Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

Mkuu, niambie kosa la huyo Dada. Hao watoto wamejieleza wazi sababu za wao kuona wanachukiwa na Baba zao.

Au kwa mtazamo wako ulitaka aseme na ambao wanachukiwa na mama zao watoke mbele?
Makosa la huyo dada yamekwisha ainishwa kutoka kwa wachangiaji waliotangulia. Ila kwa ufupi makubwa ni :-
1. Kuwahoji mbele ya wanafunzi wenzao, hii yaweza kusababisha wakawa "bullied"
2. Kuwarekodi na kutawanya clip bila consent ya wazazi wote wawili
3. Kusikiliza watoto bila baba zao hivyo kuvunja kanuni ya audi alteram partem (hear the other side)
 
Huyu dada apigwe stop haraka sana anachofanya ni makosa makubwa mno.
Migogoro ya familia wanayoijua ni baba na mama. Hapo baba hajapewa nafasi ya kusilizwa anahukumiwa!!??
Huu ujinga anaofanya huyu dada aache mara moja ama apate consultatin kutoka kwa wataalam wa mambo husika.
This is not professionalism kutoka kwa huyu mtangazaji. Kaibuka na wazo lake bila kufanya consultation na wataalam husika
 
Hili ni lifeminist tu linajikuta linamshirikisha Mungu kwenye mambo ya kipumbavu, mara nyingi au mara zote baba kukataa kuhudumia mtoto hapo ujue chanzo ni mama sema madingi hatunaga time ya kuzungumzia yanayotusibu tunakausha na Mungu ndo muamuzi.

Feminist huyu ni wa kupuuzwa hayo maombi yenyewe ukiyaangalia kwa jicho la tatu ni ya mchongo, maombi kashayafanyia rehearsal kayakariri mpuuzi mmoja wa kupuuzwa.
Hudumieni watoto bwana.
 
Wanaume walee watoto mama .wasikupotoshe .mleta mada anatetea watelekezaji watoto.kwani ni siri baba za hao watoto si hawatoi malezi.??
Miss wewe endelea kutafuta! Huoni kama ni udhalilishaji wa watoto huo? Kwanza ana-share picha zao kwenye ma-group amepata wapi hiyo consent?
 
Miss wewe endelea kutafuta! Huoni kama ni udhalilishaji wa watoto huo? Kwanza ana-share picha zao kwenye ma-group amepata wapi hiyo consent?
Nitatafuta hadi nikupate.tunzeni watoto bna.acheni kumwaga mbegu na.kupita hivii.hivi damu yako siku 365 kwa.mwaka hujui anakula nini .tena unafanya miaka hata 20 for real.mna.mioyo gani wenzetu..?
 
Hudumieni watoto bwana.
tunahudumia ila ukitaka uishi na mtoto ili umhudumie vizuri unaletewa nyodo za kijinga ili aendelee kula mpunga wa matumizi ya mtoto.

kwanza ukiona mwanamke kazaa na mwanaume kabla ya ndoa afu akaachwa bila kuolewa ujue kuna hitilafu mahala. Aiona unafuu kwa hiyo akaachia goli maksudi kutegea mimba anadhani ndo tiketi ya ndoa hajui kuwa wanaume mafala ni wachache hapa duniani yaani hatununuagi mbuzi kwenye gunia, mambo ya kibadilika mnang'ang'ania watoto na nyodo kibao,

hayo maneno hao watoto wanayasema yote wamelishwa na mama zao wawachukie baba zao, kisa baba zao waligoma kuwaoa mama zao kwa sababu hawana akili wala maadili.

wanawake wanaoachwa kwa kuonewa ni wachache na huwa wanakubaliana na hali zao maisha yanasonga, ila ukiona janamke linawalisha sumu ya chuki watoto, hilo ni gumegume lililoachwa kwa sababu halifai kuolewa na halitaolewi ng'o
 
Mkuu, niambie kosa la huyo Dada. Hao watoto wamejieleza wazi sababu za wao kuona wanachukiwa na Baba zao.

Au kwa mtazamo wako ulitaka aseme na ambao wanachukiwa na mama zao watoke mbele?
Yani we Robert pamoja na mathread yako marefuuuu unayoandikaga humu ila kuna kuna tu vitu tu dogo dogo hutujui na hutuelewi na tuna ku out smart! We hujaona kosa hapo??
 
Kwanini hakujiongeza japo awafiche sura zao?
Screenshot_20231019-043546.png

Pili, kwanini mambo ya Familia za watu ayaongelee kwenye kadamnasi bila kusikiliza pande zote?

Hawa watoto watanyanyasika kisaikolojia Shuleni. Watakuwa wanaambiwa na wenzao "Ndo maana baba yako hakujali, lione hilooo". Mambo ya watoto shuleni wote tunajua. Inaweza pekekea hata wasiwe wanaenda shule. Pia inaweza ongeza mgogoro kwenye familia.
 
Ni kweli kabisa unayoyasema. Kama hujaoa mwombe sana Mungu akupe mke mwema vinginevyo ni hatari ya kifo. Tena wengine wanakuvuruga kwa kushirikiana na mama yake mzazi. Utaomba ardhi ipasuke ujifukie. Kina mama wengi wameharibu maisha ya watoto wao kipuuzi kabisa.
Kuomba Mungu ni muhimu sana mkuu, lakini pamoja na yote ni kutambua nafasi Mungu aliyotupa sisi kama wanaume, ni kubwa sana. Binafsi ninao wivu mkubwa sana juu ya nafasi yangu kama mwanaume katika kila kitu, kimajukumu na hata kimaamuzi.
 
Yani mtu unaweza kuwa na akili nzuri ya darasani ukajua mambo mengi ila ukishaingiza chuki za kidini basi akili zinapotea..hiyo bibi ni ana chuki mnoo..huyo hafai kwenye jamii iliostaarabika
Naunga mkono hoja 👍👏
 
Ahsante Sana ku save ndugu yangu, itakusaidia wewe na wengine wa karibu yako ambao, huwa naumia Sana kusikia mtu mmoja mwenye shida na jambo ambalo liko ofisini kwangu halafu bahati mbaya hajapata msaada katika mfumo rasmi halafu anaanza kulia peke yake hajui rufaa aifikishe vipi kwangu kwa haraka.

Huwa nikiona mtu mmoja kaamua ku save, huwa naamini nyuma yake wako kumi kama siyo 20. Umoja wetu ni nguvu yetu wala na ni msingi katika kusukuma mbele maendeleo na ustawi wa jamii na kupambana na kero kero za kutengenezwa na baadhi ya wasio na Nia njema

Angalizo; Msipige Bali tumeni UJUMBE tafadhali. Na vema zaidi WhatsApp kwa kuwa naipata popote. Nikiwa nje ya nchi kama hivi sms za kawaida saa ingine mtihani. Ila Nina namba ingine pia ya 0734124191. Sms pia.

Ila call center yetu ni 0734986503 na 026 2160250. Saa za kazi siku za kazi. Kuna 116 kwa ajili ya taarifa za ukatili kwa watoto, siku zote saa 24.

Mkumbuke kuna namba ya IGP pia, 0699 998899.

Tukl vizuri kudhibiti wababaishaji na wanaoonea watu. 🇹🇿🤝

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Naunga mkono hoja 👍👏
 
Hivi wewe unafikiri ukiumbwa mwanamme basi ndio kila mwanamke alietoka ubavuni mwako ndio utakuwa unamuongoza tu ?

Kwani huyo mwanamke aliyeumbwa aliambiwa awe na kisirani na tabia mbaya kwa mwanaume zaidi ya kumtii mwanaume.

Wewe unaonekana unajua sana ya ndani kwako ila sio yanayokuzunguka, wewe unafikiri wazazi wote wa kike uwa wanawaambia ukweli watoto wao zaidi ya kuwalisha sumu na je unajua nguvu ya Mama katika kushawishi mtoto wake ? Na inawezekana hao watoto wengine wazazi wao wametengana tokea watoto wapo bado wadogo, baba anapeleka msaada kwa ajili ya mtoto mama anatupa na kukataa msaada kutokana na kisirani na tabia mbaya ambayo umeitaja (Sina shida na msaada wako sishindwi kumlea mtoto wangu koma kama ulivyokoma kunyonya ziwa la mamayako, Usije ukasababisha nikaachika kwa mume wangu wa sasa kwanza huyu mtoto umkome sio wako nilikulambisha tu asali)

Ndugu sasa unataka kulazimisha matunzo mpaka mahakamani wakati mahakama yenyewe isharidhika kuwa mama yeye gangwe na anaweza kumudu kumlea mtoto.

Hakuna sababu zisizokuwa na mashiko ndio maana welevu wa jamii wameshaliona hilo.
Mkuu, ni wanaume dhaifu tu ndio hukimbia watoto wao na kisha kuleta sababu hizi ambazo umeleta wewe.

Halafu hizi hadithi za mtoto kulishwa sumu nimeshawahi kusema humu, ukiona mtoto wako amelishwa sumu na mama yake kuhusu wewe ni ushahidi tosha ulikuwa hutimizi majukumu yako kama Baba.

Kama unataka kulea mtoto wako na mzazi mwenzako hataki anasema anamudu matunzo, afanye hivyo kukiwa na mashahidi ili baadae ikusaidie kukusafisha kwa mtoto. Akisema mtoto sio wako na wewe unaamini ni wako, hujui ni nini cha kufanya? Wanaume hatususi mkuu.
 
Alichofanya sio kizuri kinajenga picha/ taswira mbaya kwahao Watoto nankitawaathiri katika makuzi yao
 
Back
Top Bottom