Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Aidha, Dkt. Kijaji aliongeza, “Niwatake waongoza utalii (tour guides) kufuata maelekezo ya askari wa uokoji waliowekwa na TANAPA katika maeneo yote yaliyokumbwa na athari za mvua hizo. Kwani kuvuka madaraja wakati maji yanapita juu ni kuhatarisha usalama wa dereva, watalii pamoja na chombo unachoendesha.”
Naye, Naibu Kamishana wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara - TANAPA Massana Mwishawa alitanabaisha kuwa ujio wa Waziri wa Maliasili na Utalii na kuahidi kutoa fedha hizo kutaondoa changamoto hii na kuifanya miundombinu ya hifadhi kupitika mwaka mzima kuwe na mvua za masika au wakati wa kiangazi.
“Ni matumaini yetu kama taasisi matengenezo ya miundombinu hii iliyoharibiwa itakapokamilika itachagiza ongezeko la watalii na kufikia watalii milioni nane ifikapo june 2030 kama maono ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassani rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alivyoelekeza”.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti Ismail Omary alisema kuwa baada athari hizo, hifadhi ilichukua hatua za matengenezo ya dharura ya madaraja na barabara hizo ili ziweze kupitika, kuweka ulinzi na kutoa malazi ya dharura hostel na Rest house kwa wageni na madereva.
Gharama za fedha hizo bilioni 8.16 zitahusisha ujenzi wa madaraja ya Orangi ya juu, Orangi ya chini, Banagi, Bona, vivuko vya Viboko Naabi, Kalvati katika barabara ya Naabi ha Seronera, pamoja na barabara nyingine zilizoharibiwa na mvua hiyo.