Waziri Dkt. Damas Ndumbaro awasilisha marekebisho ya Sheria Mwaka 2023 na Urekebu wa Sheria wa Mwaka 2023

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,901
944

WAZIRI DKT. DAMAS NDUMABRO AONGOZA TIMU YA WATALAAMU KUWASILISHA MAREKEBISHO YA SHERIA MBELE YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, ameongoza Timu ya Wataalamu wa Wizara ya Katiba na Shera, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wizara ya Malia Asili na Utalii, Shirika la Reli, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kuwasilisha Miswada ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2023 na Urekebu wa Sheria wa Mwaka 2023 Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria tarehe 26 Mei, 2023

Katika hatua nyingine, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro tarehe 25 Mei, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu wakiwakilishwa na Sheikh Ponda Issa Ponda na Sheikh Dkt. Ibrahim Ghulaam kutoka Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu ambapo wamepata wasaa wa kukutana na kuzungumza masuala mbalimbali yahusuyo maadili na mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Ndoa.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Mradi unaofahamika kwa jina la EU-AML-CFT-ESCAY unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya Bw. Frederic Bayard walipokutana Jijini Dodoma wakati wakishiriki Uzinduzi wa Mwongozo wa Uchunguzi na Upelelezi wa Makosa ya Ufadhili wa Ugaidi, Utakatishaji Fedha na Masuala ya Rushwa. Mwongozo huo umezinduliwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magerea, Jeshi la Uhamiaji, Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa, Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Jamhuri ya Kenya.

Vilevile, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Chama cha Wanasheria wa Serikali katika Ofisi za Wizara, Mji wa Serikali Mtumba ambapo pamoja na mambo mengine wamepata wasaa wa kukutana na Wakili wa Serikali Mkuu Bw. Lucas Malunde ambaye ni Makamu wa Rais wa Chama hicho na Bi. Sia Mrema, Wakili wa Serikali Mkuu na Katibu wa Chama.

Katika mazungumzo hayo wamepata wasaa wa kuzngumza kuhusu maendeleo ya Chama na Masuala mbali mbali yahusiyo sekta ya sheria nchini.

Kwa upande wa wataalamu wa Wizara wamewakilishwa na Bw. Abdulrahamanu Mshamu,Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kwa Umma.

FxEVXrDXwAwyrXl.jpg
FxEVZPGWYAEal_4.jpg
FxEVa7WXwAcHPJD.jpg
FxEVcN3XwAIISFU.jpg
 
Back
Top Bottom