Waziri Dkt. Mpango: Watendaji wa Hazina kuweni makini zaidi Serikali bado inaibiwa sana kwenye miradi ya Halmashauri

Waziri wa fedha Dkt. Mpango amewataka watumishi wote wa Hazina kuwa makini zaidi kwa sababu fedha nyingi za serikali bado zinapotea kwenye miradi inayotekelezwa kwenye halmashauri.

Dkt. Mpango amesema Serikali inahitaji fedha ili kukamilisha miradi ya kitaifa ikiwemo ujenzi na ukarabati wa meli, ujenzi wa SGR, ununuzi wa ndege 5 nk hivyo haitavumilia uzembe wowote unaopelekea upotevu wa mapato ya serikali kwenye matumizi.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Huyu utafikiri hakuwepo hii miaka 5, halmashauri zote zina wakurugenzi wana CCM, DC's, DAS's, RAS's na RC's wote hawa ni CCM lakini bado wana CCM wanalalamika. wapuuzi nyie.
 
Ndio maana akateuliwa tena ni waziri mwenye kuipa kipaumbele miradi ya serikali; lakini sio wa uchumi wa Tanzania.
 
Sasa hizo ndege tano za nini wakati hizi ambazo tunazo zinatutia hasira tu
Labda wewe na Amsterdam ndo mnahasira zaidi.
Jamaa limenuna pesa ya malipo ya uwakili sijui litapata wapi.
Bado linadhani linaweza kubahatisha hapa Tanzania.
 
Nyinyi si miaka mitano mizima mlikuwa mnaimba mapambio ya kusifu na kuabudu kuwa JPM kamaliza ufisadi? rushwa ? kaleta nidhamu kwa watumishi wa umma ? Leo mnasema Kuna nini ?bado serikalini ? Mapimbi huwa hamchelewi kusahau?
 
Back
Top Bottom