Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,112
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Geoge Simbachawene ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata watuhumiwa waliowashambulia wapenzi wakiwa kwenye faragha wakidai kuwa wamewafumania.
Ametoa agizo hilo leo Agosti 6, 2021 jijini Dar es Salaama baada ya kuiona video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha kundi la watu wakiwavamia wapenzi hao na kuwadhalilisha.