Mwana Mtoka Pabaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 15,118
- 16,470
Mie ntawaomba kontena tupu.Matamko mengine ya awali yametekelezwa?
Mie ntawaomba kontena tupu.Matamko mengine ya awali yametekelezwa?
Ah! Mkuu sazingine vitisho vinajenga nidhamu buana!Swali hapa ..... ni kwa nini atutangazie kwenye vyombo vya habari kuwa fulani na fulani ni lazima wafike ofisini kwake siku fulani. La sivyo watapata tabu sana.
Wewe huoni kuwa anawadhalilisha hao watu ....!!
hivi hawa kwa nini wanaogopa kumjibu Lugola ki-Trump-Trump??Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameipa wiki mbili kampuni ya Kimataifa ya Iris Corporation Berhard impe majibu ya kuwa italeta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au Dola za Marekani Milioni 14 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 32 za Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, Dodoma leo,baada ya kikao na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)na viongozi wa Kampuni hiyo, Waziri Lugola alisema kampuni hiyo haiwezi ikacheza na fedha za Watanzania na walipa kodi.
Lugola aliongeza kuwa lazima fedha hizo au mtambo huo upatikane kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitakubaliana na mchezo mchafu wa aina yoyote, na pia yeye kama Waziri wa Wizara hiyo anaendelea kutekeleza maagizo ya Rais Dkt John Magufuli. “Tumezungumza nao na tumekubaliana
Aidha, Waziri Lugola amewataka wamiliki wa kampuni zilizolipwa kifisadi fedha za Mradi wa mtambo wa NIDA kujisalimisha jijini Dodoma Agosti 3 mwaka huu wakiwa na mtambo huo vinginevyo warejeshe fedha zilizotumika.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesisitiza kuwa kutokana na wito alioutoa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu pamoja na Jack Gotham kufika ofisini kwake, wasifanye jaribio la kutokuitikia wito huo, kwani wakifanya hivyo watapata tabu sana.
Inaelekea huamini katika utawala wa sheria.Ah! Mkuu sazingine vitisho vinajenga nidhamu buana!
Ungekuwepo miaka ya 80' enzi za Lyatonga Mrema akiwa na wadhifa huohuo alionao Lugola leo, unakumbuka alivyonasa madhahabu pale air port, unakumbuka alivyokuwa akiwaita na kuwapangia matajiri na wahujumu uchumi kwenda kuripoti kwake kwa muda alioutaka yeye na walitii?
Nyani ukiwachekea utaambulia mabua.
Hii nchi ilikuwa imefikia pabaya
Acha kuwatisha tu, awasweke ndani na kuwafungulia mashitaka wakajibu tuhuma zao mahakamani huko wasipotekeleza maagizo yake.
Kama inafanana na hivyo Mkuu. Inasikitisha sana. Mungu ibariki Tanzania tutoke tulipo. Loh!Unatafuta punje ya sukari kwenye mchanga??
Kangi lugola ,ataweza huu mfupa ?
Huyu Jack Gotham , mfadhili na mmoja wa wana mikakati wa Bernard membe , aliyepewa tenda hiyo ili wapige pesa za kampeni 2015, huku huyu Dickson Maimu akiwekwa pale kukamilisha dili, bila kujua mlokole wa kitengo alikuwa pale ,akiwasoma na kuwa study vilivyo ,alivyomaliza kazi yake kwa ustadi , akapewa U DG , hakika kikwete na udhaifu wake kuna mambo alistahili pongezi kwa kiasi maana alikuwa na uzalendo nusu ubandidu nusu
Je kangi ataweza huu mfupa wenye chain ndefu ?
Yetu Macho na masikio
Acha ushabiki wa kijinga Wewe..serikali IPO madarakani kusimamia Mali na fedha kwa niaba ya wananchi Mimi sina mlengo wa kichama ila kwa hili ninampongeza kangiMdogo mdogo tu ipo siku na aliyeuza nyumba za umma atatakiwa kuripoti makao makuu ya sungusungu.
"atapata tabu sana"!
Kwa waziri anapoagiza hasa wa ulinzi lazima wayekeleze mfano..mbwa tiyari kashapatikana,arusha RPC ametekeleza maagizo yote ya waziri mpaka Jana, Etc. Tuache ushabikiLugola naye kazidi kwa matamko yake sasa. Kila siku anakuja na mpya. Ya awali ameshayatekeleza?
Hana tofauti na Aggrey Mwanri RC wa Tabora ambaye akifika site hufoka mno lakini utekelezaji zero.
Lugola mpaka sasa amerukia rukia mambo mengi lakini sioni anachofanikiwa zaidi ya kutoa masaa kadhaa lakini baada ya hapo hurukia mengine.
Sawa tunasubili utekelezaji waziriWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameipa wiki mbili kampuni ya Kimataifa ya Iris Corporation Berhard impe majibu ya kuwa italeta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au Dola za Marekani Milioni 14 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 32 za Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, Dodoma leo,baada ya kikao na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)na viongozi wa Kampuni hiyo, Waziri Lugola alisema kampuni hiyo haiwezi ikacheza na fedha za Watanzania na walipa kodi.
Lugola aliongeza kuwa lazima fedha hizo au mtambo huo upatikane kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitakubaliana na mchezo mchafu wa aina yoyote, na pia yeye kama Waziri wa Wizara hiyo anaendelea kutekeleza maagizo ya Rais Dkt John Magufuli. “Tumezungumza nao na tumekubaliana
Aidha, Waziri Lugola amewataka wamiliki wa kampuni zilizolipwa kifisadi fedha za Mradi wa mtambo wa NIDA kujisalimisha jijini Dodoma Agosti 3 mwaka huu wakiwa na mtambo huo vinginevyo warejeshe fedha zilizotumika.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesisitiza kuwa kutokana na wito alioutoa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu pamoja na Jack Gotham kufika ofisini kwake, wasifanye jaribio la kutokuitikia wito huo, kwani wakifanya hivyo watapata tabu sana.
Ukitoa hapa ukajumlisha pale alafu ukaenda na moja kichwani! Hakuna fedha iliyo potea.Waliocheza na trilioni 1.5 ya watanzania ni watu kutoka nchi gani?
Kuna Uzi mmoja humu Jf ulimzungumziaHuyu Jack Gotham ni nani?
Kaka isije ikawa walishagawana hizo hela kama za Escrow, jamaa wakifunguka kikatokea kigugumizi kwa waziri! ngoja tuone, mi namini hiyo hela haipo kwa sasa!Hakuna mchezo..Hapa kazi tu!
Wa Bombardier na Dreamliner!Hivi kuna angalau mkataba mmoja hapa nchini kwetu ulio safi na wenye manufaa kwa Taifa kweli? I doubt it!