BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,020
- Thread starter
- #21
Ndugu,
Viongozi nao ni raia wa nchi hii na wana HAKI ya kumiliki migodi. Madini ni rasilimali ya WATANZANIA (including hawa viongozi) wote.
Migodi ni kama biashara yoyote ile, pato lake linaingia kwenye mfuko wa Taifa kupitia KODI. Naona tunataka kwenda kwenye enzi ambayo mtu akijituma na kujitahidi kujipatia riziki yake kupitia MIGODI awe adui wa nchi.
Hao wanaolalamika hawajui hata jinsi ya kutafuta claim na kumiliki mgodi. Huo ni uvivu wa fikra...Jitumeni Wajameni.
Kwa hiyo kesho kukigundulika mgodi wa dhahabu wenye kukisiwa una dhahabu ya thamani ya $100 billion na kuambiwa mgodi huo mwenye nao ni Yussuf Manji hakuna tatizo! kukigundulika mafuta Tanzania na ikisemwa kwamba visima vya mafuta vyenye kukisiwa kuwa na mafuta ya thamani ya $1,000 billioni na mwenye navyo ni Manji hakuna tatizo!
Hivi wanavyomuogopa hakuna hata anayemsumbua ili alipe kodi hiyo na miaka inakatika tu, akiwa na visima vya mafuta si ndio watamuona kama Mungu!
Hivi sisi wabongo ni lini tutaacha kuwa wadanganyika!? rasilimali ya Watanzania wote leo mtu kwa kutumia wadhifa wake anasema hili eneo ni langu na kinachopatika hapa ni changu badala ya kuwa pato la Taifa na bado kuna baadhi yetu wanaona hilo ni sawa tu! Duh! bado tuna safari ndefu kweli kweli!