Waziri Jafo asema atabandika majina hata ya wale waliojitoa na kura zitapigwa

CCM wan shida sana. Ukitaka kugombea, wanatoa jina lako. Ukisema sasa nawaachia, wanakulazimisha ugombee... Kwenye mtu mwenye fitina, hata ufanye nini atakuchokonoa tu.
 
Haijatumika demokrasia kuwakataza watu wasigombee

Mbowe ametumia ubabe
Wewe si urukeruke kwa furaha. Shida ipo wapi. Ubabe wa Mbowe chadema wanauheshimu. Ubabe wa magufuli CCM na watendaji wanauheshimu. Shida ipo wapi. Mtu anachezea maji wadai anakutimulia vumbi. Acha ujinga dogo
 
Sio siri kwenye usimamizi wa mambo mengine Jafo alionyesha ubora na kwanini anastahili nafasi ile kwa kazi nzuri aliyo ionyesha.

Ila kwa hili la zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa, kauli zake na maamuzi yake yanaonyesha sauti ni ya kwake ila mipango haijui na ni ya wengine.

Mimi binafsi nimemsamehe japo najua analinda ugali wake huku anamwaga wa wengine.

Screenshot_20191109-175440_Facebook~3.jpeg
 
Ikitokea majina ya wagombea wa vyama vilivyojitoa kwenye uchaguzi yakawekwa kwenye karatasi la kura kama Jaffo alivyosema na wananchi wakayapigia na kushinda. swali ni je vyama hivyo na wagombea wao watakuwa na ujasiri wa kugomea kuongoza wananchi?
Mkuu hii haikuwa na sababu ya kuanzisha uzi wake, ungeenda kwenye ule uzi wa Jaffo kubandika majina ya wagombea wote na kuuliza hili swali.

Asante.
 
Jafo Yuko sahihi.

Mchakato ulishakamilika .
Mtu aliyegombea ndiye anatakiwa atangaze kujitoa sio atolewe na Chama Hadi dakika hi hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyetangaza yeye binafsi kujitoa kwa wasimamizi wa uchaguzi.Swala la kujitoa ni.la mgombea sio Chama.Chama hakikuomba kugombea.Na hakuna mahali kwenye fomu ya kugombea ambapo Chama kiliomba kugombea

Thanks
 
Mwananchi yeyote akikushauri, ushauri wake unaweza kuchukuliwa na kufanyiwa kazi au kutofanyiwa kazi. Nakushauri Mhe. Waziri kwa heshima na taadhima huu uchaguzi ufutwe na mchakato mzima uanze ili uchaguzi ufanyike mwanzoni mwa mwaka 2020 baada ya kukutana na Vyama vyote na kukubaliana, vinginevyo uchaguzi ukifanyika kama ulivyopangwa itakuwa ni aibu kwa Taifa nzima maana naona wapiga kura wengi watasusia kupiga kura. Nawasilisha.
 
Marehemu kafa we unamupa asimamie mirathi ,hapo chacha nani kachanganyikiwa ? Mtoa agizo hilo au marehemu we jafo vipi
 
Na wakikubali wakati wa uchaguzi wataibiwa kistaarabu kweli, msitu uleule, nyani walewale, miti ilele unategemea nini wakati lengo halijabadilika
Hata ukishinda rufaa hutashinda kwenye kura, wanachotaka kuwe na wagombea kwenye uchaguzi lakini walibug kuwatoa mapema sasa wanataka kusahahisha makosa yao
 
INA MAANA KUNA MGOMBEA BINAFSI BILA KUPITIA CHAMA CHA SIASA.HII LUGHA KUWA CUAMA NDICHO KIMEJITOA,ILA WAGOMBEA WANAENDELEA ,IMEKAAJE?Bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa hauruhusiwi kugombea.hivyo chama kikisema basi najitoa,automatically na wewe mgombea huwezi kuendelea
 
Jafo Yuko sahihi.

Mchakato ulishakamilika .
Mtu aliyegombea ndiye anatakiwa atangaze kujitoa sio atolewe na Chama Hadi dakika hi hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyetangaza yeye binafsi kujitoa kwa wasimamizi wa uchaguzi.Swala la kujitoa ni.la mgombea sio Chama.Chama hakikuomba kugombea.Na hakuna mahali kwenye fomu ya kugombea ambapo Chama kiliomba kugombea

Kwa hiyo mgombea anawakilisha/anadhaminiwa na chama au Serikali?
 
Tatizo sio yeye ni anaemtuma
Hiki ndicho alichokuwa anamaanisha Matola katika post yake leo asubuhi. He is well informed. Hatari sana hii nchi. Sijui inashindikana nini waziri huyu kukaa meza moja na hawa wadau wanaolalamikia rafu hizo ili kuaddress concerns zao, badala yake wanalazimisha uhuni?
 
INA MAANA KUNA MGOMBEA BINAFSI BILA KUPITIA CHAMA CHA SIASA.HII LUGHA KUWA CUAMA NDICHO KIMEJITOA,ILA WAGOMBEA WANAENDELEA ,IMEKAAJE?Bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa hauruhusiwi kugombea.hivyo chama kikisema basi najitoa,automatically na wewe mgombea huwezi kuendelea
Mkutano mkuu wa Chama Cha siasa pekee ndio wenye uamuzi mzito Kama huo .Hilo jambo linatakiwa kuamriwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama wa kutoka kila Kona ya nchinsababu Ni la kitaifa na linahusu kila Kona ya nchi .Chadema na ACT hawajaitisha mkutano mkuu wa taifa wa dharura kutoa huo uamuzi wa kujitoa kwenye uchaguzi

Kwa mambo ya kawaida Kamati ki ndio hutoa matamko Hilo la kujitoa uchaguzi Ni zaidi ya uwezo wao.
 
Hii inaweza ikawa ni fursa adhimu ya kuwaonyesha watawala maana halisi ya nguvu ya umma, kama majina ya waliojitoa yakiwekwa napendekeza upinzani kwa umoja wao wawaeleze wafuasi wao pamoja na wengine wote wapenda demokrasia siku ya kupiga kura wakae nyumbani au wakapige kura za maruhani
 
Chama kimeondoa udhamini wake kwa mgombea anawezaje kuendelea kuwa mgombea wa hicho chama? Hivi zenu akili zimeshikiliwa na ccm?
Ukiwa kule unajitoa ufahamu akili wamewekeza kwenye ahadi ya kazi walizoahadiwa mwaka wa 4 sasa comrades wanasubiri
 
Walikuwa na tatizo la kujiandikisha! walijua watakosa uhalali wa takwimu

Sasa wanatafuta uhalali wa Wagombea, wanajua bila Wapinzani haramu itabaki kuwa haramu

Wanataka majina yawekwe ili uchaguzi uwe na sura ya vyama vingi , wahalalishe 99%
 
Back
Top Bottom