Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa

OSOKONI miaka ya 70 inamaanisha kati ya mwaka 1970 na 1980 siyo 1979! right?
By the way nafurahi kujua kuwa huyu@Nikupatejew ni Mnyasa na ndiyo maana anatokwa mishipa ya shingo kutetea Malawi kwamba inamiliki ziwa Nyasa kwa 100%!
Basi nazipuuza threads zake tangu sasa!

Wewe hiyo ya kuwambiwa kwamba ni Mnyasa ndiyo umeiona hoja. Really? Baada ya kusoma hoja yake na kusoma historia (au kutosoma labda) ndiyo umeona kwamba hiyo ndiyo hoja. Unbelievable! Read a book!
 
Most unfortunate, Maranya. Tumia hoja za kweli na sio kwamba wewe ni Mnyasa nk. Hii inaitwa ad hominem argument. Yaani badala ya kutoa hoja unamshambulia mtu binafsi. Hapo unaoneka umefilisika kihoja.
Baada ya kusema hayo, niseme kwamba. Tumerithi mipaka ya kikoloni. Mataifa ya kiAfrika yalikubaliana awali kwamba iwapo kila mmoja ataamua kwamba haipendi mipaka hii na kuchora ramani upya, basi kutakuwa na vita visivyokwisha. Mikataba ya kikoloni iliweka mpaka kwenye ufuko wa mashariki wa Ziwa Nyasa. Tutake tusitake ilikuwa hivyo.

Kinachotakiwa sasa ni diplomasia ili dunia nzima ituelewe. Na kuna precedent za migogoro kama hii duniani. Hoja ya msingi kwangu ni kwamba baada ya miaka 50 ya uhuru nchi za kiafrika hazitakiwi kuwa watumwa wa ramani na mikataba ya kikoloni kwa kiasi cha kukataa common sense.
Kwangu ni common sense kwamba watu wameishi ziwani, na ziwa ni maisha yao kwa karne na karne. Sasa mkoloni anakuja na kuweka mipaka na kumwambia jirani yetu, "ziwa lote hilo lako. Yule asikubabaishe, hana lake hapa." Sisi tunatakiwa ku-appeal kwa common sense ya jirani yetu ili tufikie makubaliano kidiplomasia.
Sikubaliani na ubabe unaoelezwa kwamba "watake wasitake, tutawaonyesha tulichomwonyesha Idi Amin." Vita si jambo la kushabikia hata kama una nguvu. Ni matatizo yasiyomithilika. Niite unavyoona. Ndugu zangu wanaovua samaki pale Mbamba Bay watapigwa mabomu, hata kama tutashinda vita. Ni wazo linalonitisha sana.

Mkuu,

Ninakubaliana na baadhi ya mawazo yako. Kama umesoma thread yangu ya jana kuna mahala nilisema kwamba Ulaya walikuwa na magomvi kama haya enzi za kina Napoleon na kwa kweli Ulaya ilikuwa haikaliki kwani kila mtu kule ni mbabe.

Ndipo Ulaya walipoamua kuitisha kikao cha mataifa yote ya Ulaya pale Vienna, Austria ya sasa kwenye mkutano waliouita Congress of Vienna-1815 ndipo wakajadili mipaka.

Hili ilikuwa lifanyike hapa Africa mwaka 1963 lakini marais wote Africa wakiemo Nyerere na Banda wakakubaliana kwamba mipaka waliyorithi kwa mikataba ya wakolini ibaki hivyohivyo. Kumbuka ni mipaka yenye mikataba na si ramani wanazodai kuwa tunazo zinaonyesha hiki au kile.

