Waziri kortini kwa kupora ardhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri kortini kwa kupora ardhi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 5, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,345
  Trophy Points: 280
  Waziri kortini kwa kupora ardhi


  na Ambrose Wantaigwa, Tarime


  [​IMG] WAZIRI wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka amefunguliwa kesi akidaiwa kuvamia ardhi na kusababisha uharibifu wa mali yenye thamani ya sh milioni 10. Katika kesi hiyo namba 74/2011 iliyofunguliwa katika Mahakama ya Ardhi wilayani hapa ilidaiwa na mlalamikaji, Ally Mrimi, mkazi wa Tarime mjini kuwa waziri huyo alivamia uwanja wake na kusababisha uharibifu huo.
  Mlalamikaji alidai wakati uwanja wake unavamiwa kulikuwapo na mawe, mchanga pamoja na uzio.
  Katika utetezi wake kupitia wakili wa Makowe Chambers Advocates, waziri huyo alikanusha madai hayo na kudai yeye ni mmiliki halali wa uwanja huo kutokana na hati iliyotolewa kisheria namba 23284 iliyotolewa Machi 28 mwaka 2009, hivyo kuiomba mahakama kutupilia mbali madai hayo.
  Aidha, alidai hawezi kulipa fidia inayodaiwa na mlalamikaji kwa kuwa kisheria hakuna sababu ya mdaiwa kulipa fidia kutokana na kosa ambalo hakutenda.
  "Kutokana na ukweli huo wa vielelezo ikiwa pamoja na nakala ya hati ya kumiliki ardhi iliyotolewa kisheria tunaiomba mahakama yako itupilie mbali madai hayo ikiwa ni pamoja na kulipwa gharama za kesi na mdai"� ilieleza sehemu ya hati hiyo ya utetezi.
  Hoja ya kupinga madai hayo, ilieleza kuwa wakala wa Barabara TANROADS ndio wenye dhamana ya kudai eneo hilo kutokana na kuwa eneo la hifadhi ya barabara na si la mlalamikaji.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,345
  Trophy Points: 280
  Kasi ya serikali ya JK kupora ardhi za raia wanyonge kweli sasa inatisha.................................
   
 3. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Utashangaa huyu waziri pamoja na kesi hii hata jiuzulu wala hata wajibishwa! Hiyo ndio nchi yetu ya wadanganyika! Uwajibikaji hakuna kabisa!
   
Loading...