Waziri G. Kabaka atembelea Vodacom ghafla

Waziri G. Kabaka atembelea Vodacom ghafla

Niko pamoja na waziri katika hili unyonyaji haukubaliki nchi hii kama wewe unataka kunyonywa mpaka usiwe na maendeleo tetea dhulma za hawa erolink. Tena kama inawezekana waziri ushitukize na tena ukipata muda. Mtu anayetetea unyonyaji ana maslahi yake binafsi hapo.
 
Sijaona kosa la waziri mpaka sasa. Angekuwa anatetea matajiri kuna watu wangemsifu hapa na unafiki wao. Lakini kwa kuwa katika janga hili akina kajambanani tuko wengi ndo maana wengine wanatafuta namna ya kumkosoa waziri ili aonekane ana makosa. Unyonyaji tunaupinga kwa nguvu zote na haukubaliki kabisa. Mwaka huu kitaeleweka tu.
 
Mtu kama huyu kawapa sababu watu hata kama ni wezi, kujibu kila swali lake kwa jibu moja tu.u

"Hatuna jibu kwa sasa, hatukutegemea ujio wako, tunahitaji muda zaidi kukupatia taarifa".

Then the whole exercise, in so far as the element of surprise is concerned, is null. It's not like this is some Vita Vya Kagera battle where one has to surprise Amin or something, this war is fought by using the law.

Unaweza kwenda ofisini kwa mtu ghafla aka file suit ya harassment na tresspassing, akakuzuia usifanye chochote mpaka awepo mwanasheria wake. Sema huko bongo tu ambako mawaziri ni kama miungu watu ndo waziri anaweza kuja ghafla ghafla tu. Waziri anazuka ghafla tu watu wana mkutano wa multi hundred million dollar deals? Anapigwa chini vizuri tu, bila hata soda.

Unless Waziri anakuja na search warrant na polisi, ili kusearch premises in a surprise visit, sioni point ya surprise.

Wabongo tushazoea kupelekana kama ng'ombe, ndiyo maana watu wanasifia haya.

Na mwisho wa siku unaweza kuambiwa ni mchezo wa kuigiza tu, hakuna lolote la maana kimsingi litakalofanyika.

Huku watu wanachekelea mpaka jino la mwisho.

Juvenal said it best, give them bread a circuses.

Except we don't even get the bread.

Only circuses.

Bad circuses at that!

mtu ambaye hajawahi ku exprience shida utamjua tu ...naona unavyowatetea hawa wapigaji kwa kiingerezq chako cha mbwembwe
 
Mkuu Kiranga. Jua waziri hakutaka kuonana na yeyote kwa lolote. Hakutaka doc yoyote kutoka kwa yeyote na taratibu zote anazijua kwani ni mara yake ya kwanza kufanya ziara? Kama maisha kwako mazuri basi acha wanyonge nao wapate unafuu hata wa macho tuu. Pole maana inaonyesha dhahiri ni muhanga wa yatakayotokea. Ila ndo ishakua.
 
Haswaa inaoneka labda na yeye ana maslahi kama mwenzie ruta lakini haki lazima itendeke mwaka huu unyonyaji sasa basi inatosha
 
Inasikitisha sana kuona Mtanzania akibeza bidii na njia za Waziri kuokoa wananchi wa Taifa lake wasinyanyaswe.
 
Sana mimi nakwambia watu kama hawa hata udiwani hawastahili kupewa. Sisi tunaongea kuhusu kuutokomeza unyonyaji jitu zima na akili zake linatetea upuuzi tu. Na ukiona mtu anatetea ubuuzi ujue hapo kuna maslahi binafsi. Na isitoshe waziri alishapata ushahidi kitambo.Uchunguzi ulianza toka mwaka jana wa hii ishu.Waziri ana uhakika na anachokifanya na nyinyi mnaotetea unyonyaji teteeni tu kama mna 10% zenu poleni, haki lazima itendeke. Ni bora wafanyakazi 500 waliopo sasa wakomeshe unyonyaji huu kuliko miaka ijayo wafanyakazi 2000 wawe outsourced na kunyonywa, tunachopigania hapa ni kwamba sheria ifatwe na unyonyaji ukome kabisa
 
Wakuu hebu wale mliopita makampuni haya hasa Erolink angalieni salary slip zenu mbona kwenye hizo salary zenu mnakatwa VAT. So hawa jamaa wanazipelekwa wapi?
 
Kwa mmfumo wa mashirika ulivyo Dunianu,ni vigumu sana kwa hao wafanyakazi 500 au wowote wa aina yao ku-win, hao Vodacom watafanya kila wawezavyo kupunguza OPEX, si ajabu ukasikia simu yako ya kastama kea inapokelewa na mnyarwanda au Mkenya.na hao ndugu zako 500 wakawa wako barabarani hawana kazi. Kwenye uchumi wa ki-ushindani nivigumu kupangia mashirika mishahara. kwa hiyo kama tatizo ni hao watu kulipwa 270K, serikali itafute njia nyengine ya kuifanya hiyo 270K itoshe, kama kupunguza inflation na kuboresha huduma za jamii, mashirika makubwa sio kama serikali yetu ambako kuna njemba zinaamua tu kupandisha mafao kutoka milioni 60 hadi 160 eti zilizokuwepo hazitoshi. Shareholders wa vodacom hawataruhusu upuuzi huo.

hapa waziri yuko kwenye wakati mgumu sana, kwani hao vodacom watamkubalia, watawachukua hao watu, wata-watrench wote, watafunga kambi ya kastama kea.watapeleka hizo kazi kwenye gharama nafuu.Mkipokelewa simu na wakenya msilie.

Mwenye makosa hapa ni EROLINK na ndio kabaka alikotakiwa afunge ziara ya kustukiza, ili ahakikishe wafanayakazi iliowaajiri wanapewa haki zao stahili.

pole sana kwa wahanga wa hili, ila mjue dunia nzima iko hivi, hata huku tuliko kila simu unayopiga kastama kea inapokelewa na wahindi/wapakistani. na mawaziri wao hawana cha kuwafanya hawa jamaa.wanatumia njia nyengine kuwabana,lakini sio kuwazukia maofisini kwao.
 
Ngedere akila sana, iko siku ya kujuta.
Kujuta kujuta sana,mwenye shamba akistuka. Mtego atawekewa, tunduni aje kunaswa.
Wamenyonya vya kutosha, sasa lazima walipe.

Huruma sikuonei, hata kama kwa mtutu.
Halali yangu ulimi, wala situmii sumu.
Nitaitumia akili, kudai kilicho changu.
Ero umenichosha kweli, mtetezi nimempata.

Kelele tulizipiga, jamani mnatunyonya.
Masikio mkaziba, mkiendelea kula bata.
Dharau mkazileta, eti baki au nenda.
Mungu sio mdhalimu, leo katusikiliza

Tunayo mengi madai, Ero wanatunyanyasa.
Laki mbili na ushee,eti ndio mshahara.
Ukiumwa kafe mbele, hapa simu kwenda mbele.
Tutazamacho ubao, sifuri level ni mwiko.
Anzia moja hadi tisa, ni kuimba na wateja.

Hatuna cha sikukuu, siku zote jumatatu.
Tuko hapa sita siku, nani akupe pumziko.
Hata mwili ukichoka, lazima uusukume.
Vinginevyo ukikacha, kazi tena ndi basi.

Waziri kaza msuli, kuondoa unyonyaji.
Kina Ero na wenzake, funzo hili walipate.
Usije legeza kamba, ndegere ataponyoka.
Ili hili liwe funzo, hata kwa vizazi vyetu.

Wenzangu Tutulizane, mechi ndio imeanza.
Lazima tupate bingwa,hata kama kwa penati.
Waziri ni refa wetu,huyu hatatuangusha.
Ero na mama Kabaka, ni nani tabeba kombe.

Huu ni mwisho wa hawa kupe. Wameshanyonya sana watoto wa watu sasa yanawatokea puani. Mtu amefanya kazi miaka mitatu anakatwa kodi,nssf/ppf akienda kuangalia anaambiwa hauna contribution yoyote. Etuimuongezewe muda bila hata aibuuu. Nakuomba muongee na waziri bila hata aibu.... sio siri chozi la mtu linathamani sana. Wengi wamelia na hii erolink. Na waweke Mafao ya wafanyakazi kabla hawajaondoka..
 
Hizi ziara za ghafla hawa mawaziri kuna siku wataaibika.

Unakwenda ofisini kwa watu na liziara lako la ghafla, unawakuta watu wameshapanga ratiba ya siku nzima wako kwenye mipango mingine, Waziri mzima unaachwa mapokezi unasoma gazeti.

Kwani kupanga mkutano kuna ugumu gani?

Na kuviziana viziana ghafla kuna ulazima gani?

Halafu, I am all for serikali kuhakikisha wananchi hawanyonywi, kwa kuweka mazingira hayo (sheria na miongozo mingine). Lakini hii habari ya serikali ku micromanage haiendani na mfumo wa soko huria ambao serikali inajinadi kwa wawekezaji kila siku.

Serikali haiwezi kuingilia utendaji wa makampuni, inatakiwa kuweka sheria na kama makampuni hayafuati sheria, mkondo wa sheria ufuatwe.
Kauli yako inaashiria ni kwa namna gani unafaidika na utaratibu uliopo na unaoumiza wengi ndani ya nizi Employment Agencies.

Kumbuka kuwa Waziri wa Kazi na Ajira yuko kwenye harakati za utekelezaji wa majukumu yake hususani katika Kusimamia Utekelezaji wa Sheria za Kazi.

Kwa mujibu wa Sheria za Kazi, Waziri wa Kazi pamoja Maafisa wa Kazi wanaofanya kazi chini yake wote kwa pamoja hawalaziki kutoa taarifa kwa Mwajiri juu ya ziara inayotaka kufanyika, inaweza kutolewa kulingana na kinachoenda kufanyika.

Waziri na Maafisa wake kutoka Idara ya Kazi wanaruhusiwa kuingia kwa Mwajiri yeyote, muda wowote na kufanya Uchunguzi/Ukaguzi na hiki ndicho kilichofanyika; haijalishi ni nani atakutwa sehemu ya kazi, awe mhudumu, receptionist, meneja au mkurungenzi wote ni wateja wake.

Kitendo cha wewe kulalamika juu ya ziara ya WAZIRI kinatia mashaka; ila kwa kukushauri tu, jenga tabia ya kuwa unapitia Kanuni na Sheria za Kazi, hususani Sheria ya Taasisi za Kazi Na.7 ya 2004 na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya 2004 zitakusaidia hata na wewe kutambua Wajibu pamoja Hazi zako.

Hitimisho:
Hawezekani mtu anaajiriwa na hizi Employment Agency kama kampuni binafsi na kupelekwa kufanya kazi kwenye Sekta ya Fedha au Sekta ya Mawasiliano ambapo mishahara yao inakuwa wazi kwa mujibu wa Sekta husika kwa mujibu wa Amri mpya ya Mishahara(Wage Order) ya Mwaka 2013 lakini mtu analipwa Sh.100,000 ukiuliza Meneja au HR anakwambia yeye hajawaajiri ila wameletwa na Kampuni nyingine ya Uajiri (kama-Out-sourced employees) kitendo ambacho kinakiuka taratibu na Sheria za Nchi. Lazima haki za Wafanyakazi zilindwe bwana.
 
Nimeandika hapo juu kuhusu uhalali wa vyombo vya dola vya ngazi husika kuvamia sehemu hizi kwa mujibu wa sheria, hilo sina tatizo nalo.

Kama wewe hujasoma hilo, hilo ni tatizo lako, si langu.

Waziri si mtendaji, ni mwanasiasa, sasa anavamia ili iweje? Anataka kukwida watu awaweke kwenye karandinga? Anataka kubeba maboksi yenye documents?

Waziri kageuka polisi?

I don't have a problem with raids, so long as they are warranted and are conducted lawfully. Kuna investigations nyingine haziwezi kuhakikiwa bila ya raid, na kuna investigations nyingine kupanga miadi ni kumpa taarifa mlengwa afiche ushahidi muhimu, ndiyo maana kuna kitu kama "surprise audit".

Tatizo langu ni hii micro management, Waziri kashindwa ku delegate hii kazi mpaka aende kufanya raid yeye mwenyewe?

Akitolewa ngeu na walinzi wa huko si yatakuwa mambo ya aibu haya? Kesho kwenye headlines "Waziri wa Tanzania atolewa ngeu na mlinzi kwa kuvamia ofisi bila miadi".

Ridiculous.

We will be the laughingstock of the world.

Nchi kibao watu wanafanya hizi labor raids, hata Marekani wanakojifanya kuwa liberals kwenye mambo ya labors washafanya labor raids kuangalia habari za illegal immigrants.

Sijawahi kusikia Waziri kajishusha kujiingiza katika a raid in this style.

Huyu Waziri anaonesha hana kazi au hajui kupanga jinsi ya kuutumia muda wake vizuri, kwa sababu ukishafanya a surprise raid kwa nia ya kukutana tu, hujapata miadi, obviously upande unaokutana nao utakuwa haujajiandaa kukujibu productively na utakuwa umeupa excuse ya "this is a surprise, we need time".

Na kama ni raid ya kutaka ku seize documents/ evidence Waziri has no business beiong in that raid. Not is he/she is efficient and focused on solving ministerial level challenges.

What's next? Waziri afukuzane na wezi barabarani?
 
Mkuu Kiranga. Jua waziri hakutaka kuonana na yeyote kwa lolote. Hakutaka doc yoyote kutoka kwa yeyote na taratibu zote anazijua kwani ni mara yake ya kwanza kufanya ziara? Kama maisha kwako mazuri basi acha wanyonge nao wapate unafuu hata wa macho tuu. Pole maana inaonyesha dhahiri ni muhanga wa yatakayotokea. Ila ndo ishakua.

Sasa kama Waziri hakutaka kuonana na yeyote kwa lolote alikwenda kufanya nini??!
 
Sijaona kosa la waziri mpaka sasa. Angekuwa anatetea matajiri kuna watu wangemsifu hapa na unafiki wao. Lakini kwa kuwa katika janga hili akina kajambanani tuko wengi ndo maana wengine wanatafuta namna ya kumkosoa waziri ili aonekane ana makosa. Unyonyaji tunaupinga kwa nguvu zote na haukubaliki kabisa. Mwaka huu kitaeleweka tu.

Mambo hayako kirahisi hivyo mdogo wangu. Unyonyaji ni dhana pana sana! Pengine ungesema mlipwe malipo ya haki kulingana na nguvu kazi na ujuzi wako!
 
Nimeandika hapo juu kuhusu uhalali wa vyombo vya dola vya ngazi husika kuvamia sehemu hizi kwa mujibu wa sheria, hilo sina tatizo nalo.

Kama wewe hujasoma hilo, hilo ni tatizo lako, si langu.

Waziri si mtendaji, ni mwanasiasa, sasa anavamia ili iweje? Anataka kukwida watu awaweke kwenye karandinga? Anataka kubeba maboksi yenye documents?

Waziri kageuka polisi?

I don't have a problem with raids, so long as they are warranted and are conducted lawfully. Kuna investigations nyingine haziwezi kuhakikiwa bila ya raid, na kuna investigations nyingine kupanga miadi ni kumpa taarifa mlengwa afiche ushahidi muhimu, ndiyo maana kuna kitu kama "surprise audit".

Tatizo langu ni hii micro management, Waziri kashindwa ku delegate hii kazi mpaka aende kufanya raid yeye mwenyewe?

Akitolewa ngeu na walinzi wa huko si yatakuwa mambo ya aibu haya? Kesho kwenye headlines "Waziri wa Tanzania atolewa ngeu na mlinzi kwa kuvamia ofisi bila miadi".

Ridiculous.

We will be the laughingstock of the world.

Nchi kibao watu wanafanya hizi labor raids, hata Marekani wanakojifanya kuwa liberals kwenye mambo ya labors washafanya labor raids kuangalia habari za illegal immigrants.

Sijawahi kusikia Waziri kajishusha kujiingiza katika a raid in this style.

Huyu Waziri anaonesha hana kazi au hajui kupanga jinsi ya kuutumia muda wake vizuri, kwa sababu ukishafanya a surprise raid kwa nia ya kukutana tu, hujapata miadi, obviously upande unaokutana nao utakuwa haujajiandaa kukujibu productively na utakuwa umeupa excuse ya "this is a surprise, we need time".

Na kama ni raid ya kutaka ku seize documents/ evidence Waziri has no business beiong in that raid. Not is he/she is efficient and focused on solving ministerial level challenges.

What's next? Waziri afukuzane na wezi barabarani?
.........Dr. Mwakyembe amekua akivamia Bandarini-TPA na pale TAZARA(TRL) kungalia kasi ya utendaji kazi na hatimaye kushauri kitu ambacho kimepelekea matatizo kupungua kwenye hizo taasisi; Waziri wa Kazi akifanya hivyo kuna tatizo gani???? pamoja na kuwepo kwa Concept ya Delegation of Power si kila kitu kinafanyiwa Delegation kiongozi.

Bado nasisitiza tusimuonee huruma Waziri kwamba akiwa na ziara kama hizo anaweza kuvamiwa na vibaka au wahuni wa mitaani, kusema hivyo ni kumtisha na kumuwekea mipaka katika utendaji wake.
 
Anacho kifanya Mwakyembe siyo sahihi na lazima niseme uongozi wa aina hiyo hauwezi hata siku moja tusaidia kama taifa. Kiongozi mzuri ni yule anaye jenga taasisi imara chini yake! Na sikustuka alipogombana na Bodi tena mpya ambayo yeye alishiriki kuunda.
 
Two wrongs do not make a right, Dr. Mwakyembe kuvamia haifanyi kuvamia kwa Waziri kuwe sawa.

Delegation si kila kitu, lakini habari za kwenda kuruka ukuta na kukwida wezi akitaka kuzifanya mwenyewe Waziri nitamuona ana wrong priorities.

Muda aliotumia kwenda kufanya raid angeweza ku conference na watu kibao, angeandika na kusoma vitu kibao, angeonana na watu kibao in a productive setting.

Kuvamia ndo anaenda kuambiwa bosi hayupo, mimi sekretari tu, mlango umefungwa, hatukujua kwamba kuna ugeni leo", atafanya nini?

Suala si kumuonea huruma Waziri, suala ni kuwaonea huruma Watanzania ambao pesa yao ya kodi inatumika kufanya maigizo haya ya mchana kweupe kwa kutumia muda adimu wa Waziri wakati kuna watu kibao wangeweza kufanya raid na kumletea taarifa zote Waziri.

Waziri anataka kuwa movie star, John Wayne style.

Ufanisi hautaki kufanya kazi kwa nguvu na fujo, unataka kufanya kazi kwa akili.

Kesho keshokutwa kesi inawekwa mahakamani, some clever defense attorneys are given reason to frame this as an unorthodox crusade using undue government resources to victimize their clients in a political witchhunt.

Waziri kashafikiria yote hayo na kuona kuwa chess la ku deal na corrupt businesses linahitaji more than brute force?
 
Anacho kifanya Mwakyembe siyo sahihi na lazima niseme uongozi wa aina hiyo hauwezi hata siku moja tusaidia kama taifa. Kiongozi mzuri ni yule anaye jenga taasisi imara chini yake! Na sikustuka alipogombana na Bodi tena mpya ambayo yeye alishiriki kuunda.

Thank you.

Watu tunataka mambo yote yafanywe na waziri tu, siku waziri akiumwa wizara nzima imelala.

Ndio uongozi tunaoutaka huu?
 
Kiranga mtetezi wa EROLINK inaonekana wewe huna hata chembe ya huruma kwa wavuja jasho kama sisi. Kwa mantiki hiyo mimi sidhani kama naweza kujadili kitu na mtu katili kama wewe. Nimeamini unaweza ukasoma ukawa na cheti lakini ukawa huna common sense. Kama kuwa great thinker ni kuwa mtetezi wa uozo kama huu sidhani kama kuna haja ya kupoteza energy kwako. Binafsi katika hili niko muwazi kwamba waziri yuko right no matter what you talk bado point inabaki kwamba Erolink ni wanyonyaji. Nikikutoa wewe na rutta the rest ya walochangia wanaafiki kwamba Erolink ni wanyonyaji. Hivi ushawahi kuona mahali popote duniani mshahara unashuka badala kuongezeka? Erolink walitushushia mshahara mwaka jana mpaka sasa basic ni 250000 upo hapo? Usitetee kitu ili mradi tu ndugu
 
Back
Top Bottom