Waziri Bashungwa unakwama wapi? Wafanyabiashara wa mafuta hawawezi kuichezea Serikali hivi

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,511
2,000
Sana JF.

Wafanyabiashara ya mafuta ni dhahili kwamba Serikali kuoitia waziri wake pamoja na taasisi yake EWURA wameshindwa kutimiza wajibu wake, Dar sasa haina mafuta, ikitokea la kutokea mji mzima hakuna mafuta. Bagamoyo road yote karibu Sheri nyingi zimegoma kuleta mafuta.

Watanzania wengi wanamaisha mabaya wana mafuta ya kubipu wale wenye robo tank macho yanawatoka Pima maana kila uendapo kituoni unaonyeshwa mikono tu kuwa hawana mafuta.

Hawa jamaa ni wajanja sana, wao wameamua kugoma wafanyakazi wao wapo kazini lakini wanakwambia hakuna mafuta yapata wiki.

Kiburi cha wafanya biashara safari hii kimeiumbua serikali. Kama wanataka bei kufika elfu2000 basis watangaze au Serikali ikubali kuwashindwa watangaze bei watakayo. Ili nao wafanane na wakulima wanavyojitangazia bei Y
 

godimpare

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
2,679
2,000
Hao wafanya biashara wa mafuta ni malofa hawajui mafuta hushuka kila uchwao?hi ni kutokana demand kupungua sasa wanataka wahold mpka lini,wafanye biashara waache uzumbukuku,itafika mahala mafuta yatashuka hadi buku kama sio jero kwa lita subiri corona izae vijukuu
 

godimpare

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
2,679
2,000
Mafuta yanaenda kushuka mwezi huu mshuko ambao utapitiliza ,wauza mafuta sio wazembe kununua kwa bei ya juu toka serikalini,bei ya mafuta ghafi kwa pipa now ni 40$ (WTI) Yataenda drop hadi 10$ kwa pipa hii ni kutokana hakuna tena mahala pa kuhifadhi na mahitaji yanazidi kuporomoka kwa sababu ya covid
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
95,504
2,000
Mkuu siyo hapa dar tu leo hii nina rafiki yangu yupo mkoani mtwara anasema amekwama wilaya moja ya mkoa huo hakuna kabisa petrol
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
3,889
2,000
Mlivyoambiwa na kingunge kuwa Magufuli hakufaa kuwa Raisi bali nyapara ndo muelewe sasa. Tanzania tunarudi tena kipindi cha Nyerere cha bidhaa kuanza kuadimika. Huyo jamaa yenu kafeli kwenye uchumi na anachojua ni kutumia manguvu na si akili.

Huu ndo wakati wa watanzania kufunguka kiakili na kuwapa uongozi wa hii nchi Chadema. Hakuna sehemu duniani vyama vya kijamaa viliwai kufanikiwa. Never
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
95,504
2,000
Kuna hujuma kwenye mafuta. Nimetembea vituo kibao hakuna mafuta nimekuja kupata Boko magengeni.
Kama Mwijage alifutwa kazi kwa kushindwa issue ya korosho, basi na huyo Bashungwa apigwe chini kwa kushindwa kusimamia tatizo la mafuta.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
95,504
2,000
Kwetu bongo hakuna corona
Hao wafanya biashara wa mafuta ni malofa hawajui mafuta hushuka kila uchwao?hi ni kutokana demand kupungua sasa wanataka wahold mpka lini,wafanye biashara waache uzumbukuku,itafika mahala mafuta yatashuka hadi buku kama sio jero kwa lita subiri corona izae vijukuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom