Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa


Nakubaliana na hoja zako ila kuna marekebisho kidogo na ninadhani umeteleza kwa bahati mbaya na unahitaji kuelimishwa. Mipaka yote haitawaliwi na ramani iliyochorwa bali inalindwa na mkataba uliopo hata kama ilikuwa ni ile tuliyoita bogus-treaties kama ule aliosaini Sultani kuuza kisiwa cha Mafia kwa kitambaa kinachoweza kuizunguka Mafia yote.
 

Kumbe muda wote unakomaa hapa Nikupateje unatafuta tuzo?
Kwanini sasa hujampelekea membe hizi latitudes sahihi bali umezileta JF!?
 
Last edited by a moderator:
Kumbe muda wote unakomaa hapa Nikupateje unatafuta tuzo?
Kwanini sasa hujampelekea membe hizi latitudes sahihi bali umezileta JF!?

Aliyekomaa nalo ni huyu Membe na sijui kwa nini amelichukua so public kiasi hiki. Hakuwa na sababu za kulipeleka Bungeni kiasi kile halafu unafika huko kwa sababu hukujiandaa majibu yenyewe yanakuwa paragraph mbili na hizi zenye makosa wakati huohuo kuna mazungmzo yanaendelea. Wenzake wote tangu Nyerere walijua kuwa hili si rahisi kiasi hiki na kulipa public interest kama linavyomtokea puani sasa.

Yeye angefanya diplomacy ya kimyakimya kama anavyofanya kimyakimya kwenye suala la OIC na husikii kelele zinamsakama.

Lakini hata leo Membe akitaka kulikoroga la OIC basi nalo alipe publicity kama alivyofanya hili la Malawi. Nadhani hili ilmempa a sounding class.
 

Sasa hapa ndio ume comment kwa busara yako yote. Ndio nini hiki umeandika?
Hili nimeliandikia mara nyingi sana hapa, kwa sasa ni marudio kwahiyo usikurupuke!
 
Mtoa mada nina wasiwasi kama wewe ni Mtanzania. Kwanza kwa kukariri Ziwa Malawi badala jina linalojulikana na Watanzania pamoja na jumuiya ya mataifa kama Ziwa Nyasa hii imenithibitishia kuwa wewe ni Mmalawi. Pole sana, ila kumiliki ziwa lililompakani kwa asilimia 100% ni kitu ambacho hakiwezekani. Kukubali umiliki wa Msumbiji na kukataa umiliki wa Tanzania ni jambo ambalo aliingii akilini.
 
Acha ujuha, hotuba si mkataba wala statement ya mahakamani. Subiri waweke documents vizuri ambazo zina details kama hujajikuta ulicho prtesent hapa ni cha mtoto.
 
Hivi unadhani haya uliyoeleza yanamsaidia Membe atakapokaa na wamalawi hapo August 20, 2012? Mbona kakaa nao majuzi lakini akienda hewani na mwenzake wa Malawi ni kama vile Membe anafundishwa geography and history?!

tatizo lako una hamisha goli ili ufunge, sasa hiyo inaonyesha udhaifu ulio kuwa nao, unaweza kuwa una akili, lakini bado hujakuwa na uwezo wa kuitumia vizuri, ndio maana sasa hadithi zako zimekwenda kwa Membe, badala ya kuongelea suala halisi, weeakness ya membe or whoever, ni weakness ya huyo mtu na sio weakness ya Taifa au ya facts, pili unatakiwa kuelewa katika kujibu swali, msahihishaji haangali hadthi yako ndefu? bali anaangalia key points, sasa mimi ninapo kusoma si angali maelezo yako marefu ambayo baadae yanapotea muelekeo, eg issue ya lattitudes or longitudes etc , ni error ndogo ambayo haiwezi kuharibu jambo kuu? nalo ni la mpaka upo wapi? at the shore of the lake or in the middle of the lake, hivi vingine unavyo ongelea ni sawa na kuweka kachumbari au kutokuwa na kachumbari
 
Wewe Mmalawi usitake kutufanya sisi wabongo hatujuwi haya mambo, kukufahamisha ziwa Nyasa kwa juu liko latitude ya 9 degree na dakika 40 kwa longitude ya 34 degree na dakika 15 (kwenye ramani ya QDS 273/2) ambayo inaitwa Lupila.

Kusini ziwa liko kwenye longitude ya 34 degree na dakika 40 ambalo ni eneo la Lundu kwa wenyeji wa huko watakuwa wanapafaham na latitude yake ni 10 degree na dakika 45 (QDS 297-1 Lituhi).

Naomba nikukumbushe kitu kimoja unapotaja hizi point huwezi kutaja latitude pake yake bila kutaja longitude yake na kwa UTM Ssystem huwezi kutaje X- cordinate bila Y - cordinate na ARC1960 kwa WGS84 ni conversion tu ndugu yangu 300m kwa X na 200m kwa Y.
 

Asante kwa ufafanuzi mkuu!

Huyo mmalawi wakuogopwa!
 
We gamba chama hapa tunazungumzia masuala ya kitaifa. Hizo siasa zako za mataputapu ya mabwepande ziache huko huko lumumba.

Mkuu Mwita,
Tasi hana gamba; mimi ni mzalendo halisi niashi kwa kipato halali sitegemei ajira kutoka serikali ya JMT; CCM wala sifanyi biashara na vyombo hivyo, mimi ni clean ila nina wasiwasi sana na watu wa kaliba yako wanaopiga kelele gamba la kobe ilhali wao wenyewe wamevaa magamba ya kasa; hapa nilimpongeza Yericko Nyerere kwa kuongea ukweli na kuonyesha uzalendo na utaifa, pitia posti za vijana wako wa Chadema kina matola, precise pangolin na wengine tu; badala ya kuwakemea vijana wako umekimbilia kunishutumu, mimi nilipitia JKT najua nini maana ya utaifa na unazi wa kichama, kwangu taifa mbele period!!! I trust you don`t be simple just because you want to side with some stupid and simple minded makamanda

Chama
Gongo la mboto DSM
 
MIMI NATATIZIKA SANA NA SUALA LA MIPAKA YA NCHI! kwakweli mimi sijawahi kufika mipakani, kwani hakuna visible thing to show the national boundary??

Maana tangu miaka yooote hii Mkapa,- Mwinyi hakuna mgogoro malawi, Tz wote wapo ok, isipokuwa vipindi hivi viwili Nyerere ambaye nilidhani alisolve.

kiramani kwakweli mimi naona ziwa tunalo watz
 

Mkuu hebu tujikite kwenye hii mada kijografia zaidi ili tufikie lengo, tuweke mengine pembeni kwa nia ya kufikia lengo kwa logic and reasoning.
Samahani kama sijakufurahisha kaka.
 

Ujuha wa wamalawi na wanaowaunga mkono umelala kwenye imani ya kile wakiitacho makubaliano ya wajerumani na waingereza,wala si makubaliano wenyeji wa mwambao wa ziwa hilo,hata kama akili yako haijakomaa ni mahakama ya nguruwe pekee inayoweza toa haki kwa Malawi kumiliki ziwa lote wakati hilo ziwa linagusa ardhi ya nchi nyingine inayokaliwa na watu ambao wanayo haki ya asili kutumia maji ya ziwa hilo. Iwe Membe kakosea malatitude na malongitude au kapatia ukweli unabaki kama ulivyo kuwa ziwa ni mali ya wale wanaoapakana nalo nusu kwa nusu.
 
Nimeisoma Heligoland Treaty neno kwa neno na nimerudia mara kadhaa. Na kila nikiisoma sioni tutachomokea wapi kuhusu hili la Malawi.
Temporary treaty aimed at resolving the boundaries between British sphere of influence and German sphere of influence.
Only lake victoria was marched upon the delimiting line between them.
The rest of interterritorial waters were not, simply because there were no lands (habitable) between Tanganyika and Nyasaland.
The Lake was being treated by both as international waters. There were German and British gunboats sailing freely in those waters prior to 1914.... why do you think Britain allowed German vessels in their waters? Or vice versa?
 
ni vita za 2015 ndani ya ccm mkuu... kitu gani huoni hapo??? yani unaona mkia halafu bado unauliza mku**du wa mbwa uko wapi??? nyanyua mkia utaona tundu
 
asante kwa masahihisho, hilo ziwa unataka kuniambia kuwa kabla ya kuja kwa wakoloni lilikuwa linatumika na upande mmoja tu yaani malawi?? halafu mbaya zaidi watershed ipo upande wetu yaani milima inayotiririsha maji ipo kwetu kwa nn tunyimwe haki ya kulitumia kisa wakoloni??
 
Mnyasa wa Maravi huyu ...:hat:
mimi naona hapa kuna hoja, hebu tuchangie badala ya kuhukumu mleta hoja kama mnyasa wa malawi au wa TZ! Kesho akichangia mmakonde utasema nae ni wa msumbiji?
natoa rai kwa wataalamu wa sheria za mikataba ya kimataifa mliomo humu jamvini mtusaidie kujibu swali hili: Je shauri hili likipelekwa mbele ya mizani ya umoja wa mataifa kuna hoja itakayotusaidia wa TZ kushinda kesi hii?
maana kama JK( rais) kadanganywa mara nyingi tu na wasaidizi wake kwa nini membe nae asipotoshwe na wasaidizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…