Waziri G. Kabaka atembelea Vodacom ghafla

Waziri G. Kabaka atembelea Vodacom ghafla

Au kushusha salari pia ni kosa la waziri? hivi wewe hujiulizi kwa nini erolink inajadiliwa sana kuliko recruitment agencies zingine? Au wewe ndio katika wale wanaosema tatizo ni lake kwako halikuhusu? Hatutaki ndugu zetu waje kunyonywa kama sisi. Kama wewe kwenu mambo safi na mboga 7 ubarikiwe mkuu.
 
Kiranga mtetezi wa EROLINK inaonekana wewe huna hata chembe ya huruma kwa wavuja jasho kama sisi. Kwa mantiki hiyo mimi sidhani kama naweza kujadili kitu na mtu katili kama wewe. Nimeamini unaweza ukasoma ukawa na cheti lakini ukawa huna common sense. Kama kuwa great thinker ni kuwa mtetezi wa uozo kama huu sidhani kama kuna haja ya kupoteza energy kwako. Binafsi katika hili niko muwazi kwamba waziri yuko right no matter what you talk bado point inabaki kwamba Erolink ni wanyonyaji. Nikikutoa wewe na rutta the rest ya walochangia wanaafiki kwamba Erolink ni wanyonyaji. Hivi ushawahi kuona mahali popote duniani mshahara unashuka badala kuongezeka? Erolink walitushushia mshahara mwaka jana mpaka sasa basic ni 250000 upo hapo? Usitetee kitu ili mradi tu ndugu

Tushaongelea habari za Erolink kabla hata ya raid ya huyo Waziri, nikalaani unyonyaji sio Tanzania tu, bali ulimwenguni pote.

Sio tu nimewasema vibaya hao Erolink, nimeusema vibaya mfumo mzima wa uwakala unaofanya kuwapo kwa middle men wanaokinga mkono kuchukua kipato cha wavuja jasho katika mtindo endelevu. Nikamtaja mpaka Pope Emeritus Benedict XVI kwamba katika mambo machache niliyokubaliana naye papa mwenzangu, moja ni hili la kutopenda mawakala wanaofanya watu wasiwe na permanent employment, wanafanya kazi kama viraka tu.

Perchance Nyani Ngabu will recall, maana aliniuliza namaanisha Pope huyu wa sasa au Pope Emeritus.

Kwa hilo huwezi kusema Kiranga anatetea Erolink na unyonyaji, ukisema hivyo utakuwa one track minded, unaona mtu yeyote anayemsema Waziri ni mtetezi wa Erolink bila kujua kwamba inawezekana Erolink wakawa wanyonyaji na Waziri akakosea kuwashikisha adabu.

This is not an either or question, why do you want to make it one? George Bush style "If you are not with us, you are with the terrorist" ?

Habari za kushuka mishahara, mawakala kuchukua cha juu na lack of transparency tushazikemea sana na Consigliere EMT hapa, nafikiri ni wiki ya jana kama si ya juzi if I am not mistaken.

Kwa hiyo ukisema mimi natetea mawakala unakosea sana.

Mimi mwenyewe ni mvuja jasho na nishafanya kazi kupitia mawakala, niwatetee kwa kisa gani?

Lakini hilo halina maana Waziri mzima ajiingize katika raid halafu mimi ni support. Strategically Waziri hatumii muda wake vizuri, anahatarisha usalama wake, anatumia fedha za walipa kodi vibaya, anabahatisha bahatisha ili kupata results, anaendekeza maigizo kuliko kazi, ana risk kuwekwa mapokezi na kuambiwa mabosi hawapo, anapunguzia hadhi ofisi ya waziri, anachukulia wengine kazi zao hizi za kufanya raids, anaipa serikali bad publicity kwamba ni serikali inayofanya kazi informally shaghalabaghala kwa mawaziri wake kujizukia tu sehemu bila miadi, anaingilia process nzima kutoka ngazi ya juu sana bila kuangalia dispute resolution pointers wala criminal justice system proceedings kwa kutaka kufanya upolisi bila mafunzo.

Anazua ma issue kibao!

Mimi hata kama ni Marxist nut ninaye salute kila siku asubuhi "Workers of the world, unite, you have nothing to lose but your chains" siwezi kum support huyu Waziri kufanya raid. Kwa sababu strategically ata undermine haki za wafanyakazi kwa kuanza kuwapa hawa mawakala msemo kwamba wanaandamwa unfairly na politically, ndiyo maana kazi ya polisi unaona anakuja kuifanya Waziri.

We don't need brute force and showism. We need smarter ministers who can do much without the need of empty overhyped drama.
 
Matokeo machache yaliyojitokeza baada ya ziara ya waziri jana
1. Vodacom yaanza kufanya uhakiki wa michango ya nssf/ppf
2. Erolink wadai huwa wanapeleka mafao lakini hawapeleki
3.erolink wathibitika bila kificho,wanapiga panga mishahara ya wafanyakazi. Kwa mujibu wa takwimu kichwa kimoja kinapata take home kati ya 650000 -700000
4. Mafao ya uzazi,matibabu ,posho na marupurupu mengine erolink wanapewa na vodacom lakini wanatia mfukoni mwao

Mnaotetea erolink teteebi na haya
 
so ulitaka waziri apange appoinment na wezi ...wezi huwa wanazukiwa tu uwape taarifa ili wapate ya kujitetea ...

Baadhi ya wabongo never stop to amaze me the way they think.

You mean "wezi" operating legally in the country?

Yaani waziri mzima badala ya ku-deal na "wezi" anawatembelea hao "wezi"? What for?

Ama kweli ndo maana nchi imejaa "wezi" b'se badala ya kuwatokomeza mnawaruhuhusu kuendeleza "wizi" wao legally.

Wengine hata wanawalipa hao "wezi" wako kwenye simu, internet na mazagazaga mengine.

Vipi kama hao "wezi" wakipiga risasi huyo waziri huko kwenye maskani yao na kufa kwa kuwaingilia kichwa kichwa?

Huu ni upepo utapita tuu. Hata mama Tibaijuka alikuja kwa staili kama hiyo kwenye wizara yake, kwani unamsikia tena na mikwara yake?

vo4.JPG
 
Mnaotetea erolink teteebi na haya

Mkuu sidhani kama kuna anayeitetea Erolink na hayo makampuni mengine unless awe na interests huko. Nimesoma michango mingi kwenye hili suala, na wengi wamejikita upande mmoja tuu wa tatizo, probably kwa kuzozea kujadili matukio.

Wengine tunatwanga kotekote, with no apology. No doubt kuwa practice za Erolink na hayo makampuni mengine zilikuwa kinyume na expectations za Watanzania wengi, hasa wale waliojiriwa kupitia kwenye hayo makampuni. Lakini at the sometime, raia yoyote anayo haki ya kuihoji serikali how come imeibiwa hizo alleged 3 billions na hayo makampuni? How come government authorities failed to ensure that those companies abide with the rules and regulations?

Parliament made law, kazi ya executive ni ku-enforce hiyo sheria na mahakama to interpret and apply the law. So far ni makampuni mangapi ambayo yameshafikishwa mahakamani na serikali kwa kuvunja sheria husika? Nitakuwa nimekosema kama nikisema uamuzi wa serikali "kusitisha mara moja utaratibu wa Mawakala kuwaajiri wafanyakazi wanaowatafutia kazi" badala ya ku-enforce sheria husika ni usanii?

Ripoti ya wizara husika inadai kuwa "utaratibu wa kukodisha wafanyakazi unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira ni kinyume cha Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999"

Inaendelea kusema kuwa, "kwa mujibu wa Kifungu 4 cha Sheria hiyo, majukumu ya msingi ya Wakala wa Huduma za Ajira ni kuwaandaa na kuwaunganisha Watafuta Kazi na Waajiri kwa kutoa mafunzo na ushauri elekezi kwa watafuta kazi, kutafuta fursa za ajira na kutoa taarifa za soko la ajira. Hivyo, Mawakala hawapaswi kuwa waajiri wa wafanyakazi waliowatafutia kazi kwa niaba ya Waajiri wengine."

As a common man in the street, I cannot hold liable those companies for their malpractices, but definitely I can hold liable the government liable kwa kuibiwa shn bilioni 3 na hayo makapuni na for failing to ensure that they follow the law and regulations pertaining in the relevant industry. Serikali ilikuwa wapi muda wote wakati wao na raia wanaibiwa mchana kweupe?

Serikali haiwezi kujipendekeza kwangu kama raia kwa kudai eti "imeamua kusitisha mara moja utaratibu wa Mawakala kuwaajiri wafanyakazi wanaowatafutia kazi" halafu hapo hapo ikadai kuwa "utaratibu wa kukodisha wafanyakazi unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira ni kinyume cha Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999".

Serikali itasitishaje kitu ambacho tayari kilikuwa kimeshasitishwa/katazwa na sheria? Kama sheria inasema usipite hapa na wewe ukakaidi na kupita sitapitisha amri ya kukusitisha wewe kupita hapa, bali nita-enforce sheria inayokukataza kupita hapa kwa kukufikisha kwenye vyombo husika vya sheria ili uadhibiwe kwa mujibu wa sheria. Wapo ambao watakakubali kudanganywa, lakini siyo mimi.
 
Baadhi ya wabongo never stop to amaze me the way they think.

You mean "wezi" operating legally in the country?

Yaani waziri mzima badala ya ku-deal na "wezi" anawatembelea hao "wezi"? What for?

Ama kweli ndo maana nchi imejaa "wezi" b'se badala ya kuwatokomeza mnawaruhuhusu kuendeleza "wizi" wao legally.

Wengine hata wanawalipa hao "wezi" wako kwenye simu, internet na mazagazaga mengine.

Vipi kama hao "wezi" wakipiga risasi huyo waziri huko kwenye maskani yao na kufa kwa kuwaingilia kichwa kichwa?

Huu ni upepo utapita tuu. Hata mama Tibaijuka alikuja kwa staili kama hiyo kwenye wizara yake, kwani unamsikia tena na mikwara yake?

Wabongo wengi wanapenda show, ukiwaambia wachague kati ya mtu anayechapa kazi kwelikweli lakini hataki show na mtu ambaye ana show tupu lakini hafanyi kazi watachagua yule mwenye show.

Kwa sababu vichwa vingi vinatazama mambo kwa juu juu tu.

Ndiyo maana unakuta watu wengi wanaweza kushabikia upuuzi kama Waziri kuvamia ofisi za watu, it has that showism and shock value.

Wakati Waziri angeweza kufanya hayo hayo, na hata zaidi, bila ya kupoteza muda wake na kujidhalilisha kwa kuwa part of a raid kama mbwa wa polisi.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mkuu sidhani kama kuna anayeitetea Erolink na hayo makampuni mengine unless awe na interests huko. Nimesoma michango mingi kwenye hili suala, na wengi wamejikita upande mmoja tuu wa tatizo, probably kwa kuzozea kujadili matukio.

Wengine tunatwanga kotekote, with no apology. No doubt kuwa practice za Erolink na hayo makampuni mengine zalikuwa kinyume na expectations za Watanzania wengi, hasa wale waliojiriwa kupitia kwenye hayo makampuni. Lakini at the sometime, raia yoyote anayo haki ya kuihoji serikali how come imeibiwa hizo alleged sh. bilioni 3 na hayo makampuni? How come government authorities failed to ensure that those companies abide with the rules and regulations?

Ripoti ya wizara husika inadai kuwa "utaratibu wa kukodisha wafanyakazi unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira ni kinyume cha Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999"

Inaendelea kusema kuwa, "kwa mujibu wa Kifungu 4 cha Sheria hiyo, majukumu ya msingi ya Wakala wa Huduma za Ajira ni kuwaandaa na kuwaunganisha Watafuta Kazi na Waajiri kwa kutoa mafunzo na ushauri elekezi kwa watafuta kazi, kutafuta fursa za ajira na kutoa taarifa za soko la ajira. Hivyo, Mawakala hawapaswi kuwa waajiri wa wafanyakazi waliowatafutia kazi kwa niaba ya Waajiri wengine."

As a common man in the street, I cannot hold liable those companies for their malpractices, but definitely I can hold liable the government liable kwa kuibiwa shn bilioni 3 na hayo makapuni na for failing to ensure that they follow the law and regulations pertaining in the relevant industry. Serikali ilikuwa wapi muda wote wakati wao na raia wanaibiwa mchana kweupe?

Serikali haiwezi kujipendekeza kwangu kama raia kwa kudai eti "imeamua kusitisha mara moja utaratibu wa Mawakala kuwaajiri wafanyakazi wanaowatafutia kazi" wakati hapo hapo ikadai kuwa "utaratibu wa kukodisha wafanyakazi unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira ni kinyume cha Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999".

Serikali itasitishaje kitu ambacho tayari kilikuwa tayari kimeshasitishwa/katazwa na sheria? Wapo watakakubali kudanganywa, lakini siyo mimi.

I knew there was a reason I had to drag Consigliere in here for the legal angle.

Thank you.

Ndiyo maana mimi nikahoji, kama serikali ina ushahidi kwamba hawa watu ni wezi, kwa nini wasipelekwe polisi pale kukamata watu na proceedings za kesi zianze?

La, kama serikali haina ushahidi, Waziri kuvamia kutasaidia nini? I can understand squad ya wakazi ikivamia kukamata makabrasha kwa court ordered warrant and all, if at all that was the case, Waziri anafanya nini kwenye raid kama hiyo?

Au ndiyo zile habari za yule Sheriff aliyependa sana sifa ambaye kila askari wake wakienda kufanya uvamizi sehemu, akijua tu kwamba waandishi wa habari na wapiga picha watakuwepo, alikuwa anasubiri mhalifu kashikwa na a liutenant, yeye anaenda kupiga naye picha tu ili aonekane magazetini?

Kama watu wamevunja sheria, waziri anaenda hapo kufanya nini? Anaenda kukata nao deal ale mlungula na kwaachia off the hook? Maana ma conspiracy theory mengine mtu anaweza kuyaalika hivihivi kwa kutaka sifa.

Kwa nini wasiachie mkondo wa sheria ufuatwe?

Natafuta kuelewa Waziri kafuata nini huko sioni, naona kujipelekapeleka kwa Waziri kunazua maswali mengi kuliko majibu.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kazi kwelikweli.Huu ndio mwaka 2014 na tunaendelea kufanya maobi tuondokane na udhalimu huu ulikithiri.Imefikia hatua watu wanautaka ukwasi hata kwa kuua ili mradi malengo yatimie.Mungu tunusuru na janga hili la ajira za kinyonyaji
 
Lkn kuna rumors kwamba kama erolink wataondolewa pale voda kati ya wafanyakazi 500 walioajiriwa na erolink voda ina mpango wakubaki na wafanyakazi 200 tu ili kupunguza ulipwaj wa kiasi kikubwa cha kodi na mambo ya bima ya watu 500 so kuna uwezekano watu 300 kurud mtaan kuanza hustleln na upya
 
Ni afadhali kuliko kuwa na wafanyakazi 500 unaowalipa sh mia mia...
 
Wasipoondolewa hao wakoloni tutakufa jamani kwa sababu hiyo laki mbili kwa mwezi ni majanga.
 
Back
Top Bottom