Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Nimeamua kuiweka hii kwenye separate thread kwa sababu nimeona ina extra concept kulingana na ile ya jana.

Wakati nanunua gazeti nilitumaini kabisa Membe atakuwa na hoja ya ku-convice kwani humu JF mnaongea tu kama mimi. Kwa wale waliosoma RAIA MWEMA wafungua attached paper kwenye ukurasa wa iv. Ndipo anaeleza msimamo wa Serikali kuhusu mpaka wa Ziwa Malawi.

Nakiri kwamba hata wakati naleta thread ile ya kwanza, nilitumaini Bernard Membe atakuwa ameongelea findings ambazo zingetushawishi na mimi nisingesita kuungana kwenye nia ya kukidhi madai haya ya Lake Malawi.

Lakini baada ya kusoma speech ya Membe basi matumaini yote ya kulipata Lake Malawi yamenitoka. Narudia sipingi Tanzania kupata sehemu ndogo ya Lake Malawi kama baadhi mnavyoropoka. Na hata mnavyoropoa wengine hainipi matumani ya kulipata hilo Ziwa. Lakini aliyenisikitisha zaidi ni Waziri Membe na sasa kwangu ni dhahiri kwamba tusahau kabisa kulipata Ziwa hili.

Siku moja nilifanya hesabu ubaoni nikapata jibu na baadaye nikaongeza madoido mwalimu akanikata maksi akasema "Kujitawaza kwingi mwisho unashika kinyesi". Naona ndugu yetu Waziri Membe kaingia katika mtego huu. Kwa nini nasema hivi? Ninanukuu majibu yake kama ifuatavyo:


****
Mheshimiwa Spika,
Lipo tatizo la muda mrefu kati yetu na nchi jirani ya Malawi linalohusiana na mpaka kwenye Ziwa Nyasa. Tatizo lenyewe ni kwamba Malawi wanadai kwamba ziwa lote kaskazini ya Msumbiji kuelekea Ruvuma na Mbeya ni mali yao kwa mujibu wa Mkataba wa Heligoland uliowekwa mwaka 1890.

Mheshimiwa Spika,
Tanzania kwa upande wetu tunasema kuw ampaka wa kweli kati yetu na malawi unapita katikati ya ziwa hivyo kufanya
eneo lote la Kaskazini Mashariki ya Ziwa kati Latitude digrii 9 na digrii 11 kuwa mali ya Tanzania kwa mujibu wa mkata huouo wa Heligoland wa mwaka 1890 ambao ulikubali kuwa kwa vile kuna maeneo ya mpaka ambayo hayana mantiki, pande zinazohusiana zikutane na kurekebisha. Aidha tunazo ramani ambazo waingereza wenyewe walipitisha mpaka katikati kama ulivyo mpaka kati ya Msumbiji na Malawi.
****

Nimemalizia hapa kwa sababu mengine yanayofuata ni diplomatic process. Sasa hapa tuchambue hotuba hii ya Membe. Binafsi nimeusoma mkataba wote wa Heligoland na wala si alichokisema Membe. Kama membe anataka kuikomboa Tanzania walau tupate sehemu ya Ziwa basi washauri wake wamempotosha kutumia mkataba ule ambao hautetei hoja yake hata kidogo.

Lakini pia Membe ni mmoja wa wanaodhani watanzania wa sasa hawajui kufukua mambo na ndiyo maana kwenye thread yangu nimesema tutumie usomi wetu. Membe ametaja kwamba sehemu ya ziwa kati ya Latitude digrii 9 na digrii 11 ni mali ya Tanzania.

Hapa ndipo Membe ameumbuka umbuko ambalo hatalisahau. Kwa nini nasema kaumbuka. Kaumbuka kwa sababu geography ya Tanzania wote tunaijua. Ncha ya juu kabisa ya Lake Malawi iko kwenye coordinate { S9.49214 E34.03563} ambapo ni only 7.0km kutoka kijiji kiitwcho Matema kilichopo kwenye coordinate { S9.49601 E33.97215}.

Ukiangalia coordinate hizi maana yake ni kwamba Ziwa Malawi linaishia kwenye Latitude 9.49214. Sasa hapa Membe anasema eti ni kuanzia Latitude 9. Kwa maana hii ya Membe kama Ziwa ni letu kuanzia latitude 9 maana yake ni kwambaMmembe kafanya makosa kwa kulirefusha ziwa hili kwa umbali wa 54.4km kuelekea kaskazini!

Watu mnaotoka kusini hasa Mbeya mnafahamu sehemu iitwayo Matamba. Hapa coordinate zake ni { S9.01171 E34.09959}. Kwa mujibu wa Membe, hii Matamba ingekuwa imeguswa na Ziwa hili!

Hakika waliomletea Membe hizi data wamemvuruga kuliko kulietengeneza suala hili. Ziwa Malawi au Nyasa linaishia kwenye Latitude 9.49214 kama nilivyosema hapo juu. Hapa membe kadanganya Bunge na kadanganya watanzania kasi kwamba sijui sasa ni nani mwenye nguvu ya kulitetea hili.

Tuje sasa kwa upade wa kusini yaani unaotambuliwa na membe kama sehemu yaetu ya Ziwa. Membe anasema sisi mali yetu ni mpaka kwenye latitude 11. Sijui wangapi mmeona kosa hili la mwaka. Unaposema kwamba unaishia hapa kwenye Latitude 11, je mnaotetea hoja hii mnaelewa madhara yake? Kama hamyajui basi mimi nayasema hapa.

Kama Membe kasema Bungeni kwamba tunaishia kwenye Latitude 11 basi maana yake pale ni kaskazini ya sehemu iitwayo Liuli ambayo iko { S11.05023 E34.63908}. Kumbe, Mwanakijiji wa Liuli haruhusiwi kuvua samaki kwenye ziwa lile kwa sababu ni sehemu ya Malawi, kwa mujibu wa Waziri Bernard Membe!

Yaani mwanakijiji huyu wa Liuli, anakuwa amekiuka mpaka kwa kilomita 6.6 kwa mujibu wa Serikali anayoshiriki membe wala si kwa mujibu wa Serikali ya Malawi!

Nimeanza na mfano huo wa Liuli ambao najua wengine hampaju ahapo. Sasa tuje kwenye mfano ambao wengi mnaujua na mmeutumia kunipinga humu na kuniita mimi ni mmalawi.

Mfano wenyewe ni wa Mbamba Bay. Ndiyo maana nimesema kajipangeni hii kesi tutajikuta tunasambaratika tukidhani tunatetea huku tunajiangamiza. Narudia kusema kwa mujibu wa hotuba ya Waziri Membe ni kwamba umiliki wetu wa Ziwa hili unaishia kwenye latitude 11. Mbamba Bay iko kwenye coordinate { S11.30519 E34.80449}.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Mbamba Bay haiko katika eneo linalotambuliwa na Waziri Membe kwa latitude degree 0.30519!

Uki-convert hizi latitude kwenda kwenye kilomita basi maana yake Membe haitambui Mbamba Bay kwani iko 33.7km nje ya eneo ambalo Tanzania tunamiliki ziwa!

Waziri membe pia inaelekea kuwa hajui mpaka unavyopita pale Msumbiji. yeye anasema kule ni nunu kwa nusu lakini wote fungueni ramani muone kama hilo nalo lina ukweli. Mpaka wa Msumbiji ni nusu kwa nusu kuanzia kwenye latitude 11 had 13 lakini kuanzia hapo kueleka kule chini kusini ziwa lote liko sehemu ya Malawi na linaishia kwenye coordinate {S14.44635 E35.23539} ambako ni latitude 14.44635.

Hivyo, tujenge hoja zinazojikita kwenye ukweli na tusishabikie mambo kama vile Simba na Yanga. Hapa hatufanyi ushabiki. Hapa tunasaidia kujenga na kupima hoja kama kweli tunaweza kuisaidia nchi yetu kupata sehemu ya ziwa hili.

Ninasubiri kwa hamu kuona mtakuja na hoja gani kuhusu hizi findings zinazochambua hotuba ya Membe na matokeo yake niliyoeleza humu.
 
sasa tuingie kwenye google MAPS kisha tuweke hizo coordinates then tuonyeshe Membe katoa wapi na nani mkweli
 
all in all ziwa nyasa lipo mpakani hatuwezi kunyimwa kulitumia sababu ya mikataba ya wakoloni mpaka utakuwa katikati ta ziwa hawataki tutawatwanga na kulichukua lote kabisa!
 
Serikali yetu inasikitisha sana. Wakati wenzetu wakitumia mikataba kama ushahidi, serikali yetu inatumia ramani!!!
Ramani iliyochorwa na Mwingereza???!!!. Kama mwingereza alikuwa na interest zake binafsi kuchora ramani hizo??!!
Serikali yetu inapaswa kutafuta strong evidences kwamba Ziwa Nyasa ni letu.
 
Kwani kabla ya wakoloni kutugawa, hao watu waliopo kando ya ziwa upande wa TZ hawakuwepo?? Bilashaka kama walikuwepo basi walikuwa wakitumia hilo ziwa kwa uvuvi na matumizi mengine. Basi Kama wanataka ziwa lote, waingie ndani zaidi ya mpaka ili wasiwaathiri waliokuwa wakilitumia ziwa hilo tangu enzi. Haya mambo ya mikataba waliyofanyia huko Berlin haliwezi kuwatendea haki watu wanaoishi kando ya ziwa. Ndiyo maana ilikuja kukubalika kuwa sehemu ya mpaka wenye ziwa, basi mpaka uwe katikati. Na kwa ziwa kama Victoria, nchi zote tatu zilizolizunguka zinaumiliki katika ziwa hili.
 
wamalawi wanaita lake malawi (nyasa kwao ni tusi k**a)

watanzania tunaita lake nyasa

Mytake : Hivi tunagombea ziwa lipi?
 
Nikupateje kwanza niseme tu kwamba sihitaji kukupata kama jina lako lilivyo.
Pili nikuulize unachohangaikia ni kitu gani? Ile thread yako nyingine ulipewa hoja za kutosha kukujibu hoja zako. Sasa umekuja kuanzisha nyingine yenye hoja zile zile.
Hii bidii unayofanya kujaribu kuhadaa watu na vilatitudes hapa wala haikusaidii wewe mnyasa na makuwadi wenzako wa kinyasa mliojazana hapa nchini.
Malawi hawawezi kumiliki ziwa lote, watake wasitake lazima kuna kipande chetu ndani ya ziwa nyasa.
 
Last edited by a moderator:
Nikupateje kwanza niseme tu kwamba sihitaji kukupata kama jina lako lilivyo.
Pili nikuulize unachohangaikia ni kitu gani? Ile thread yako nyingine ulipewa hoja za kutosha kukujibu hoja zako. Sasa umekuja kuanzisha nyingine yenye hoja zile zile.
Hii bidii unayofanya kujaribu kuhadaa watu na vilatitudes hapa wala haikusaidii wewe mnyasa na makuwadi wenzako wa kinyasa mliojazana hapa nchini.
Malawi hawawezi kumiliki ziwa lote, watake wasitake lazima kuna kipande chetu ndani ya ziwa nyasa.

Kama yale ndiyo yalikuwa majibu na unadhani ni yanajibu basi ni kwa kiwango chako na wenye uelewa wa aina yako ambao mkipewa evidence mnakimbilia kusema vi-latitude wakati ndivyo baba yako akvipeleka kule bungeni.

Lengo langu ni wote tuone kwamba hoja zinazojengwa juu ya hili ni hoja za kitoto ambazo hazisaidi kuifaidisha Tanzania chochote na tangu kule nilisema ni danganya toto ku-deviate masuala ya msingi kama ya Ulimboka, SSRA, Ufsadi nk.
 
Nikupateje kwanza niseme tu kwamba sihitaji kukupata kama jina lako lilivyo.
Pili nikuulize unachohangaikia ni kitu gani? Ile thread yako nyingine ulipewa hoja za kutosha kukujibu hoja zako. Sasa umekuja kuanzisha nyingine yenye hoja zile zile.
Hii bidii unayofanya kujaribu kuhadaa watu na vilatitudes hapa wala haikusaidii wewe mnyasa na makuwadi wenzako wa kinyasa mliojazana hapa nchini.
Malawi hawawezi kumiliki ziwa lote, watake wasitake lazima kuna kipande chetu ndani ya ziwa nyasa.

jaribu kumuelewa na si kwamba mtu akijan na hoja then mnaanza kusema yeye ni mnyasa sijui mmalawi...hii thread imejikita zaidi kwenye hotuba ya membe...je membe yuko sahihi?? maana na yeye ametaja vi latitude...na kingine tusikimbilie kusema malawi hawawezi kumiliki ziwa lote hilo..sasa kama point zenu ni dhaifu kama za mebe ka nini wasimiliki?...tujikite kwenye hoja na kama tunaijua jiografi vizuri tulete ushahidi na sio kukimbilia kusema..wewe mmalawi
 
Mimi nafikiri juna ujuha usio na sababu. Waziri ameeleza hatua zinazochukuliwa na contention ya Tanzania kuhusiana na suala hilo. Malawi nao wana contention yao lakini sisi tunachosema i kwamba nusu ya hilo ziwa ni mali yetu na ni vizuri Malawi wakaelewa hivyo. Sasa issue ya kutafsiri latitudes or longitudes ni suala la kufahamu zimekaaje and it is a subject for another day. Lakini kwa kuzingatia kwamba Waziri ametoa onyo na kuyataka makampuni yanayofanya utafiti wa mafuat kuacha mara moja ni pointer kwamba tuna claims kama serikali.

Kilicho wazi hapa ni kujaribu kujenga hoja ambayo itaonyesha kama vile waziri na serikali ni dhaifu katika hili. Huo ni upuuzi kwa sababu juhudi za serikali msimamo wake katika hili vinafahamika. Hizi hila zenye jicho la kisiasa haziwezi kubadilisha kitu. Suala la ziwa Nyasa litatatuliwa na serikali na siyo mwenyekiti wa kamati yoyote (anayejigeuza kuwa Executive) au na bunge au wapiga kelele na wakosoaji wasio na hoja.
 
sasa tuingie kwenye google MAPS kisha tuweke hizo coordinates then tuonyeshe Membe katoa wapi na nani mkweli

Mkuu BORGIAS,

Nikusadie kidogo. Googlemaps inaweza isiwe accurate sana ingawa haya yote ninayosema unaweza kuyathibitisha huko. Kumbuka ramani hizi ziliwekwa miaka ya 1800 ambapo computer hazijagunduliwa.

Data alizotakiwa atumie Membe ni zile ambazo wataalamu wengi hapa nchini hutumia kwenye map reading. Pale Wizara ya ardhi zipo kibao kwa kila mkoa. Ni accurate sana.

Map reading ya mwisho hapa tanzania ilifanyia mwaka 1960 kwa kutumia Geodemic system iitwayo ARC1960. Ukienda kwenye googlemap wanatumia system ya mwaka 1984 iitwayo WGS84.

Hivyo, unapaswa kulizingatia hili.
 
Serikali yetu inasikitisha sana. Wakati wenzetu wakitumia mikataba kama ushahidi, serikali yetu inatumia ramani!!!
Ramani iliyochorwa na Mwingereza???!!!. Kama mwingereza alikuwa na interest zake binafsi kuchora ramani hizo??!!
Serikali yetu inapaswa kutafuta strong evidences kwamba Ziwa Nyasa ni letu.

Hebu waelez maana hata mimi nimesahau kukitaja unachokitaja. Kwamba baada ya Wordl Wara the first kwamba kuna ramani zilionyesha hivyo, na Waziri anatamka hivyo Bungeni na anapata washangiliaji huko Bungeni na huku mitandaoni. Ni uvivu wa kusoma na kutafiti kiasi kwamba inatia aibu.
 
OSOKONI miaka ya 70 inamaanisha kati ya mwaka 1970 na 1980 siyo 1979! right?
By the way nafurahi kujua kuwa huyu@Nikupatejew ni Mnyasa na ndiyo maana anatokwa mishipa ya shingo kutetea Malawi kwamba inamiliki ziwa Nyasa kwa 100%!
Basi nazipuuza threads zake tangu sasa!
 
Last edited by a moderator:
Mimi nafikiri juna ujuha usio na sababu. Waziri ameeleza hatua zinazochukuliwa na contention ya Tanzania kuhusiana na suala hilo. Malawi nao wana contention yao lakini sisi tunachosema i kwamba nusu ya hilo ziwa ni mali yetu na ni vizuri Malawi wakaelewa hivyo. Sasa issue ya kutafsiri latitudes or longitudes ni suala la kufahamu zimekaaje and it is a subject for another day. Lakini kwa kuzingatia kwamba Waziri ametoa onyo na kuyataka makampuni yanayofanya utafiti wa mafuat kuacha mara moja ni pointer kwamba tuna claims kama serikali.

Mkubwa,

Nimesoma hotuba yote ya Membe mle Bungeni. Sijui kama wewe umeisoma. Sijaeleza mengine kwa sababu context ya thread hii ni kuonyesha jinsi Tanzania ni kama tumekurupushwa kulitetea jambo hili.

Tuje kwenye suala la Malawi kukatazwa kufanya utafiti. Usipoisoma vizuri ile context unaweza kuamini kwamba wamekatazwa. Lakini ukisoma hotuba ya Membe anasema kwamba kuna ndege za utafiti zilikuja zikatua January na February kwenye east coast of Lake Malawi.

Kama ndivyo ilivyo basi hapo ni kweli wanastahili kukatazwa maana ndege inatua nje ya mpaka ambao ni shoreline. Lakini kwa sababu waziri anajua huwa hatusomi na tunakurupuka, anajua kwamba hatutajiuliza hivyo.

Hivyo, kilichokatazwa na Malawi walichokubali ni kitendo cha ndege zao kutotoa kwenye eneokama Mbamba Bay.

Lakini Serikali suala la kwamba wasitumie ile nusu ya maji kuelekea kwetu membe anasema waliwashawishi wamalawi mkutanoni wasiitumie pia. Hapa Membe anasema inaelekea wenzetu walituelewa.

Sasa utasemaje kuwa inaelekea walituelewa kana kwamba mliwatumia barua na mnategemea baada ya kuisoma wanaweza kuwaelewa. Si hivyo. Walitoa rai hiyo mkutanoni na Membe alitakiwa kutuambia jibu la Wamalawi mle mkutanoni, je walikubali au walikataa.

Kulinagana na magazeti ya Malawi hata ya leo (NyasaTimes) wamesema hakuna cha kuwakataza kufanya research kwenye maji yao.

Hebu tafakari hapa. kwa nini membe hasemi resolution ya hizo meetings walizofikia na anaishi kuzitaja tarehe zake tu.

Sasa kama tulipitwa na sisi, binafsi nimeweka kwenye kalenda yangu kwamba kuna meeting nyingine siku 12 zijazo yaani August 20, 2012 itafanyikia mji uitwao Mzuzu huko Malawi. Tuwe watchfully tujue ni nini kiliendelea huko.
 
Most unfortunate, Maranya. Tumia hoja za kweli na sio kwamba wewe ni Mnyasa nk. Hii inaitwa ad hominem argument. Yaani badala ya kutoa hoja unamshambulia mtu binafsi. Hapo unaoneka umefilisika kihoja.
Baada ya kusema hayo, niseme kwamba. Tumerithi mipaka ya kikoloni. Mataifa ya kiAfrika yalikubaliana awali kwamba iwapo kila mmoja ataamua kwamba haipendi mipaka hii na kuchora ramani upya, basi kutakuwa na vita visivyokwisha. Mikataba ya kikoloni iliweka mpaka kwenye ufuko wa mashariki wa Ziwa Nyasa. Tutake tusitake ilikuwa hivyo.
Kinachotakiwa sasa ni diplomasia ili dunia nzima ituelewe. Na kuna precedent za migogoro kama hii duniani. Hoja ya msingi kwangu ni kwamba baada ya miaka 50 ya uhuru nchi za kiafrika hazitakiwi kuwa watumwa wa ramani na mikataba ya kikoloni kwa kiasi cha kukataa common sense.
Kwangu ni common sense kwamba watu wameishi ziwani, na ziwa ni maisha yao kwa karne na karne. Sasa mkoloni anakuja na kuweka mipaka na kumwambia jirani yetu, "ziwa lote hilo lako. Yule asikubabaishe, hana lake hapa." Sisi tunatakiwa ku-appeal kwa common sense ya jirani yetu ili tufikie makubaliano kidiplomasia.
Sikubaliani na ubabe unaoelezwa kwamba "watake wasitake, tutawaonyesha tulichomwonyesha Idi Amin." Vita si jambo la kushabikia hata kama una nguvu. Ni matatizo yasiyomithilika. Niite unavyoona. Ndugu zangu wanaovua samaki pale Mbamba Bay watapigwa mabomu, hata kama tutashinda vita. Ni wazo linalonitisha sana.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom