Dkt. Mpango amuwakia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Aliyedai Hawaoni Juhudi za Serikali Kukamilisha Miradi ya Mkoa Huo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,060
49,744
My Take
Hata Mimi naungana na VP Mpango ,kusema kwamba haoni ni uongo mkubwa na muendelezo wa ubishi,ujuaji na ujeuri wa watu wa Mkoa wa Mbeya.

Kiufupi ni utovu wa Nidhamu.

Katika kipindi ambacho Mbeya imependelewa Kwa miradi ni awamu hii ya 6 ambayo Spika anatoka Mkoa huo.

---

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameonesha Kutofurahishwa na kauli ya mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi Mkoa wa Mbeya Dkt Stephen Mwakajumilo kwamba hawajaona juhudi zozote ambazo zinachukuliwa kukamilisha baadhi ya miradi ya Mkoani humo

Dkt Mpango amesema Mkoa wa Mbeya na Mikoa yote nchini Kuna miradi mingi ya Maendeleo inayotekelezwa katika sekta mbalimbali ya Miundombinu, Maji, Umeme, Afya na elimu licha ya kwamba Nchi ina mahitaji makubwa, hivyo mwenyekiti kiu yake ni kutaka kuona miradi mingi inatekelezwa.

My Take
Hata Mimi naungana na VP Mpango ,kusema kwamba haoni ni uongo mkubwa na muendelezo wa ubishi,ujuaji na ujeuri wa watu wa Mkoa wa Mbeya.

Kiufupi ni utovu wa Nidhamu.

Katika kipindi ambacho Mbeya imependelewa Kwa miradi ni awamu hii ya 6 ambayo Spika anatoka Mkoa huo.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya mpaka leo hajui kua ni jinai kuikosoa CCM?
 
Hivi umemuelewa huyo mwenyekiti??
Au kisa kawapiga kwenye mshono mkuu, yeye kasema yale aliyoona hayajaendelezwa huyo Mpango kasema kipi ametekeleza kama sio kaleta siasa na mwisho kusema ccm oye??

Sio ujeuri, na hili ndo tatizo lenu mkiambiwa ukweli mnasema watu jeuri.
 
Taja yaliyofanywa mkuu. Mwenyekiti yupo sahihi
Ukienda Rungwe na Kyela Kuna miradi 3 mikubwa ya Barabara za lami mikubwa,2 TanRoads na 1 Tarura hapo sijasema iliyokamilika

Juzi tuu hapa VP kazindua mashine ya MRI Rufaa Mbeya

Hospital ya Mkoa CT Scan imeanza kufanya kazi

Barabara ya Njia 4 imeanza kujengwa ,mkataba wa Igawa-Tunduma uko tayari

Mradi mkubwa wa Maji kutoka Rungwe Hadi Mbeya unaendelea

Serikali ya Mama imekamilisha uwanja wa Songwe runway,jengo la Abiria,imefungwa taa na Sasa wanajenga cold room

Mwisho Kuna miradi mingi midogo midogo isiyo na idadi.
 
Huyo mwenyekiti atakuwa Msafwa tu ndio sababu haoni maendeleo yanayoletwa na akina Spika Dr Tulia Mwansasu PhD, Nabii na Mtume Mwamposa na Mnec Richard Kasesela 😄😄🔥
 
Kumbe
Huyo ndio mwenye chama ana fursa ya vikao Hadi vya Kitaifa Kwa nini asikosoe huko? Nidhamu ya chama inasemaje? Hata kwenye ngazi ya familia hakuna ujinga wa hivyo
CCM inatakiwa kuikosoa mafichoni!! Mpo nyuma ya muda san dunia ya leo sio ile ya 1977, makosa now hayajifichi yatatolewa hadharan tu hata ukiyaongelea chooni!!
 
Hivi umemuelewa huyo mwenyekiti??
Au kisa kawapiga kwenye mshono mkuu, yeye kasema yale aliyoona hayajaendelezwa huyo Mpango kasema kipi ametekeleza kama sio kaleta siasa na mwisho kusema ccm oye??

Sio ujeuri, na hili ndo tatizo lenu mkiambiwa ukweli mnasema watu jeuri.

Hivi umemuelewa huyo mwenyekiti??
Au kisa kawapiga kwenye mshono mkuu, yeye kasema yale aliyoona hayajaendelezwa huyo Mpango kasema kipi ametekeleza kama sio kaleta siasa na mwisho kusema ccm oye??

Sio ujeuri, na hili ndo tatizo lenu mkiambiwa ukweli mnasema watu jeuri.
VP is undefined..sio mpole na sio mkali, sio mkweli na sio muongo, sio mwenye afya na sio mgonjwa, sio mwenye akili na sio mjinga, sio malaika na sio shetani...
 
Naunga mkono hoja, mbeya ni moja ya majiji hovyo kabisa.

Hadi leo bado wapo na single lane. Foleni za kipuuzi kabisa. Achilia mbali uchafu. Kimsingi serikali imewakomoa wananchi wa Jiji la Mbeya kwa muda mrefu sana.

Waineeni huruma
Kwani hujui kwamba Kuna Ujenzi unaendelea hapo?
 
My Take
Hata Mimi naungana na VP Mpango ,kusema kwamba haoni ni uongo mkubwa na muendelezo wa ubishi,ujuaji na ujeuri wa watu wa Mkoa wa Mbeya.

Kiufupi ni utovu wa Nidhamu.

Katika kipindi ambacho Mbeya imependelewa Kwa miradi ni awamu hii ya 6 ambayo Spika anatoka Mkoa huo.

Spika anatoka Mbeya kweli, kwani kaongeza kitu gani? Hebu tuondolee hicho kigagula hapa
 
Back
Top Bottom