Waziri Lugola: Marufuku kuwatambua Wahamiaji haramu kwa kigezo cha pua ndefu na kuimba wimbo wa Taifa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, amepiga marufuku tabia ya Maafisa Uhamiaji hasa waliopo mikoa ya mipakani kuwatambua Wahamiaji haramu kwa kigezo cha pua ndefu, kuimba wimbo wa Taifa na urefu wa mwili wake.

Lugola amepiga marufuku hiyo Jana alipokuwa akiongea moja ya mikutano yake mkoani Kagera ambako yuko kwenye ziara yake ya kikazi iliyoanzia Januari 2, mwaka huu.

"Idara ya Uhamiaji kutambua wahamiaji haramu kwa kigezo cha pua ndefu, kuimba wimbo wa Taifa na urefu wa mwili wake nimepiga marufuku," alisema.

Aidha Lugola ameongeza kuwa Idara ya Uhamiaji ina taratibu na vigezo vyake kiweledi katika kushughulikia suala hilo, hivyo amesisitiza viendelee kutumika kubaini nani raia na nani si raia.
IMG_20190107_214029.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah ndio maana yule jamaa aliyevuka kutoka Malawi akazama Mbeya kuchukua ID ya kupigia kura alipoambiwa na jamaa wa uhamiaji aimbe wimbo wa taifa wa Tz aliimba..

Kama sio juhudi zako Nyerere na uhuru tungepata wapiiiiiiiiiiiii,hahah nadhani ushajua kilichofuata hapo.
 
Chini ana jeans

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilimradi amechishe...

Anyway,
Sijui kama screening itafanikiwa maana wengine ni wazaliwa katika Wilaya hizo tangu miaka ya 60 baada ya wazazi wao kukimbilia Tanzania miaka hiyo au chini yake na bado wana hati za zamani za Uraia zilizo tolewa na ofisi hizo za Uhamiaji miaka hiyo. Je, watafanyaje kuwakana hao walio watambua japo wasifu wa nje (physical representations) na rafuzi zao vina dhihirisha asili ya Utaifa wao????
Huwa nasema Tanzania inabeba gharama / mzigo pasipo ulazima! Matibabu, elimu nk. Baadhi ya watalaam waliosoma bure Tz walirudi makwao na elimu waliyo ipata Tz inasaidia mataifa yao huko.

Bado ndugu zao ambao hawakutaka kurudi kwa sababu zao wenyewe bado wamefaidi mapori ya hifadhi za Taifa Tz kwa kufugia ngombe bure kabisa.... Tanzania hii, hakunaga. Labda tu kwa sasa ambapo wafugaji wote awe mkubwa au mdogo wote wameondolewa katika mapori hayo na uoto wa asili unaanza kurejea na wanyama kurejea upya, walau heko kwa hilo, ila swali ni je, is this protection/ ban sustainable????

Hali kadharika (ugaji, makazi, ukataji miti/ mkaa) horera na wa hovyo vimeathiri mazingira haijawahi kutokea! Bado uharibifu unaendelea na wala sijui ni lini hali hii itakoma, hapa na Makazi wa mikoa jilani ya Kanda ya ziwa kwa Ujumla wanachangia kwa kiasi kikubwa, Msukuma asione pori utafikiri Mhaya kaona senene!
 
Kwa kauli hii naona anawatetea baadhi yao aliokaa nao front kisa nyadhifa zao ama??
 
Au pua pana (Wanai
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, amepiga marufuku tabia ya Maafisa Uhamiaji hasa waliopo mikoa ya mipakani kuwatambua Wahamiaji haramu kwa kigezo cha pua ndefu, kuimba wimbo wa Taifa na urefu wa mwili wake.

Lugola amepiga marufuku hiyo Jana alipokuwa akiongea moja ya mikutano yake mkoani Kagera ambako yuko kwenye ziara yake ya kikazi iliyoanzia Januari 2, mwaka huu.

"Idara ya Uhamiaji kutambua wahamiaji haramu kwa kigezo cha pua ndefu, kuimba wimbo wa Taifa na urefu wa mwili wake nimepiga marufuku," alisema.

Aidha Lugola ameongeza kuwa Idara ya Uhamiaji ina taratibu na vigezo vyake kiweledi katika kushughulikia suala hilo, hivyo amesisitiza viendelee kutumika kubaini nani raia na nani si raia.View attachment 989229

Sent using Jamii Forums mobile app
Au pua pana (Wanaijeria na wengineo West Africa), au uzuri kupindukia (Wasomali, Ethiopia n.k.). Au....
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, amepiga marufuku tabia ya Maafisa Uhamiaji hasa waliopo mikoa ya mipakani kuwatambua Wahamiaji haramu kwa kigezo cha pua ndefu, kuimba wimbo wa Taifa na urefu wa mwili wake.

Lugola amepiga marufuku hiyo Jana alipokuwa akiongea moja ya mikutano yake mkoani Kagera ambako yuko kwenye ziara yake ya kikazi iliyoanzia Januari 2, mwaka huu.

"Idara ya Uhamiaji kutambua wahamiaji haramu kwa kigezo cha pua ndefu, kuimba wimbo wa Taifa na urefu wa mwili wake nimepiga marufuku," alisema.

Aidha Lugola ameongeza kuwa Idara ya Uhamiaji ina taratibu na vigezo vyake kiweledi katika kushughulikia suala hilo, hivyo amesisitiza viendelee kutumika kubaini nani raia na nani si raia.View attachment 989229

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kumbe Lugola yupo?
 
Back
Top Bottom