikali kwa masharti ya kulipa kidogo kidogo.

Kunyang'anya kiwanja kwa wasioendeleza, binafsi nadhani waziri anafanya kwa mujibu wa sheria. Hata nyaraka za umiliki zinataja miaka ambayo unapaswa kuwa uwe umejenga nyumba yako. Kama anafanya kwa mujibu wa sheria, yeye binafsi hapaswi kuwa na lawama. Kinachotakiwa ni kuangalia sheria kama ni kandamizi au la. Ikiwa ni kandamizi, basi hatua zinazohusika kubadilisha sheria zinajulikana.

Lingine ni kuwa, si wote ambao wanashindwa kujenga ni wale wasio na uwezo. Ukweli ni kuwa, kuna idadi kubwa tu ya watu wanaomiliki viwanja zaidi ya kimoja. Ambao hawana mpango wa kujenga, lakini wana mpango wa kuuza endapo bei zitapanda (arbitragerrs or speculators). Hawa wanataka wafaidike na price difference between two markets or times. Hata mimi ninavyo viwanja viwili huko bongo. Na nategemea kununua zaidi. Nikidunduliza hela huku, narudi huko home bongo mwezi desemba nanunua kiwanja, basi maisha yanaendelea. Nasikia Dodoma is another potential investment destination. Nitatembelea nione hali ilivyo.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,929
2,000
Syo kweli kuwa waliopewa ni watu wa kawaida,kwani wale watu wa kawaida waliomba na wengi waliomba ili wajenge, mfano ukienda Mbweni na Bunju maeneo ya low density ndo yamekuwa mapori na hayo ndo waligawana mafisadi wa ardhi kushirikiana na majizi serikalini.

Lukuvi kaza buti baba siku ya kuwafutia basi tukumbuke sisi walala hoi tuje tuvinunue hata kwa mkopo.
Baba hongera sana mkombozi wa wanyonge kwa busara na hekima zako mungu akuwekee mkono wake udumu ktk kweli na haki
Kwa hiyo watu wana viwanja, wana hela na wameamua tu hawataki kujenga hata kibanda kidogo cha kushikia kiwanja? Nyie sema mna wivu wa kike tu hamtaki wengine wafaidi.
 
Umeongea kwa hekima sana Mkuu. Lakini tukumbuke kwamba viwanja vingi ambavyo havijajengwa ni vile vya low density ambako kwa kweli wengi waliopewa ni watu wa kawaida tu. Hivyo kufanya uamuzi wa jumla kwamba wote ambao hawajajenga wanyang'anywe sio haki, na ninauwa wa kwanza kukiri kama kuna hiyo sheria basi ni sheria kandamizi. Hata hivyo, ndio maana nikasema Lukuvi ajikite katika kuangalia jinsi ya kusaidia watu ambao kweli kweli hawajajenga kwa kuwa hawana uwezo wa kujenga.

Na pia wapo wachache waliovipata kwa nia ya kuhodhi tu. Nadhani hilo sio suala gumu kufuatilia. Siku hizi mambo yako wazi sana.

By the way, nikuambie kitu cha kuchekesha . Serikali ya Tanzania ilipewa kiwanja cha kujenga ofisi ya ubalozi pale mjini Addis Ababa, Ethiopia. Ilipita zaidi ya miaka kumi bila kiwanja kujengwa, kikawa kimezungukwa na majengo mengine, serikali ya Tanzania ikidai haina fedha na kuiomba serikali ya Ethiopia isiwanyang'anye hicho kiwanja! Sijui kama sasa wamejenga!
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,929
2,000
Ishu ni kuhodhi viwanja bila kuendeleza wakati wanyonge hawana pa kuishi.
Lukuvi baba shika hivyo hivyo hadi wa PUU
Kwani hao wenye viwanja wakijenga hao wanyonge ndio watapata sehemu ya kuishi? Hiyo sio point kwa kuwa hayao ni mabo mawili hayana uhisiano kabisa. Kama kuna wanyonge wasio na pa kuishi serikali iendeleze mradi wa kugawa viwanja.
 
celinawetu

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
1,215
2,000
Kwa hiyo watu wana viwanja, wana hela na wameamua tu hawataki kujenga hata kibanda kidogo cha kushikia kiwanja? Nyie sema mna wivu wa kike tu hamtaki wengine wafaidi.

Kama ni suala la kufaidi sote tunataka tufaidi, wacha mminywe sawasawa hadi mu puuu muache viwanja wenye shida wajenge
 
celinawetu

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
1,215
2,000
Kwani hao wenye viwanja wakijenga hao wanyonge ndio watapata sehemu ya kuishi? Hiyo sio point kwa kuwa hayao ni mabo mawili hayana uhisiano kabisa. Kama kuna wanyonge wasio na pa kuishi serikali iendeleze mradi wa kugawa viwanja.
Ili wao wagawiwe maporini kama manyoka!!!! Achieni hivyo viwanja mlivyogawana tuvinunue tujengee hata michepuko kuliko kuviacha waishi nyoka na mapanya buku
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,102
2,000
Suala la kujenga nyumba na makazi kwanza ni jukumu la Shirika la Nyumba la Taifa.

Haya mengine ya kuja kuwasumbua watu wenye plani na priority za maisha yao ni unyanyasaji na uonevu uliopitiliza...
Kiwanja kama mlishanipa... mnatakiwa mniachie mimi for as long as hati bado ipo valid!

Kingine anachokosea Lukuvi ni kujipatia pesa kwa utaratibu usio rafiki wa kulazimisha upimaji wa maeneo ya watu waliojitafutia kwa jasho lao au kwa kurithi...!

Serikali kama imeishiwa fedha ikiri tu kuwa haina fedha badala ya kuwasumbua wananchi na kuwafanya waishi kama digi digi ndani ya nchi yao..

Aidha ni wakati muafaka wa kila mwananchi amiliki ardhi ndani ya nchi yake... Iweje tuwe na nchi yenye wananchi alafu ardhi yote iwe mali ya serikali?

Au bado mnaamini kuwa watanzania hawana uwezo wa kuthibiti matumizi ya ardhi hadi serikali iingilie kati..??
 
muchetz

JF-Expert Member
Aug 16, 2010
914
1,000
Syo kweli kuwa waliopewa ni watu wa kawaida,kwani wale watu wa kawaida waliomba na wengi waliomba ili wajenge, mfano ukienda Mbweni na Bunju maeneo ya low density ndo yamekuwa mapori na hayo ndo waligawana mafisadi wa ardhi kushirikiana na majizi serikalini.

Lukuvi kaza buti baba siku ya kuwafutia basi tukumbuke sisi walala hoi tuje tuvinunue hata kwa mkopo.
Baba hongera sana mkombozi wa wanyonge kwa busara na hekima zako mungu akuwekee mkono wake udumu ktk kweli na haki

Kwani lazime tujue ujinga wako? Ungekaa kimya tusingejua u mjinga kiasi gani. Anyhow the choice is yours.
 
mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,694
2,000
Syo kweli kuwa waliopewa ni watu wa kawaida,kwani wale watu wa kawaida waliomba na wengi waliomba ili wajenge, mfano ukienda Mbweni na Bunju maeneo ya low density ndo yamekuwa mapori na hayo ndo waligawana mafisadi wa ardhi kushirikiana na majizi serikalini.

Lukuvi kaza buti baba siku ya kuwafutia basi tukumbuke sisi walala hoi tuje tuvinunue hata kwa mkopo.
Baba hongera sana mkombozi wa wanyonge kwa busara na hekima zako mungu akuwekee mkono wake udumu ktk kweli na haki
Mkuu jielekeze katika mantiki za mtoa hoja. Ameelezea kwa kina na uhalisia kuhusu umiliki wa viwanja na uwezo wa mtu binafsi kuviendeleza ktk mazingira ya sasa ya kiuchumi. Epuka "perception errors". Siyo ukweli ya kwamba yeyote aliyepewa kiwanja, labda cha "low density" na kushindwa kukiendeleza ana historia ya kuwa fisadi. Hizi roho za kimaskini na kifukara za kutaka mwingine anyang'anywe upewe wewe sijui zinatokea wapi nyakati hizi!
 
Mookiesbad98

JF-Expert Member
Feb 1, 2015
1,687
2,000
Nafunga mkono hoja. Sio wote waliopata viwanja Wana Hali nzuri ya kujenga kwa haraka.

Kuna watu Wana maviwanja mengi na hawaendelezi hao ndio wanaweza kutaifishwa. Mfanyakazi wa serikali au sekta binafsi kabahatika kupata kiwanja kilichopimwa halafu umnyanganye.

Mfano Kibada, mbweni na meneo mengine wapi watu wa kipato Cha chini.

Waziri asidhani Kama Ana uwezo wa kununua nyumba Mbezibeach labda mil 500 ni watu wachache wenye baraka za Aina hiyo.

Sijawahi tembea Dar hii bila kukuta eneo la Patel & Co. Hao ndio wasipoendeleza wanyanganywe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom