Waziri Dkt. Mpango: Watendaji wa Hazina kuweni makini zaidi Serikali bado inaibiwa sana kwenye miradi ya Halmashauri

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
Waziri wa fedha Dkt. Mpango amewataka watumishi wote wa Hazina kuwa makini zaidi kwa sababu fedha nyingi za serikali bado zinapotea kwenye miradi inayotekelezwa kwenye halmashauri.

Dkt. Mpango amesema Serikali inahitaji fedha ili kukamilisha miradi ya kitaifa ikiwemo ujenzi na ukarabati wa meli, ujenzi wa SGR, ununuzi wa ndege 5 nk hivyo haitavumilia uzembe wowote unaopelekea upotevu wa mapato ya serikali kwenye matumizi.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Huyu Mpango mbona anajidhalilisha kwa kufuata ya JPM kutaka kununua ndege wakati hizi tulizonazo hazitumiki to full capacity! Mshauri boss wako mzitumie hizo fedha kupunguza umasikini unaosema umekumbana nao huko kwenu ulipokuwa unaomba ubunge! Kununua ndege wakati huu ni upoyoyo wa hali ya juu hasa kwa nchi Masikini kama Tanzania.

Sometimes be bold enough and tell your boss the truth, if he has any brains he will respect you! When you keep quiet when things go wrong when you could have given wise counsel, you are abusing your integrity.
 
Zinapoteaje tena, wakati nidhamu ya watumishi wa umma,imeongezeka na mianya ya rushwa imezibwa, au ilikuwa ni kwa baadhi ya kada pekee. Ilianza kujengewa nidhamu?
 
Mbona tuliambiwa wizi umedhibitiwa serikali kwa sasa chini ya awamu hii ya tano? Au amejisahau kwenye hiyo propaganda mfumo?
 
Mbona tuliambiwa wizi umedhibitiwa serekali kwa sasa chini ya awamu hii ya tano? Au amejisahau kwenye hiyo propaganda mfumo?
Kudhibitiwa haimaanishi kuwa wizi umekwisha!

Tena zile halmashauri za wapinzani ziliongoza kwa ubadhirifu!
 
Nakubaliana na Waziri Mpango kwa asilimia 100

Serikali inapigwa kinoma

Kwenye miradi ya ujenzi vinara wa upigaji ni PMU, Works department & User departments - sytle ya upigaji ni ten percent (wanakula michongo na contractors, consultants, supplier wa material, na nk.)

Kwa miradi isiyo ya ujenzi ambayo mingi inapatikana kwenye sekta za elimu na afya wapigaji ni user departments husika - sytle ya upigaji ni miposho tuu (unakuta sehemu kubwa ya mradi ni posho)
 
Huyu kiazi katangazwa na Halmashauri kuwa mbunge.

Hii ni sawa na mtoto kutukana utupu wa mama yake ambayo ndio njia iliyotumika kumleta duniani.
 
Back
Top Bottom