Waziri Lugola: Aliyekuwa Mkurugenzi NIDA, Dickson Maimu na Jack Gotham wasipoitikia wito ‘watapata tabu sana’

Japo nami si muu
Lugola naye kazidi kwa matamko yake sasa. Kila siku anakuja na mpya. Ya awali ameshayatekeleza?

Hana tofauti na Aggrey Mwanri RC wa Tabora ambaye akifika site hufoka mno lakini utekelezaji zero.

Lugola mpaka sasa amerukia rukia mambo mengi lakini sioni anachofanikiwa zaidi ya kutoa masaa kadhaa lakini baada ya hapo hurukia mengine.[/QUOT

Japo nami sizimii matamko, lakini najiuliza kama kila anakopita kuna issues ataacha mpaka tamko la kwanza lipate jibu ndio atoe lingine? Labda style yao ya ufanyaji kazi ndio wangebadilisha kuwa wawashe mioto humo ndani kiutendaji sie huku tuone matokeo...sio lazima kila kitu kitoke kwa matamko na matarumbeta.
 
Mkuu mimi kitambulisho cha uraia mbona nimechukua baada ya miezi 3? Tena nilichelewa mwenyewe tu kwenda ila waliniambia kilikua tayari baada ya wiki 2
Hongera mkuu, itakua uko Dar es Salaam. Huku mkoani ni shida sana mwaka mzima watu wanasubiri hakuna majibu. Leseni za udereva mpya nazo ni tabu hazitoki. Kila ID ambayo ni biometric mkoani utalia sana
 
Kangi lugola ,ataweza huu mfupa ?

Huyu Jack Gotham , mfadhili na mmoja wa wana mikakati wa Bernard membe , aliyepewa tenda hiyo ili wapige pesa za kampeni 2015, huku huyu Dickson Maimu akiwekwa pale kukamilisha dili, bila kujua mlokole wa kitengo alikuwa pale ,akiwasoma na kuwa study vilivyo ,alivyomaliza kazi yake kwa ustadi , akapewa U DG , hakika kikwete na udhaifu wake kuna mambo alistahili pongezi kwa kiasi maana alikuwa na uzalendo nusu ubandidu nusu


Je kangi ataweza huu mfupa wenye chain ndefu ?

Yetu Macho na masikio
Mlokole mtu mbaya sana, Bot pia amepozi sana
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema, kuna kampuni zimelipwa fedha kifisadi kwenye mradi wa vitambulisho vya taifa.

Amezitaja kampuni hizo ni Gotham International Limited inayodaiwa Sh bilioni 2.8, Iris Corporation Berhard Sh bilioni 22.9, Gwiholoto Impex Limited Sh milioni 946.4, Sykes Travel Agent Sh milioni 5.9, Dk Shija Paul Rimoy Sh milioni 27, Aste Insurance inayodaiwa Sh bilioni 1.2 na BMTL Sh milioni 569.1.

Amesema kampuni hizo zinadaiwa Sh bilioni 28.5.

Ameagiza aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu na Jacky Gotham waende Dodoma Agosti 3 kujieleza.

“Wafike ili watoe maelezo yanayojitosheleza hasa kwenye ule mtambo wa shilingi bilioni 32 inaonekana fedha imetolewa lakini mtambo haujaletwa,” amesema na kuagiza watu hao waandikiwe barua na hata kupigiwa simu na wasifanye jaribio lolote la kutofika siku hiyo.

Amesema Kampuni ya Iris ilikuwa mkandarasi na walihusika katika kuleta mtambo, kampuni ya Gotham ilikuwa mshauri mwelekezi na ililipwa fedha za dharura kwenye viwango ambavyo si sahihi.
 
Maadam anatetea fedha za walipa kodi, NINJA chapaka kazi! angalau umeonyesha unafuu kuliko yule.
 
Kangi bin Lugola alipua bomu lingine NIDA ndio kichwa cha habari kilitakiwa kisome:D:D
 
Last edited:
why waje kwako kujieleza wewe ni nani ?please waziri wangu wa mambo ya ndani onyesha kwa vitendo jinsi ya kuishi kwa wajibu wa kisheria,nenda kwenye kituo cha polisi na fungua mashitaka dhidi ya wakurugenzi hao,polisi watachunguza,watakusanya ushahidi then apply their mind kama watuhumiwa wana kesi ya kujibu,kama wanao wata arrest watuhumiwa na kuwapeleka mahakamani,huu ndio utaratibu wetu mh.waziri kinyume cha hapo ni mihemko tu,sasa wakijieleza kwako utawafanya nini?au ndio kama wale ma RCs na DCs wanaoamrisha weka ndani hao!
 
ni jambo jema na nimpongeze waziri kuhakikisha kuwa fedha za wananchi zinapata usimamizi mzuri.
 
Back
Top Bottom