Waziri Lukuvi badala ya kuwatishia Watanzania wa hali chini kichumi wawezeshe, si kila aliyepewa kiwanja ni fisadi au ana kipato kama wewe

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,991
2,000
Nafunga mkono hoja. Sio wote waliopata viwanja Wana Hali nzuri ya kujenga kwa haraka.

Kuna watu Wana maviwanja mengi na hawaendelezi hao ndio wanaweza kutaifishwa. Mfanyakazi wa serikali au sekta binafsi kabahatika kupata kiwanja kilichopimwa halafu umnyanganye.

Mfano Kibada, mbweni na meneo mengine wapi watu wa kipato Cha chini.

Waziri asidhani Kama Ana uwezo wa kununua nyumba Mbezibeach labda mil 500 ni watu wachache wenye baraka za Aina hiyo.

Sijawahi tembea Dar hii bila kukuta eneo la Patel & Co. Hao ndio wasipoendeleza wanyanganywe
Mkuu wanasema hawana uwezo wa kujua nani ana uwezo nani hana, kwa hiyo inabidi wanyang'anywe wote tu.

Sasa mimi ninachojiuliza, hao wapya watakaopewa wanajuaje wana uwezo wa kujenga kuliko wale walionyang'anywa? Ndio maana nikasema usikute ni mpango wao wa kugawana hivi viwnja kama walivyogawana nyumba za serikali!
 
N16

Member
Jul 21, 2019
13
45
Kuendeleza maana yake si ujenge nyumba iishe, hata ukiweka msingi umeendeleza.Mimi mtazamo wangu ni speculator tu ndiye ananunua viwanja haombi hata kibali cha ujenzi fikra yake bei ipande apate faida.
 
Mookiesbad98

JF-Expert Member
Feb 1, 2015
1,821
2,000
Nadhani amekurupuka bila kuangalia athari kwa wananchi. Fedha imekauka watu watajengea na nini?

Yasije yakatokea Yale ya mji mpya kigamboni city na Mama Tibaijuka kumbe iilikuwa wananchi wanaondolewa kisayansi mabepari wapate ardhi.
 
celinawetu

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
1,303
2,000
Mkuu jielekeze katika mantiki za mtoa hoja. Ameelezea kwa kina na uhalisia kuhusu umiliki wa viwanja na uwezo wa mtu binafsi kuviendeleza ktk mazingira ya sasa ya kiuchumi. Epuka "perception errors". Siyo ukweli ya kwamba yeyote aliyepewa kiwanja, labda cha "low density" na kushindwa kukiendeleza ana historia ya kuwa fisadi. Hizi roho za kimaskini na kifukara za kutaka mwingine anyang'anywe upewe wewe sijui zinatokea wapi nyakati hizi!

Sasa wajitokeze waeleze wana malengo gani na hivyo viwanja,
Tatizo mkuu kuna sehemu ni mapori na kama umejenga basi utakuwa na wakati mgumu wa kufukuzana na wadudu wabaya na wezi, wanatupa shidaaa
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,991
2,000
Sasa wajitokeze waeleze wana malengo gani na hivyo viwanja,
Tatizo mkuu kuna sehemu ni mapori na kama umejenga basi utakuwa na wakati mgumu wa kufukuzana na wadudu wabaya na wezi, wanatupa shidaaa

Mie hapa. Lengo langu ni kujenga nikilipwa mafao yangu ya kustaafu kwa kuwa kwa sasa sina uwezo wa kujenga
 
gnassingbe

JF-Expert Member
Jun 14, 2015
4,831
2,000
Historia ya Mh. Lukuvi inaonyesha kuwa alitokea unyongeni sana, na wapo waliomsaidia kufika hapo alipofika. Cha ajabu sasa badala ya kutumia uzoefu na uwezo alioupata kuwasaidia wanyonge kuinuka, yeye amebaki kuwatisha kama walivyofanya wakoloni. Nchi za wenzetu real estate ndio huwa wanajenga nyumba, wafanyakazi wanachukua morgage wanakwenda kuishi kwenye hizo nyumba huku wakikatwa kidogo kidogo kutoka kwenye mishahara yao.
Kuna miradi ya NHC inafanya hivyo!
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,991
2,000
Kuendeleza maana yake si ujenge nyumba iishe, hata ukiweka msingi umeendeleza.Mimi mtazamo wangu ni speculator tu ndiye ananunua viwanja haombi hata kibali cha ujenzi fikra yake bei ipande apate faida.
Lakini suala jingine la msingi ni kwamba, wakati Lukuvi anapiga kelele kuwa watu wanyang'anywe viwanja, je serikali imefanya nini kupeleka huduma za msingi kama maji na umeme huko? Leo hii nikijenga nyumba huko, nitapata maji ya bomba? Je nitavuta umeme kirahisi? Barabara zimechongwa?
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,950
2,000
Mara nyingi hali ngumu ya kipato ndo inawabana watu wasiweze kuendeleza maeneo yao, mishahara haiongezeki, biashara hazi perform, uwekezaji kwenye sekta binafsi unachechemea, kilimo hakieleweki, vijana wengi wanalandalanda tu bila kuwa na kazi za kufanya lakini kutwa kujisifia tumenunua ndege na bado tunaongeza zingine, ni shida aisee..
 
Hili nalo neno, siyo kulazimisha watu wajenge wakati hakuna miundombinu wezeshi
 
Kweli Mkuu. Nimesema hakuna mtu mwenye kiwanja, ana shida ya nyumba, ana uwezo wa kujenga lakini hataki kujenga. Kama wapo ni wachace ambao wanavizia kuviuza kwa bei za juu. Na hao ni wale ambao Wizara ya ardhi yenyewe iliwapa viwanja kwa mlango wa nyuma, au wafanyakazi wa wizara yenyewe!
 
Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
3,230
2,000
Ishu ni kuhodhi viwanja bila kuendeleza wakati wanyonge hawana pa kuishi.
Lukuvi baba shika hivyo hivyo hadi wa PUU
kwa hiyo bora tunyan'ganywe halafu wewe ndo utafaidika na nini?
binafsi akiamua kuchukua mwache achukue najua thamani niliyonunulia hicho kiwanja wakati huo nikifanya kazi kwa mtu nikilipwa shilingi 120,000/- kama mshahara. nikakopa kwa watu nikaweza kununua kiwanja cha 690,000 wakati huo lakini nilifanikiwa kwa kutoa awamu mbili kwa kuandika barua kwa meneja wa mradi.
kwa muda mrefu kweli sijakiendeleza na sio sitaki ila kwa changamoto zinazonikabiri kwa zaidi ya miaka saba sasa na nimeshindwa kuendeleza ujenzi.
sasa kama kaamua kukichukua mwache achukue tu ili ninyi ambao hamkupata wakati ule mfurahi japo ikumbukwe ilikuwa ni kwenda tu kujaza form na kisha unagawiwa kiwanja.
roho zetu zitauma kwa kuwa tutakuwa tumepoteza kitu cha thamni lakini ikumbukwe pia tutakuwa tumethurumiwa kwa kuwa sisi ni wapangaji kwa miaka zaidi ya 60 kwa kadri ya hati ya mkataba wa kiwanja.
 
Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
3,230
2,000
Hili nalo neno, siyo kulazimisha watu wajenge wakati hakuna miundombinu wezeshi
cha kwangu barabara hazipitiki halafu mtu aliyejilimbikizia ardhi kila kona ya nchi hii anaamua kuninyanganya yeye aliyebadili open space kuwa viwanja na akiwa mwenyekiti wa bodi ya CDA wakati ule alishindwa kutengeneza mazingira rafiki watu wamiliki viwanja lakini yeye kila siku kujilimbikizia maeneo.
sisi kilio chetu kutampelekea MUNGU kwa kuwa tunajua jambo hili litafanywa kwa matabaka itakuwa kama harusi za watani zangu wahaya wakati ule hawajajua kuwa kuna watu wengine zaidi ya wahaya kwa kuwabagua kwenye vinywaji hupati Heineken kawa sio muhaya
Bora ya mfalme Daudi alivyojua amefanya kosa kwa kumchukua mke wa mtu alifanya toba 2samweli 12:1-13 lakini si huyu ambaye shule yake kubwa katika utaalamu wa ardhi na kujali jamii haitusaidi.
Kama mfalme Daudi alivyompiga Uria kwa kisingizio cha vita ndivyo huyu Lukuvi anatupora ardhi yetu kwa kisingizio cha makusanyo wakati viwanja alivyopima kashindwa kuuza.
2SAMWELI 12:9-10Kwa nini umelidharau neno la MUNGU kwa kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Uria Mhiti umempiga kwa upanga, nawe ukamchukua mke wake awe mke wako,+ naye ukamuua kwa upanga wa wana wa Amoni.10 Na sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako mpaka wakati usio na kipimo, kwa sababu ulinidharau mimi, ukamchukua mke wa Uria Mhiti, awe mke wako.’
MWENYEZI MUNGU atatufanyia hukumu kwa hili
 
Nyati

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
2,405
2,000
Kuendeleza maana yake si ujenge nyumba iishe, hata ukiweka msingi umeendeleza.Mimi mtazamo wangu ni speculator tu ndiye ananunua viwanja haombi hata kibali cha ujenzi fikra yake bei ipande apate faida.

