BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,845
Nilishawahi kusikia Mkapa na yule aliyekuwa anampigia debe kwenye kinyang'anyiro cha 2005, A. Kigoda nao wana mgodi wao wa dhahabu. Nilidhani ni porojo tu lakini baada ya kuona hii article inawezekana ikawa ni kweli
Waziri Kapuya aibiwa
na David Frank, Arusha
Chanzo: Tanzania Daima
Waziri Kapuya aibiwa
na David Frank, Arusha
Chanzo: Tanzania Daima
MGODI wa madini ya rubi unaomilikiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya, uliopo wilayani Longido, mkoani Arusha, umeibiwa mashine ya kupulizia hewa ndani ya mgodi (compressor).
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Basilio Matei, zinaeleza kuwa wizi huo ulitokea Septemba 16, mwaka huu, wakati wa usiku katika mgodi huo uliopo katika Kijiji cha Kiseeriani.
Kamanda Matei alisema kwamnba kutokana na tukio hilo, watu wanne wanashikiliwa na polisi. Aliwataja watu hao kuwa ni Nyinyila Mwambasa (31), dereva wa gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 826 AJT, mkazi wa Makao Mapya, Arusha, Daniel Barnabas (2, mkazi wa Lendikinya wilayani Monduli, Lomayani Kalea (25), mkazi wa Buguruni Namanga na Jumanne Ramadhani (26), mkazi wa Arusha.
Akielezea tukio hilo, Kamanda Matei alisema kwamba watu hao baada ya kuiba mashine hiyo walitoroka kwa kutumia gari hilo, lakini walikamatwa walipofika maeneo ya Namanga.
Alisema kwamba wizi huo ulipangwa kwa muda mrefu na baadhi ya watumishi wa mgodi huo kwa kuwa si rahisi kwa watu wa nje kuweza kuingia ndani ya mgodi bila mwenyeji.
Katika tukio jingine, Kamanda Matei alisema kwamba majambazi watatu wakiwa na silaha za moto, jana, walimjeruhi kwa risasi Mhasibu wa kampuni ya Utalii ya Abacombe and Kent ya Arusha, Fabiana Mhindi, wakati akiwa katika gari la kampuni hiyo lililokuwa na fedha alipokuwa akitokea benki ya NBC.
Alisema tukio hilo ambalo majambazi hao hawakufanikiwa kupora fedha zilizokadiriwa kuwa sh milioni 2.8 lilifanyika jana saa 9.45 alasiri, nje ya lango kuu la kuingilia ofisi za kampuni hiyo.
Alisema baada ya mhasibu huyo kufika katika lango hilo akiwa na dereva Athuman Mnyombe (35), aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili T869 AFL wakisubiri kufunguliwa lango hilo, ghafla walitokea watu watatu wakiwa katika pikipiki yenye namba T199 AMB na kuwavamia.
Baada ya kuvamia walifyatua risasi moja hewani ili kuwatisha kabla ya kupiga risasi nyingine katika kioo cha mbele cha gari hilo, iliyomjeruhi mhasibu huyo begani.
Mara baada ya kutokea kwa jambo hilo mhasibu huyo alitoa taarifa polisi waliofanikiwa kuwakamata majambazi wawili kati ya watatu katika eneo jirani na hoteli ya kitalii ya Impala.
Aliwataja watu wanaoshikiliwa kuwa ni Samuel Lucas (23), mkazi wa Sakina Kiranyi na Emmanuel Willium (23), mkazi wa Ekenywa wilayani Arumeru.