Hivyo, pamoja na kuwalaumu wakoloni na sisi tujilaumu tulichokifanya mwaka 1963 na ambacho hata Nyerere alikifanya kw akumpiga Id Amini kwa kuvunja OAU Charter kumega mpaka uliokubaliwa mwaka 1963 wakati Obote ni Prime Minister wa Uganda na Rais wa Uganda akiwa Kabaka.
 
jaribu kumuelewa na si kwamba mtu akijan na hoja then mnaanza kusema yeye ni mnyasa sijui mmalawi...hii thread imejikita zaidi kwenye hotuba ya membe...je membe yuko sahihi?? maana na yeye ametaja vi latitude...na kingine tusikimbilie kusema malawi hawawezi kumiliki ziwa lote hilo..sasa kama point zenu ni dhaifu kama za mebe ka nini wasimiliki?...tujikite kwenye hoja na kama tunaijua jiografi vizuri tulete ushahidi na sio kukimbilia kusema..wewe mmalawi



Watanzania ni wavivu sana wa kufiri na wepesi wa kutoa majibu yasiyo na tija. Umesahau Jk alijibu waandishi kwenye pre-conference ughaibuni kuwa hajui kwanini Tanzania ni masikini? Na juzi kasema akipata B.$ kwa mwezi ataifanya tz kuwa heaven? Sintashangaa kesho akisema anatamani baada baada ya kikomo chake cha urais anatamani riz awe mfalme wa tz.

Nasubiri na waganda waidai bukoba, wakenya nao waidai kaskazini Yao Aluta continue
 
Haya ndiyo makosa mengi yanayo waongoza vijana wetu, hizo coordinate unazotumia fanya utafiti ili ujiridhishe maana zimewekwa kati ya mwaka 1984-2000 na ndizo zinazotumiwa na Google katika ramani zake,

Google wameleta matatizo makubwa kila pembe ya dunia kwa ramani zake kupotosha mipaka halisi ya kikoloni!

Narudia tena mpaka halisi unaotambuliwa na Tanzania ni KATIKA ya Ziwa Nyasa kwa mujibu wa ARC1960.

NB:

Kuweni makini sana ndugu zangu kuna mamluki ndani ya nchi yetu walioanza siku nyingi kuuza siri, na mmoja ni huyu mwanzisha uzi huu wanajaribu kuwagawa na kupotosha umma juu ya ukweli halisi!

Mipaka mingi barani Afrika iliwekwa miaka ya 1800 na wakoloni! Hakukuwa na teknolojia za kisasa kama unavyopotosha umma hapa na ***** wako hapa!
 
Haya ndiyo makosa mengi yanayo waongoza vijana wetu, hizo coordinate unazotumia fanya utafiti ili ujiridhishe maana zimewekwa kati ya mwaka 1984-2000 na ndizo zinazotumiwa na Google katika ramani zake,

Google wameleta matatizo makubwa kila pembe ya dunia kwa ramani zake kupotosha mipaka halisi ya kikoloni!

Narudia tena mpaka halisi unaotambuliwa na Tanzania ni KATIKA ya Ziwa Nyasa kwa mujibu wa ARC1960.

NB:

Kuweni makini sana ndugu zangu kuna mamluki ndani ya nchi yetu walioanza siku nyingi kuuza siri, na mmoja ni huyu mwanzisha uzi huu wanajaribu kuwagawa na kupotosha umma juu ya ukweli halisi!

Mipaka mingi barani Afrika iliwekwa miaka ya 1800 na wakoloni! Hakukuwa na teknolojia za kisasa kama unavyopotosha umma hapa na ***** wako hapa!

Angalau leo umesema maneno yenye hekima; wafundishe vijana wa Chadema wengi ni watapika pumba hawana wanachojua

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Nikupateje ungemaliza hii mada kwani hata mm nimeshaielewa na Mods ntawaomba waunganishe hizi mada kwani membe yupa sahihi kabisa na naomba mfuatilie link za August kwa mm nisiyesoma hapo nimekubali
user-offline.png
August

icon1.png
Re: Heligoland-Zanzibar Treaty:The basis For Malawi Claims
report ya usa ya 1964 kuhusu hilo suala
http://www.law.fsu.edu/library/collection/limitsinseas/ibs037.pdf\



IV. BOUNDARY ALIGNMENT
The alignment of the boundary will be discussed in two parts in accordance with the
treaties establishing them: 1) Lake Nyasa and 2) between Lake Nyasa and the Zambia
tripoint.
In accordance with the terms of Article I of the Anglo - German agreement of 1890, the
boundary from the Mozambique tripoint on the eastern shore of Lake Nyasa strikes
northward and follows the eastern, northern, and western shores of the lake.11
The Anglo - German agreement of 190112 affords the alignment of the boundary between
Lake Nyasa and the Zambia tripoint as indicated in Section 1. "It begins at the mouth of
the Songwe River at Lake Nyasa and follows this river upwards to its junction with the
Katendo (Katende) Stream in the Shitete district; it then follows the Katendo upwards to its
intersection with longitude 33, east of Greenwich, ascertained by the Commission, which is
marked on both sides of the Katendo by a boundary pillar (1); it then runs in a straight line
at an azimuth of 230º (from true north) to the top of Nakungulu (Nkungulu) Hill (2), which is
on the water parting of the geographical Congo Basin.

V. PRESENT SITUATION
There are no known disputes about the boundary at the present time. Future economic
activity in the area might require that additional attention be given the boundary because of
problems that may arise over water rights and transportation needs. Likewise, a detailed
delimitation of the shore boundary of Lake Nyasa might be necessary because of the large
fluctuations of the water level of the lake.

Hebu wataalam wa Geograph tusaidieni
 

Attachments

  • ziwa nyasa_thumb[1].jpg
    ziwa nyasa_thumb[1].jpg
    29.2 KB · Views: 49
Nimeamua kuiweka hii kwenye separate thread kwa sababu nimeona ina extra concept kulingana na ile ya jana.

Wakati nanunua gazeti nilitumaini kabisa Membe atakuwa na hoja ya ku-convice kwani humu JF mnaongea tu kama mimi. Kwa wale waliosoma RAIA MWEMA wafungua attached paper kwenye ukurasa wa iv. Ndipo anaeleza msimamo wa Serikali kuhusu mpaka wa Ziwa Malawi.

Nakiri kwamba hata wakati naleta thread ile ya kwanza, nilitumaini Bernard Membe atakuwa ameongelea findings ambazo zingetushawishi na mimi nisingesita kuungana kwenye nia ya kukidhi madai haya ya Lake Malawi.

Lakini baada ya kusoma speech ya Membe basi matumaini yote ya kulipata Lake Malawi yamenitoka. Narudia sipingi Tanzania kupata sehemu ndogo ya Lake Malawi kama baadhi mnavyoropoka. Na hata mnavyoropoa wengine hainipi matumani ya kulipata hilo Ziwa. Lakini aliyenisikitisha zaidi ni Waziri Membe na sasa kwangu ni dhahiri kwamba tusahau kabisa kulipata Ziwa hili.

Siku moja nilifanya hesabu ubaoni nikapata jibu na baadaye nikaongeza madoido mwalimu akanikata maksi akasema "Kujitawaza kwingi mwisho unashika kinyesi". Naona ndugu yetu Waziri Membe kaingia katika mtego huu. Kwa nini nasema hivi? Ninanukuu majibu yake kama ifuatavyo:


****
Mheshimiwa Spika,
Lipo tatizo la muda mrefu kati yetu na nchi jirani ya Malawi linalohusiana na mpaka kwenye Ziwa Nyasa. Tatizo lenyewe ni kwamba Malawi wanadai kwamba ziwa lote kaskazini ya Msumbiji kuelekea Ruvuma na Mbeya ni mali yao kwa mujibu wa Mkataba wa Heligoland uliowekwa mwaka 1890.