Sheria ipi mkuu? Si hivyo kama wakiamua hata wakute msingi wanakufanyia weee acha tu! Kuna jamaa alikuwa na nyumba ya nyuma nusu wampoke hadi alipowaitia mganga wa kienyeji akawatishia NYAU. Waoga hao, wakija kwako komaaa nao usiwasikilize waite vijana wa kijiweni wawatoe baruti. Komaa tu mkuu
 
santali

JF-Expert Member
Aug 9, 2017
321
250
Walipashwa kuweka utaratibu wa shirika la nyumba linajenga kwenye viwanja vya watu hao walipewa wanakopeshwa ili visikae wazi wakati watu wengine wanataka, na Lukuvi shirika la nyumba liko chini yake utaratibu ungewekwa wangejenga wanakopeshwa thamani ya nyumba, kiwanja kinabaki kama dhamana
 
Shirika la nyumba tatizo ni kama benki, wanatoza hela nyingi sana. Yaani gharama ya kufikisha msingi tu wewe binafsi unaweza kuwa umemaliza nyumba!
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,991
2,000
kwa hiyo bora tunyan'ganywe halafu wewe ndo utafaidika na nini?
binafsi akiamua kuchukua mwache achukue najua thamani niliyonunulia hicho kiwanja wakati huo nikifanya kazi kwa mtu nikilipwa shilingi 120,000/- kama mshahara. nikakopa kwa watu nikaweza kununua kiwanja cha 690,000 wakati huo lakini nilifanikiwa kwa kutoa awamu mbili kwa kuandika barua kwa meneja wa mradi.
kwa muda mrefu kweli sijakiendeleza na sio sitaki ila kwa changamoto zinazonikabiri kwa zaidi ya miaka saba sasa na nimeshindwa kuendeleza ujenzi.
sasa kama kaamua kukichukua mwache achukue tu ili ninyi ambao hamkupata wakati ule mfurahi japo ikumbukwe ilikuwa ni kwenda tu kujaza form na kisha unagawiwa kiwanja.
roho zetu zitauma kwa kuwa tutakuwa tumepoteza kitu cha thamni lakini ikumbukwe pia tutakuwa tumethurumiwa kwa kuwa sisi ni wapangaji kwa miaka zaidi ya 60 kwa kadri ya hati ya mkataba wa kiwanja.
Du umeongea kwa uchungu sana Mkuu!
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
26,065
2,000
Kila wakati Lukuvi anapenda kutoa tishio kwa Watanzania waliopewa viwanja na serikali kuwa watanyang'anywa kwa kuwa hawana uwezo wa kujenga. Yaani Lukuvi anachosema ni kwamba, hawakustahili kupewa hivyo viwanja kwa kuwa wao hali yao ya kuichumi iko chini na hawana uwezo wa kujenga hara
Kwanza hujamuelewa lukuvi
Pili sheria inataka hivyo
Anachokataa lukuvi usiache pori,jengawalau chumba kimoja weka mtu awe anasafisha
Sio vitisho utanyang'anywa kweli nenda ukurasa wa pili wa hati yako kasome kuna masharti ya kuazimwa hiyo ardhi na ukaweka saini yako,anachofanya lukuvi ni kufuata sheria tu
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,991
2,000
Kwanza hujamuelewa lukuvi
Pili sheria inataka hivyo
Anachokataa lukuvi usiache pori,jengawalau chumba kimoja weka mtu awe anasafisha
Sio vitisho utanyang'anywa kweli nenda ukurasa wa pili wa hati yako kasome kuna masharti ya kuazimwa hiyo ardhi na ukaweka saini yako,anachofanya lukuvi ni kufuata sheria tu
Mwambie Lukuvi kwamba nataka kujenga, lakini kiwanja changu kilipo hakuna barabara wala maji. Na umeme uko mbali sana. Aweke basi angalau hiyo miundo mbinu mie nitajenga angalau chumba kimoja.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom