Waziri Kapuya aibiwa

Ndugu,

Viongozi nao ni raia wa nchi hii na wana HAKI ya kumiliki migodi. Madini ni rasilimali ya WATANZANIA (including hawa viongozi) wote.

Migodi ni kama biashara yoyote ile, pato lake linaingia kwenye mfuko wa Taifa kupitia KODI. Naona tunataka kwenda kwenye enzi ambayo mtu akijituma na kujitahidi kujipatia riziki yake kupitia MIGODI awe adui wa nchi.

Hao wanaolalamika hawajui hata jinsi ya kutafuta claim na kumiliki mgodi. Huo ni uvivu wa fikra...Jitumeni Wajameni.

Kwa hiyo kesho kukigundulika mgodi wa dhahabu wenye kukisiwa una dhahabu ya thamani ya $100 billion na kuambiwa mgodi huo mwenye nao ni Yussuf Manji hakuna tatizo! kukigundulika mafuta Tanzania na ikisemwa kwamba visima vya mafuta vyenye kukisiwa kuwa na mafuta ya thamani ya $1,000 billioni na mwenye navyo ni Manji hakuna tatizo! :confused:
Hivi wanavyomuogopa hakuna hata anayemsumbua ili alipe kodi hiyo na miaka inakatika tu, akiwa na visima vya mafuta si ndio watamuona kama Mungu!

Hivi sisi wabongo ni lini tutaacha kuwa wadanganyika!? rasilimali ya Watanzania wote leo mtu kwa kutumia wadhifa wake anasema hili eneo ni langu na kinachopatika hapa ni changu badala ya kuwa pato la Taifa na bado kuna baadhi yetu wanaona hilo ni sawa tu! Duh! bado tuna safari ndefu kweli kweli!
 
Unajua the very interesting thing na hizi habari mpya all over sudden, why now sasa tunasikia wazi kuwa waziri ana mgodi wa madini kwa nini hatukusikia media yetu ikisema siku zote? I mean something is not right or is in fact right,

kwa sababu never before tumewahi kusikia haya, kwa hiyo ninaamini kuwa something is up na ni for the good of the people at large, waziri kuwa na mgodi wa madini ni sawa kisheria zetu uchwara, lakini can we look at it deeply kama kweli sheria zote zilifuatwa katika waziri kuupata mgodi huo? Aliupata lini akiwa waziri au before? Kama ni baada ya kuwa waziri aliupataje?

Je toka aupate amekuwa akifuata sheria zote za serikali katika kuwa mmiliki wa mgodi, guys kwa kweli yanayojiri na viongozi wetu ni very interesting, sasa ni wajibu wetu wananchi kuchunguza ukweli ulipo, badala ya kusubiri kina Zitto na Slaa,

Twendeni kazini tuache blah1 blah! hatuwezi kufanyiwa na wengine kila kitu, sasa ni zamu yetu wakuu, tutafuteni dataz tuziweke hapa, media ya bongo watakuja kuzichukua hapa!
 
ES,
right on point bro.....enough with "do nothingism" mindset. Kama CCM wote wangekuwa kama wewe basi gurudumu la maendeleo lingekuwa kileleni saa hii....enough is enough, ili tufanikiwe inabidi partisan politics ziende likizo!!!.
 
Niliwahi kusema hapa sio wana CCM wote ni mafisadi, kuna wengine wengi tu wanaitakia mema nchi yetu. Field Marshall ni mmoja wao. Inatia moyo kusikia mwanachama hai wa CCM anatamka kwamba sihamii chama kingine, lakini kama kungekuwa na uchaguzi hivi karibuni basi ningepigia kura chama cha upinzani kwa matumaini kwamba labda CCM iking'olewa madaraka itaamua kujisafisha ili irudishe credibility yake.
 