Mheshimiwa Spika,
Tanzania kwa upande wetu tunasema kuw ampaka wa kweli kati yetu na malawi unapita katikati ya ziwa hivyo kufanya
eneo lote la Kaskazini Mashariki ya Ziwa kati Latitude digrii 9 na digrii 11 kuwa mali ya Tanzania kwa mujibu wa mkata huouo wa Heligoland wa mwaka 1890 ambao ulikubali kuwa kwa vile kuna maeneo ya mpaka ambayo hayana mantiki, pande zinazohusiana zikutane na kurekebisha. Aidha tunazo ramani ambazo waingereza wenyewe walipitisha mpaka katikati kama ulivyo mpaka kati ya Msumbiji na Malawi.
****

Nimemalizia hapa kwa sababu mengine yanayofuata ni diplomatic process. Sasa hapa tuchambue hotuba hii ya Membe. Binafsi nimeusoma mkataba wote wa Heligoland na wala si alichokisema Membe. Kama membe anataka kuikomboa Tanzania walau tupate sehemu ya Ziwa basi washauri wake wamempotosha kutumia mkataba ule ambao hautetei hoja yake hata kidogo.

Lakini pia Membe ni mmoja wa wanaodhani watanzania wa sasa hawajui kufukua mambo na ndiyo maana kwenye thread yangu nimesema tutumie usomi wetu. Membe ametaja kwamba sehemu ya ziwa kati ya Latitude digrii 9 na digrii 11 ni mali ya Tanzania.

Hapa ndipo Membe ameumbuka umbuko ambalo hatalisahau. Kwa nini nasema kaumbuka. Kaumbuka kwa sababu geography ya Tanzania wote tunaijua. Ncha ya juu kabisa ya Lake Malawi iko kwenye coordinate { S9.49214 E34.03563} ambapo ni only 7.0km kutoka kijiji kiitwcho Matema kilichopo kwenye coordinate { S9.49601 E33.97215}.

Ukiangalia coordinate hizi maana yake ni kwamba Ziwa Malawi linaishia kwenye Latitude 9.49214. Sasa hapa Membe anasema eti ni kuanzia Latitude 9. Kwa maana hii ya Membe kama Ziwa ni letu kuanzia latitude 9 maana yake ni kwambaMmembe kafanya makosa kwa kulirefusha ziwa hili kwa umbali wa 54.4km kuelekea kaskazini!

Watu mnaotoka kusini hasa Mbeya mnafahamu sehemu iitwayo Matamba. Hapa coordinate zake ni { S9.01171 E34.09959}. Kwa mujibu wa Membe, hii Matamba ingekuwa imeguswa na Ziwa hili!

Hakika waliomletea Membe hizi data wamemvuruga kuliko kulietengeneza suala hili. Ziwa Malawi au Nyasa linaishia kwenye Latitude 9.49214 kama nilivyosema hapo juu. Hapa membe kadanganya Bunge na kadanganya watanzania kasi kwamba sijui sasa ni nani mwenye nguvu ya kulitetea hili.

Tuje sasa kwa upade wa kusini yaani unaotambuliwa na membe kama sehemu yaetu ya Ziwa. Membe anasema sisi mali yetu ni mpaka kwenye latitude 11. Sijui wangapi mmeona kosa hili la mwaka. Unaposema kwamba unaishia hapa kwenye Latitude 11, je mnaotetea hoja hii mnaelewa madhara yake? Kama hamyajui basi mimi nayasema hapa.

Kama Membe kasema Bungeni kwamba tunaishia kwenye Latitude 11 basi maana yake pale ni kaskazini ya sehemu iitwayo Liuli ambayo iko { S11.05023 E34.63908}. Kumbe, Mwanakijiji wa Liuli haruhusiwi kuvua samaki kwenye ziwa lile kwa sababu ni sehemu ya Malawi, kwa mujibu wa Waziri Bernard Membe!

Yaani mwanakijiji huyu wa Liuli, anakuwa amekiuka mpaka kwa kilomita 6.6 kwa mujibu wa Serikali anayoshiriki membe wala si kwa mujibu wa Serikali ya Malawi!

Nimeanza na mfano huo wa Liuli ambao najua wengine hampaju ahapo. Sasa tuje kwenye mfano ambao wengi mnaujua na mmeutumia kunipinga humu na kuniita mimi ni mmalawi.

Mfano wenyewe ni wa Mbamba Bay. Ndiyo maana nimesema kajipangeni hii kesi tutajikuta tunasambaratika tukidhani tunatetea huku tunajiangamiza. Narudia kusema kwa mujibu wa hotuba ya Waziri Membe ni kwamba umiliki wetu wa Ziwa hili unaishia kwenye latitude 11. Mbamba Bay iko kwenye coordinate { S11.30519 E34.80449}.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Mbamba Bay haiko katika eneo linalotambuliwa na Waziri Membe kwa latitude degree 0.30519!

Uki-convert hizi latitude kwenda kwenye kilomita basi maana yake Membe haitambui Mbamba Bay kwani iko 33.7km nje ya eneo ambalo Tanzania tunamiliki ziwa!

Waziri membe pia inaelekea kuwa hajui mpaka unavyopita pale Msumbiji. yeye anasema kule ni nunu kwa nusu lakini wote fungueni ramani muone kama hilo nalo lina ukweli. Mpaka wa Msumbiji ni nusu kwa nusu kuanzia kwenye latitude 11 had 13 lakini kuanzia hapo kueleka kule chini kusini ziwa lote liko sehemu ya Malawi na linaishia kwenye coordinate {S14.44635 E35.23539} ambako ni latitude 14.44635.

Hivyo, tujenge hoja zinazojikita kwenye ukweli na tusishabikie mambo kama vile Simba na Yanga. Hapa hatufanyi ushabiki. Hapa tunasaidia kujenga na kupima hoja kama kweli tunaweza kuisaidia nchi yetu kupata sehemu ya ziwa hili.

Ninasubiri kwa hamu kuona mtakuja na hoja gani kuhusu hizi findings zinazochambua hotuba ya Membe na matokeo yake niliyoeleza humu.
Ondoa supplimentary yako ya jiografia hapa jf wewe subiri tunaoijua mipaka kwa vitendo tukuonyeshe wewe na wamalawi wenzio!Huo usomi mbuzi wako usituletee hapa tunaijua nchi na wananchi wanaijua nchi kabla yako wewe na mmemkwa yako hiyo
 
Lakini baada ya kusoma speech ya Membe basi matumaini yote ya kulipata Lake Malawi yamenitoka. Narudia sipingi Tanzania kupata sehemu ndogo ya Lake Malawi kama baadhi mnavyoropoka. Na hata mnavyoropoa wengine hainipi matumani ya kulipata hilo Ziwa. Lakini aliyenisikitisha zaidi ni Waziri Membe na sasa kwangu ni dhahiri kwamba tusahau kabisa kulipata Ziwa hili.

Kwa nini hupingi sisi kupata sehemu ndogo? Kwa mawazo yako, hiyo sehemu ndogo, ni haki yetu kuipata au unaona tupewe kwa fadhila ya Wamalawi?
 
Kwakweli hizi mbio Za kugombea mali asili ambazo hazitalifaidisha taifa hata sizielewi,watanzania tuna mali asili kibao lakini sioni faida yake kwa taifa,acha wamalawi wachukue hilo ziwa labda wao watafanya maendeleo.
 
Kwa nini hupingi sisi kupata sehemu ndogo? Kwa mawazo yako, hiyo sehemu ndogo, ni haki yetu kuipata au unaona tupewe kwa fadhila ya Wamalawi?

Yaani huyu jamaa hili hoja yake iwe halali nilivyomsoma anataka hadi sehemu ya nchi kavu iwe ni ya malawi
 
Haya ndiyo makosa mengi yanayo waongoza vijana wetu, hizo coordinate unazotumia fanya utafiti ili ujiridhishe maana zimewekwa kati ya mwaka 1984-2000 na ndizo zinazotumiwa na Google katika ramani zake,

Google wameleta matatizo makubwa kila pembe ya dunia kwa ramani zake kupotosha mipaka halisi ya kikoloni!

Narudia tena mpaka halisi unaotambuliwa na Tanzania ni KATIKA ya Ziwa Nyasa kwa mujibu wa ARC1960.

NB:

Kuweni makini sana ndugu zangu kuna mamluki ndani ya nchi yetu walioanza siku nyingi kuuza siri, na mmoja ni huyu mwanzisha uzi huu wanajaribu kuwagawa na kupotosha umma juu ya ukweli halisi!

Mipaka mingi barani Afrika iliwekwa miaka ya 1800 na wakoloni! Hakukuwa na teknolojia za kisasa kama unavyopotosha umma hapa na ***** wako hapa!

Yeriko,

Nakuheshimu sana hivyo nakujibu kiheshima.

Kama umesoma post zangu zote hayo unayoyasema nimeyataja na nimeeleza kwamba mwaka 1960 MAPDATUM ya ramani zetu ilikuwa ARC1960. Na nikasema ramani zote hizi ziko pale Wizara ya ardhi.

Kuhusu Googleearth mimi niliacha kuitumia tangu mwaka 2006 baada ya kuwa inanipoteza. Juzi nimebishana na rafiki yangu ananishawishi niitumie anasema inamletea accurate measurement lakini bado sijawa na imani na googleearth. Tatizo la google earth ni kwamba inakutupa umbali hata wa kilomita tano toka actual point.

Hivyo, sijatoa kwenye google earth hizi coordinates hata kidogo na hata ukizichukua na ukaenda huko unaweza kukuta tofauti.

Lakini nikufundishe kitu kimoja kuhusu hizi MAPDATUM yaani ARC1960, WGS84 na zinginezo ziko zaidi ya 30. Hata kama kuna tofauti mara nyingi haifiki kilometa moja. hivyo mwenye ARC1960 na WGS1984 hamtazidiana zaidi ya kilomita moja.

Waziri hakutaja ametumia MAPDATUM ipi. Binafsi nilitarajia atumie ARC1960 na wakati naandika hii post nililizingatia hili. Hivyo ondoa kabisa mashaka na coordinate hizi kwani gap aliloleta Membe ni kubwa si chini ya kilomita 20.

Huwezi kumtetea Membe alivyoitanga Mbamba Bay kwa kigezo cha MAPDATUM ya ama WGS84 au ARC1960 wakati kaitenga Mbamba bay kwa 33.7km!

Kaliongezea urefu ziwa Malawi kwa kilomita zaidi ya 50. Hapo hoja ya MAPDATUM kwamba ni ARC1960 au WGS84 haina mshiko kabisa ndugu yangu.
 
Mimi hata sielewi haya mahesabu yenu ya LATITUDE maana nilichokisikia Membe akisema ni kuhusu SEHEMU ya ZIWA kwani ndio unggonvi wetu na Malawi sio miji iliyopo na mipaka ya nchi kavu siku zote hai nyooki (straight)..Mimi nachoweza kusema ni kwamba Ile ilikuwa Tanganyika hivi sasa tuna nchi inaitwa tanzania ambayo mikapa yake ni tofauti kabisa na ile ilokuwepo sijui mwaka 1896..Sijui na sisi tuweke madai ya Rwanda na Burundi!..Nakumbuka vizuri sana Kenya waliwahi kusema Mlima Kilimanjaro upo Kenya na wakaja na ramani zao, Idd Amin naye akadai mto Kagera akaja na sababu zake, Wazanzibar nao sasa wanataka kuijua mpaka wao na Bara yaani hii laana ya Mafuta imekutufikia..

Marehemu Mwalimu Nyerere alipotembelea hapa mwaka 1999 kabla ya kifo chake alisema kitu hiki na wengi hatukumwelewa kabisa... Alisema (not exact word) "Kwa mwendo huu hatuwezi kuendelea hata kama yatapatikana mafuta, tena anaomba Mungu -mafuta yasipatikane maana tutakuja kuuana.".
 
hivi serikali haina ArcGIS hata MapInfo tu.

Error inayokubalika angalau +-5m, sasa mtu anaongelea Km? Kama ni kweli itakuwa ajabu.

Alitakiwa atume watu hata na GPS ya mkono wakahakiki kabla ya kutoa majibu bungeni.
 
Mi naona tulichukue ziwa lote liwe letu ikwzkn na malawi iwe sehemu kama zanzibar tu
 
hivi serikali haina ArcGIS hata MapInfo tu.

Error inayokubalika angalau +-5m, sasa mtu anaongelea Km? Kama ni kweli itakuwa ajabu.

Alitakiwa atume watu hata na GPS ya mkono wakahakiki kabla ya kutoa majibu bungeni.

Ndugu yangu Kongosho,

Kumbe wataalam mko wengi humu na mnaweza kusaidia. Unachokisema ndicho ambacho nimemjibu Yeriko Nyerere kwenye post namba 36.

Mimi sishangai hawa watu kupotoka hivi geographically tena sehemu ambako tulitarajia kuna wataalamu wa hizi geo-issues.

Hebu kumbuka Kafumu huyu mbunge wa Igunga. Unakumbuka kwamba yeye alikuwa commissioner wa madini hivyo geo-issues kwake haikutakiwa kuwa tatizo.

Lakini si unakumbuka kituko kilichomtokea wakati wa kampeni kule Igunga kwamba alipanda helicopter kwenda kukampeni kijiji kimoja na kisha helikopta ikapotea na kukikosa kijiji kile. Kisa ni mambo hayahaya tunayoyasema sasa, kutojua mapreading.

Ndiyo maana simshangai Membe na kuja na data zilizokosewa kwa umbali wa zaidi ya kilomita 30!!! Wewe na mimi tunaona ni kituko. Na ni kweli ni kituko cha mwaka kwani jinsi miaka inavyokwenda hata hiyo mita 5 accuracy yake inazidi kuwa improved.

Binafsi mimi nimefika mahala accuracy ya instruments zangu ni chini ya mita 3 na wala si 5 kama unazotaja hapo juu. Na ndiyo maana hizi coordinates nimeziandika nikiwa na uhakika huo hazitapingwa labda waje na topic tofauti kama wanavyofanya hapa wengine lakini si kuzi-dispute findings zangu.

Walio karibu na Membe wamueleza hili au asome yeye mwenyewe humu kuliko akae huko na kuiponda JF kwamba inawasakama wakati inawarekebisha marekebisho ambayo wataalamu wake huko serikalini wameshindwa na hadi kumpotosha.
 
jaribu kumuelewa na si kwamba mtu akijan na hoja then mnaanza kusema yeye ni mnyasa sijui mmalawi...hii thread imejikita zaidi kwenye hotuba ya membe...je membe yuko sahihi?? maana na yeye ametaja vi latitude...na kingine tusikimbilie kusema malawi hawawezi kumiliki ziwa lote hilo..sasa kama point zenu ni dhaifu kama za mebe ka nini wasimiliki?...tujikite kwenye hoja na kama tunaijua jiografi vizuri tulete ushahidi na sio kukimbilia kusema..wewe mmalawi

Edson hakuna kipya hapa. Yote ni marudio tumeshasoma na kujadili sana hili suala. Ninachoshangaa Nikupateje kulianzisha upya kwa staili nyingine wakati context ni ile ile.
Ziwa nyasa haliko straight kwamba lisimame usawa wa latitude x na longitude y mwanzo mwisho. Linaanzia latitude x hadi y na longitude a hadi b!
 
Last edited by a moderator:
Yaani huyu jamaa hili hoja yake iwe halali nilivyomsoma anataka hadi sehemu ya nchi kavu iwe ni ya malawi

Yaani anataka mtanzania ambaye yupo kwenye shore ya Lake Nyasa, akikanyaga maji tu kaingia Malawi na wamalawi wanaweza kumkamata kwa kuvuka mpaka bila visa? Na wamalawi waweze kufika within meter moja ya shore ya Lake Nyasa upande wa Tanzania bado wakawa wapo kwao na tusiwafanye lolote? Mtanzania akitaka kwenda kuvua aombe fadhila ya Wamalawi? Na ikitokea Tsunami mpaka ndo unaingia ndani zaidi Tanzania? This is the most ridiculous idea I have ever come across....
 
Edson hakuna kipya hapa. Yote ni marudio tumeshasoma na kujadili sana hili suala. Ninachoshangaa Nikupateje kulianzisha upya kwa staili nyingine wakati context ni ile ile.
Ziwa nyasa haliko straight kwamba lisimame usawa wa latitude x na longitude y mwanzo mwisho. Linaanzia latitude x hadi y na longitude a hadi b!

Hoja ni coordinate alizotaja Membe mle Bungeni na sijui kama hujui kwamba si mimi niliyemuandikia hotuba ile na kutaja latitudes 9 hadi 11!!!
It is that simple.
 
Nikupateje wengine hatusumbuki sana na kauli za membe anayesubiri kusikia sauti ya kuoteshwa. Huenda akioteshwa atarekebisha makosa unayojaribu kuyaainisha.
Umezungumzia mpaka wa Tanzania ziwa nyasa kuwa latitude 9 kwahiyo mji wa liuli kuwa nje ya nchi. Kitu ambacho unakimisi hapo ni kwamba hukujaribu kuangalia mipaka ya nchi kwa ujumla wake ili uone Tanzania inaanzia wapi na kuishia wapi in geographical point of view.
Kwakuwa ziwa nyasa haliko wima wima kwahiyo usahihi ni kusema eneo letu la ziwa nyasa linaanzia latitude x hadi y kaskazini na kuanzia latitude v hadi z kusini! Kwakufanya hivyo ndipo utaona hayo maeneo unayoyataja kama matamba na liuli yanabaki ndani ya nchi yetu na si kama ambavyo umetafsiri vibaya.
 
Last edited by a moderator:
Edson hakuna kipya hapa. Yote ni marudio tumeshasoma na kujadili sana hili suala. Ninachoshangaa Nikupateje kulianzisha upya kwa staili nyingine wakati context ni ile ile.
Ziwa nyasa haliko straight kwamba lisimame usawa wa latitude x na longitude y mwanzo mwisho. Linaanzia latitude x hadi y na longitude a hadi b!

ni wapi pengine tumejadili haya ma-latitude mkuu? ile thread yake nyingine ya jana alikuwa hajasoma gazeti la raia mwema..gazeti kalisoma leo na ndipo akaona hizo latitude 9 hadi 11 na ndipo akaanza kuangalia zimekaaje na akaaja na thread hii....ni kweli sehemu ya ziwa ni yetu lakini je hizo latitude za membe alizosoma bungeni ni sahihi? au zinapotosha umma?....juzi humu nilisoma comen ya mwana jf mmoja (de'levis) alisema hiyo tare 27 wakati wa mkutano wa membe na huyo wazir wa mambo ya nje wa malawo bwana chiume ..membe alisema ziwa hilo asilimia 50 ni mali ya tanznaia na asilimia 50 inayobaki ni ya malawi..ndipo waziri chiume akamuuliza kama ni hvyo hili ziwa limefika hadi mozambique na kuna sehemu ya ziwa hili ni mali ya mozambique sasa kama malawana tanaznia zinamiliki ziwa kwa 50 by 50 asilimia je msumbiji ina asilimia ngapi..kwa mujibu wa de'levis inasemakena membe alikaa kimya na hakujibu.....
na wewe usitaje x au Y sema kabisa kuwa latitude ni kadhaa kama alivyofanya mleta mada..tusiishie kusema tu kuwa mada ni ile ile hakuna jipya.....
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom