Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, ametoa wito kwa Wanasiasa wote nchini kutoka vyama vyote vya siasa kuhakikisha wanalinda na kuheshimu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hasa wakati huu ambapo taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2025.
Dkt. Ndumbaro alitoa kauli hiyo wakati wa semina ya kampeni ya msaada wa kisheria iliyofanyika katika Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma. Semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo viongozi wa serikali wa ngazi ya mtaa pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ngazi ya kata, tawi na shina kuhusu masuala ya kisheria na uendeshaji wa haki kwa wananchi.
Akizungumza katika semina ambayo imefanyika siku ya jana Mei 12, 2025 Dkt. Ndumbaro alisisitiza kuwa ni wajibu wa kila mwanasiasa kuzingatia na kutekeleza matakwa ya Katiba ili kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika kwa amani, haki na kwa mujibu wa sheria. Aliongeza kuwa katiba ndiyo mwongozo wa maisha ya kisiasa na kiutawala nchini, hivyo ni lazima iheshimiwe na kulindwa na kila Mtanzania, hususan wanasiasa.
Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro alieleza kuwa serikali ya CCM itaendelea kuheshimu ukomo wa muda wa uongozi kama ulivyoainishwa kwenye Katiba, ambayo inaeleza kuwa serikali hukaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano tu. Hivyo, alisisitiza kuwa serikali ya sasa itaendelea kutekeleza majukumu yake hadi mwaka 2025 na haitakiuka Katiba kwa namna yoyote ile.
Kwa upande wao, baadhi ya viongozi wa serikali na wa CCM waliopata mafunzo hayo walisema semina hiyo imewapa maarifa muhimu kuhusu sheria na haki, jambo litakalowasaidia kuwahudumia wananchi kwa uadilifu na ufanisi zaidi. Wamemshukuru Waziri Ndumbaro kwa kupeleka elimu hiyo muhimu na kuahidi kuitumia kwa manufaa ya wananchi katika maeneo yao.