Jamaa ana own Mgodi, this is very intresting. Sasa yeye sio mchimbaji holela? Na mbona hafukuzwi kwa sababu migodi inabidi ibinafsishwe? Tanzania inatia kichefuchefu, mungu atunusuru....
 
kuwa na mgodi kwa waziri si tatizo, kwani watanzania wengine wenye mapesa yao pia wana vitega chumi vyengine kama viwanda, biashara kubwa kubwa na hata hiyo migodi yenyewe

tatizo ni kujiuliza hivi, huo mgodi kaupata lini? kwa njia zipi? ni mtaji wa mamilioni mangapi? jee pesa hizo kazipata kwa njia ipi? jee mgodi huo unaingiliana na cheo chake? jee anatumia wadhifa wake kuhakikisha faida kwenye mgodi huo?

ikiwa moja kati ya hayo hapo juu lina walakin, basi waziri wetu huyu inabidi ajieleze kiuwazi kwa wananchi
 
Kwa hiyo kesho kukigundulika mgodi wa dhahabu wenye kukisiwa una dhahabu ya thamani ya $100 billion na kuambiwa mgodi huo mwenye nao ni Yussuf Manji hakuna tatizo! kukigundulika mafuta Tanzania na ikisemwa kwamba visima vya mafuta vyenye kukisiwa kuwa na mafuta ya thamani ya $1,000 billioni na mwenye navyo ni Manji hakuna tatizo! :confused:

Hivi sisi wabongo ni lini tutaacha kuwa wadanganyika!? rasilimali ya Watanzania wote leo mtu kwa kutumia wadhifa wake anasema hili eneo ni langu na kinachopatika hapa ni changu badala ya kuwa pato la Taifa na bado kuna baadhi yetu wanaona hilo ni sawa tu! Duh! bado tuna safari ndefu kweli kweli!

Ndio Hakuna Tatizo! "kukigundulika" - kumbuka wenye kutaka kufanya biashara hizi hufanya utafiti wa kina kujua wapi kunafaa kuchimbwa na kurudisha gharama. Hakuna "kukigundulika". Ondoa mawazo haya na fanya utafiti zaidi.

Sawa ameshagundua...kuna sheria zinazofuatwa ili kuhakikisha nchi inafaidika na ugunduzi na mradi wake. Umesema "kutumia wadhifa wake anasema hili eneo ni langu..." - kuna sheria za umilikaji wa migodi mzee. Mimi naona WEWE bado una safari ndefu, huwezik kupigania haki yako kama hujui hata haki yako ni nini.

Jaribu kufanya utafiti zaidi kabla ya maneno uliyoyasema hapo juu. Ungeweza kupendekeza nini kiongezwe/kirekebishwe katika sheria ya umilikishwaji wa migodi etc lakini ni wazi huelewi hata sheria zilizopo zinasema nini.

Kwani Manji akifuata sheria na akamiliki....na....akapata hela....na akalipa kodi. Kuna ubaya gani? JFYI opponent wake Manji anamiliki migodi mingi tu Tanzania, lakini hii sio ishu.
 
Hivi kuna sheria yo yote inayokataza au kuzuia Tax Returns za makampuni kuchapishwa na vyombo vya habari?

Ninauliza hili ili kuwepo na uwezekano wa makampuni yanayomilikiwa na viongozi yalazimishwe kuchapisha financial statements zao magazetini ili ionekane wamelipa kodi kiasi gani. Hii itazidisha transparency na accountability kwenye uongozi.
 
Ndio Hakuna Tatizo! "kukigundulika" - kumbuka wenye kutaka kufanya biashara hizi hufanya utafiti wa kina kujua wapi kunafaa kuchimbwa na kurudisha gharama. Hakuna "kukigundulika". Ondoa mawazo haya na fanya utafiti zaidi.

Sawa ameshagundua...kuna sheria zinazofuatwa ili kuhakikisha nchi inafaidika na ugunduzi na mradi wake. Umesema "kutumia wadhifa wake anasema hili eneo ni langu..." - kuna sheria za umilikaji wa migodi mzee. Mimi naona WEWE bado una safari ndefu, huwezik kupigania haki yako kama hujui hata haki yako ni nini.

Jaribu kufanya utafiti zaidi kabla ya maneno uliyoyasema hapo juu. Ungeweza kupendekeza nini kiongezwe/kirekebishwe katika sheria ya umilikishwaji wa migodi etc lakini ni wazi huelewi hata sheria zilizopo zinasema nini.

Kwani Manji akifuata sheria na akamiliki....na....akapata hela....na akalipa kodi. Kuna ubaya gani? JFYI opponent wake Manji anamiliki migodi mingi tu Tanzania, lakini hii sio ishu.

Kwa hiyo wewe Tanzania kukigundulika mafuta yenye thamani ya $1,000 billioni na visima hivyo vikiwa owned na Manji badala ya serikali huoni tatizo lolote! ama kweli mvunja nchi ni mwananchi! Huyu huyu manji baada ya kuuza magodown yake kwa shilingi 47 billioni hadi hii leo hataki kulipa kodi ya shilingi 1.3 billion leo unamtegemea awe na visima vya mafuta halafu awe tayari kulipa kodi! :confused:

Mimi haki ninayopigani ni haki ya Watanzania wote ili na wao wawe na kiwango cha maisha ya kuridhisha na hili linawezekana kabisa kama viongozi wakiacha ulafi na ubinafsi wa kujilimbikizia mali. Inakuwaje watu wawe na migodi inayowaingizia mabilioni ya pesa na wakati huo huo asilimia kubwa ya Watanzania wakiishi katika maisha ya dhiki kubwa. Hawajui hata mlo wao mwingine utatoka wapi. Hawajui kodi ya pango wataitoa wapi, hawajui m(wa)toto wao watamsomesha vipi kwa kuwa hawana uwezo wa kumudu gharama za shule, hawajui wakiugua watapata wapi fedha za kujitibu na kununua dawa.

Hakuna haki yoyote ya raia mmoja kumiliki mgodi au migodi ya madini! Hebu wewe unayejua sheria ziweke hizo sheria hapa za watu binafsi kumiliki migodi ili tuzichambue tuone kama zimeweka maslahi ya Watanzania mbele. Nina maswali yafuatayo kwako. Je sheria ya kuruhusu mtu binafsi kuown mgodi ilitungwa mwaka gani? Iliandikwa kwenye govt gazette? Je alinunua mgodi huu kwa kiasi gani na ni nani aliyepanga bei ya mgodi huo? Je mapato nayoyapa anaandika mahesabu (financial statements) kuonyesha kila mwaka amepata mapato kiasi gani, je mtu ambaye hana wadhifa serikalini ana nafasi sawa na kiongozi wa siri kali au CCM kupata mgodi au ndio yale yale ya kujilimbikizia mali, kutoa rushwa na ufisadi wa hali ya juu ambapo mtu wa kawaida hana uwezo wa kuown mgodi? Na huyo waziri analipa kodi inayostahili kwa mfuko wa Taifa au mapato yote anayatia mfukoni bila mfuko wa taifa kuambuliya chochote? Lete hizo sheria kama unavyozifahamu ili tuzichambue. Hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino tunao.
 
Then hao viongozi watasema, biashara fulani ina tax exemption , kumbe sababu ni biashara zao, mkija wengine sheria inabadilika.
So at the end of the day sio kwamba watakuwa wanatetea maslahi ya nchi bali ya kwao.
 
Kiswahili kinakuwa tatizo hata kwa waswahili wenyewe... WAZIRI KAPUYA AIBIWA! mbona taarifa nilizonazo ni kuwa waziri Kapuya leo kapelekwa India kwa matibabu zaidi sasa ataibiwa vipi naomba ufafanuzi hapo..

Kilichoibwa ni hivyo vitu sio waziri...

Teh teh teh teh

Acha mzaha Masatu,

Mbona hicho kiswahili fasaha kabisa?
Kuibiwa vitu ndo nini? Waziri kaibiwa( mali zake)
 
Kwa hiyo wewe Tanzania kukigundulika mafuta yenye thamani ya $1,000 billioni na visima hivyo vikiwa owned na Manji badala ya serikali huoni tatizo lolote! ama kweli mvunja nchi ni mwananchi! Huyu huyu manji baada ya kuuza magodown yake kwa shilingi 47 billioni hadi hii leo hataki kulipa kodi ya shilingi 1.3 billion leo unamtegemea awe na visima vya mafuta halafu awe tayari kulipa kodi! :confused:

Mimi haki ninayopigani ni haki ya Watanzania wote ili na wao wawe na kiwango cha maisha ya kuridhisha na hili linawezekana kabisa kama viongozi wakiacha ulafi na ubinafsi wa kujilimbikizia mali. Inakuwaje watu wawe na migodi inayowaingizia mabilioni ya pesa na wakati huo huo asilimia kubwa ya Watanzania wakiishi katika maisha ya dhiki kubwa. Hawajui hata mlo wao mwingine utatoka wapi. Hawajui kodi ya pango wataitoa wapi, hawajui m(wa)toto wao watamsomesha vipi kwa kuwa hawana uwezo wa kumudu gharama za shule, hawajui wakiugua watapata wapi fedha za kujitibu na kununua dawa.

Hakuna haki yoyote ya raia mmoja kumiliki mgodi au migodi ya madini! Hebu wewe unayejua sheria ziweke hizo sheria hapa za watu binafsi kumiliki migodi ili tuzichambue tuone kama zimeweka maslahi ya Watanzania mbele. Nina maswali yafuatayo kwako. Je sheria ya kuruhusu mtu binafsi kuown mgodi ilitungwa mwaka gani? Iliandikwa kwenye govt gazette? Je alinunua mgodi huu kwa kiasi gani na ni nani aliyepanga bei ya mgodi huo? Je mapato nayoyapa anaandika mahesabu (financial statements) kuonyesha kila mwaka amepata mapato kiasi gani, je mtu ambaye hana wadhifa serikalini ana nafasi sawa na kiongozi wa siri kali au CCM kupata mgodi au ndio yale yale ya kujilimbikizia mali, kutoa rushwa na ufisadi wa hali ya juu ambapo mtu wa kawaida hana uwezo wa kuown mgodi? Na huyo waziri analipa kodi inayostahili kwa mfuko wa Taifa au mapato yote anayatia mfukoni bila mfuko wa taifa kuambuliya chochote? Lete hizo sheria kama unavyozifahamu ili tuzichambue. Hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino tunao.

Kiongozi kama alivyo mtanzania mwingine ana haki ya kuwa na miradi ya kumuongezea kipato. Cha msingi muhukumu kwa kutumia influence ya madaraka kukiuka taratibu za biashara au mradi husika, na si kumhukumu kuwa na mradi huo.

Utajiri hauji kwa vikundi, isipokuwa kutumia fikra na jitihada binafsi katika kufikia malengo yako, leo ukisubiri miradi ya watu ikuletee maendeleo yako binafsi, utakufa maskini. Nani wa kumfanyia kazi mwingine?

Hivi leo tunataka mtu ambaye ameingia madarakani akiwa na miradi yake binafsi inayompa pesa nyingi, aiuze au agawe mali zake hizo? Mambo hayawezi kwenda namna hiyo.

Kama mtu kawekeza kwenye mafuta yakagundulika kuwa na hifadhi kubwa, unataka serikali iutwae huo mradi? Unakumbuka yaliyotokea kwenye azimio la Arusha? Hicho ndo kilichofanyika, miradi ikafa hatimaye wakaingiza wanachoita UBINAFSISHAJI.

Kama kuna kampuni au mtu halipi kodi, huo ni udhaifu wa mamlaka zetu. Ni mara ngapi tumesikia nchi za watu watu wakifilisiwa au mali zao zikiuzwa kwa kukwepa kodi? Tukifikia hatua hiyo, watu watakuwa wanapeleka wenyewe kodi kabla hawajafatwa.

Na ndo hapo dhana ya kutengeneza mabilionea itafanikiwa, watatoa ajira kwa wengi na huenda nawe "Bubu ataka kusema" na wengine watajikuta maisha yamekuwa bora. Kwani kwa Mengi kuwa na pesa wangapi wamefanikiwa kuwa na maisha bora? Wengi tu! Tukiwa na watu kama hao laki moja, TUTAENDELEA.
 
Sikusema kwamba viongozi wasiwe na miradi ya kuwaongezea mapato. Ninachosema madini ni rasilimali ya WATANZANIA WOTE na wala siyo ya viongozi na watanzania wachache watakaotumia nyadhifa na utajiri wao kujipatia migodi hiyo.

Hivyo kwa maoni yangu migodi yote ndani ya Tanzania inastahili kuwa owned na serikali badala ya mtu mmoja. Watanzania wengi wanaishi katika maisha ya dhiki kubwa kwa kisingizio cha umaskini wa nchi yetu, lakini hili si kweli umaskini huo unasababishwa na ulafi wa ufidasi wa viongozi wachache kujilimbikizia utajiri uliokithiri badala ya kuhakikisha utajiri wa Tanzania unawanufaisha Watanzania wote bila kujali nafasi zao za uongozi au hali yao kifedha. Hao viongozi wanaweza kuanzisha miradi mingine chungu nzima lakini migodi iachwe ili imilikiwe na WATANZANIA WOTE.
 
Strong Points!, wakuu hebu jiburudisheni kidogo na hizi points za wakuu wa dini!

1. serikali kutoa tamko linaloeleweka na la wazi kuhusu tuhuma za ufisadi zinazowakabili baadhi ya watendaji wake badala ya kuendelea kukaa kimya. serikali inapaswa kujibu hoja za Mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa badala ya kumnyamazisha kwa kumtishia kumshtaki.

2. "Serikali itoe tamko linaloeleweka kuhusu utata wa mkataba wa mgodi wa Buzwagi, wasimtishe Dk Slaa kwa kukimbilia mahakamani maana yeye hawezi kutoa hoja za kitoto kwani ni msomi kama wao,"

3. serikali inatakiwa ieleze bayana namna mgodi wa Buzwagi unavyomnufaisha Mtanzania au hata Wasukuma na Wanyamwezi wenye ardhi yao katika mgodi huo.

4. taasisi mbalimbali kusimama kidete na kutoa matamko kuikumbusha serikali wajibu wake katika kutetea maslahi ya taifa na watu wake, badala ya maslahi ya kikundi kidogo cha watu.

5. "Tutawezaje kuondokana na viongozi wabovu wanaowatumikisha wananchi badala ya kuwatumikia, kama si mashirika na wadau wa maendeleo kupiga kelele?"

6. tabia ya watu wachache kunufaika na rasilimali za nchi huku wengine wakibaki kuwa maskini na kuipeleka nchi pabaya. tabia hiyo sio tu inaliongezea taifa umaskini bali pia inaleta utumwa kwa taifa mbele ya mataifa mengine na isipodhibitiwa ni hatari.
kwa nini kusiwe na uwiano wa matumizi ya rasilimali za nchi kati ya wazawa na wageni?"

7. hoja nzito kama za ufisadi zinatakiwa kusimamiwa na viongozi wa dini kwa kuzihubiri katika sehemu zao za ibada ambako wahusika wanaabudu ili wabadili tabia. "Mafisadi wana imani zao na wanaabudu, viongozi wa dini wakihubiri hoja hizo huenda zikafika kwa walengwa mapema zaidi kuliko wanasiasa,"

8. tafiti zilizofanywa hivi karibuni zimeonyesha kuwa asilimia 38 ya bidhaa zote zinazoingizwa nchini ni bandia.

9. ni ukweli usiopingika kwamba mikataba mingi nchini haiwanufaishi wananchi. mbali na ubovu wa mikataba, woga wa watendaji katika kusimamia ukweli na tabia yao ya kujikomba kwa serikali na kusahau maslahi ya wananchi pamoja na maamuzi ya kushitukiza ni baadhi ya mambo yanayoleta umaskini nchini. watendaji wengi wanatumikia matakwa ya serikali badala ya wananchi na hawana uchungu wa kutetea maslahi ya nchi, zaidi ya kujilimbikizia mali na kutafuta madaraka.

10. "Inakuwaje nchi ina polisi, usalama wa taifa, Takukuru, wataalam na viongozi wa ngazi zote ishindwe kudhibiti ufisadi kama siyo kutokuwa na moyo wa kizalendo?"
 
I didnt know kama tuna wawekezaji wazawa kwenye migodi, anyway huyu naye ana mkataba na serikali lakini umefanywa kuwa siri?

Kama wameiba watanzania, tugeuze maneno iwe wamechukua kwani wao ndio wezi wakubwa wa mali zetu. Jamani ni bora muwe mnawafata hao hao msije mtaani kwani na wao wanatuibia, especially Kara na RA bila kumsahau EL.
 
Kiongozi kama alivyo mtanzania mwingine ana haki ya kuwa na miradi ya kumuongezea kipato. Cha msingi muhukumu kwa kutumia influence ya madaraka kukiuka taratibu za biashara au mradi husika, na si kumhukumu kuwa na mradi huo.

Mkuu hakuna anayepinga kuwa ni haki yake kisheria zetu uchwara kuwa na mgodi, isipokuwa katika mchezo wa siasa inapotokea ishu kama ya mafisadi, na mkataba wa Buzwagi, politically correctness ni kwamba inaondoa imani ya wananchi kwa viongozi wao,

Kwa hiyo ili kuirudisha imani hiyo ya wananchi kwa viongozi wao, serikali kwa kuutmia vyombo vyake vya kisheria, inatakiwa kujisafisha kila kona, ikiwa ni pamoja na kuweka wazi mali za viongozi wetu na uhalali wao kisheria kumiliki mali hizo, ikiwa ni pamoja na kutuhakikishia kuwa walizipata kwa njia za haki kisheria, na kwamba wanazimiliki kwa kufuata masharti yote ya serikali bila kupindishwa, na walizipata lini wakiwa mawaziri au wakiwa wananchi tu wa kawaida?

kwa sababu kama wanaweza kuzipindisha sheria zetu ili kuwapa wageni kumiliki madini yetu, itakuwaje wakiimiliki wao wenyewe viongozi kama vile huo mgodi wa Kapuya?
 
Watu hawapingi viongozi kuwa na mali au kumiliki hivyo vitu, the problem ni transparency katika kuvipata hivyo vitu na muendelezo wake katika nyanja za kiuchumi, kama kodi, foreign currency control na flactuation of the currency, mikopo kama tulivyo ona wa Mzindakata....na impact yake kwa mtanzania wa kawaida eg mtu achukue mkopo mahali ashindwe kuulipa then serekali ibebe hilo jukumu, au mtu kwa uzembe wake ashindwe kuendesha biashara yake vizuri, then serekali imsaidie kwa kumfutia kodi, ni kumpa mtaji kwa mlango wa nyuma at your expense.
 
Hawawezi kuweka wazi jinsi walivyomiliki hii migodi kwa sababu hawakufuata sheria za nchi na wamejipendelea wakubwa na labda matajiri, ndio maana wengi wetu tunashangaa kusikia Kapuya ana mgodi wake. Na sia ajabu wenye migodi wako wengi tu, lakini kwa sababu ya usiri mkubwa uliokuwepo hatuwajui ni akina nani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom