Waziri Kombo awasili Kosovo kwa ziara rasmi

Waziri Kombo awasili Kosovo kwa ziara rasmi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
WAZIRI KOMBO AWASILI KOSOVO KWA ZIARA RASMI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasili jijini Prishtina nchini Kosovo kwa ajili ya kuanza ziara rasmi pamoja na kushiriki Mkutano wa Tatu wa Kimataifa kuhusu Wanawake, Amani na Usalama utakaofanyika nchini humo kuanzia tarehe 2 hadi 3 Juni, 2025.

Ziara hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Kosovo.

Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Prishtina, Mhe. Waziri Kombo amepokelewa na Mshauri wa Rais wa Kosovo masuala ya Sera ya Mambo ya Nje, Bi. Rejhan Vuniqi pamoja na Kaimu Mkuu wa Kituo cha Ubalozi wa Tanzania nchini Italia unaowakilisha pia nchini Kosovo, Bi. Eva Kaluwa.

Akiwa nchini humo, mbali na kushiriki mkutano huo mkubwa wa kimataifa, Mhe. Waziri Kombo atakutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kosovo, Mhe. Dkt. Vjosa Osmani Sadriu pamoja na kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje na masuala ya Diaspora wa nchi hiyo, Mhe. Donika Gervalla Schwarz.

Kadhalika Mhe. Waziri Kombo ambaye kwenye ziara hiyo amefuatana na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizarani, Balozi Swahiba Mndeme na wajumbe wengine atatembelea Chemba ya Biashara ya ushirikiano kati ya Kosovo na Marekani na kukutana na Bodi na Mwenyekiti wa Chemba hiyo, Bw. Arian Zeka.

Aidha, wakati wa Mkutano wa Tatu wa Kimataifa kuhusu Wanawake, Amani na Usalama, Mhe. Waziri Kombo anatarajiwa kuhutubia kwenye Jopo la Majadiliano kuhusu mada isemayo “Utangamano wa Amani katika Karne ya 21: Nini kinahitajika.

Mhe. Waziri Kombo na ujumbe wake watarejea nchini tarehe 04 Juni 2025.
 

Attachments

  • IMG-20250601-WA0039.jpg
    IMG-20250601-WA0039.jpg
    328.1 KB · Views: 18
  • IMG-20250601-WA0038.jpg
    IMG-20250601-WA0038.jpg
    363.7 KB · Views: 16
  • IMG-20250601-WA0040.jpg
    IMG-20250601-WA0040.jpg
    345.9 KB · Views: 17
  • IMG-20250601-WA0041.jpg
    IMG-20250601-WA0041.jpg
    352.3 KB · Views: 18
Ila wewe mwamba na Balozi Kombo hayo sio mapenzi ni mahaba🤣🤣🤣🤣

Mwambie balozi Kombo akaribie sana hapa Kosovo
 
Balozi Kombo atafuta nini kwenye nchi maskini na ilotapakaa mambo ya Rushwa na Ufisadi?
 
  • Kicheko
Reactions: rr4
Balozi Kombo atafuta nini kwenye nchi maskini na ilotapakaa mambo ya Rushwa na Ufisadi?
Umasikini ni mbaya sana ndugu yangu.
Kosovo yenyewe imetoka vitani miaka si mingi. Ajabu tunaenda kwao. Na usikute pia amepewa na bakuli la kutembeza huko kuomba Hela ya kufanyia uchaguzi.
 
Awe makini Cosovo kukinukisha dk sifuri wabishi kama sisi ndio tunaishi hapa ila mzembe mzembe hutoboi wana roho ngumu kama Warusi
 
Umasikini ni mbaya sana ndugu yangu.
Kosovo yenyewe imetoka vitani miaka si mingi. Ajabu tunaenda kwao. Na usikute pia amepewa na bakuli la kutembeza huko kuomba Hela ya kufanyia uchaguzi.
Ajabu sana.

Kwanza Kosovo na nchi zingine zinounda ilokuwa Jamhuri ya Yugoslavia za Serbia, Bosnia-Hercegovina, Montenegro, Kosovo na North Macedonia, pamoja na Albania na Moldova ni viinchi vidogo na maskini.

Pili, hivi viinchi ambavyo haviko kwenye umoja wa Ulaya yaani so wanachama na vyaitwa Non-EU Balkan States.

a hata zile ziloingizwa kwenye EU kama Romania, Bulgaria, Greece, Croatia na Slovenia kwa watu wa West hizo ni tourist destinations ingawa mtazamo huu na masuala ya sasa wa migogoro ya kijiografia zilipaswa kupangaliwakwa jicho la tatu.

Kosovo bado ndani kwenyewe hakujatulia kisiasa na hata nje bado wana mgogoro wa muda mrefu na Serbia yaani mtu waweza kupigwa risasi wakati wowote mtaani mtu akichukizwa (kumbuka vita vya Kosovo watu walihifadhi silaha ndani).

Wakosovo wasumbua nchi za Ulaya magharibi kwa "Organised Crime" yaani uhalifu wa kimataifa na aina zake zote.

Mie naijua Kosovo na nimeishi na jamaa hawa Ulaya wana roho ngumu kichizi mkizinguana ni chuma tu.

Waziri Kombo kwenye hili itakuwa ngumu kwa wafuatiliaji makini kumwelewa afuata nini huko?

Tusikie ametembelea Estonia, Hungary, Romania au Croatia na Slovenia kuna mengi ya kujifunza teknolojia za gharama nafuu, usafiri, ufundi stadi na mengine. Ukipata walimu kadhaa wa ufundi stadi, udereva wa malori ya kisasa na masuala ya teknolojia wakafundisha watanzania litakuwa jambo la mbolea mno.

Ila Kosovo? big no.
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Awe makini Cosovo kukinukisha dk sifuri wabishi kama sisi ndio tunaishi hapa ila mzembe mzembe hutoboi wana roho ngumu kama Warusi
Wakosovo ni watu maskini sana na ndo wanosumbua Ulaya kwa uhalifu na wamejifunza kwa Romania ambao waliingizwa EU mwaka 2000.

Watu wa Romania wengi wameingia kwenye elimu na wana kazi na biashara zao Ulaya.

Kosovo ndo bado wasumbua kinoma.
 
  • Thanks
Reactions: rr4
thabiti kombo mtu poa sana, mbona kikao ni cha wanawake, au mie ndo sijaelewa?
 
Back
Top Bottom