Responded Waziri Aweso atoa maelekezo mabomba ya Kijiji cha Mayonje - Sumbawanga yatengenezwe na huduma ya maji irejee

Responded Waziri Aweso atoa maelekezo mabomba ya Kijiji cha Mayonje - Sumbawanga yatengenezwe na huduma ya maji irejee

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
WhatsApp Image 2026-02-09 at 16.25.46.jpeg
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameelekeza Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Sumbawanga Mkoa wa Rukwa Wilaya ya Sumbawanga kurekebisha mabomba yaliyoharibiwa Kijiji cha Mayonje, Kata ya Milepa katika Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini, ndani ya wiki moja ili kurejesha huduma.

Aweso ametoa malekezo hayo kupitia kwa Meneja wa RUWASA Mkoa, Eng Boazi Piusi Matundali ikiwa ni baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza kuwa Wakazi wa eneo hilo wanapitia changamoto ya kukosa huduma ya maji tangu mwezi wa 11, 2025 mwanzoni baada ya Uchaguzi Mkuu.

Mhandisi Matundali amesema “Kulitokea uharibifu wa mabomba na kilichochelewesha matengenezo ni kwa kuwa suala hilo lilikuwa linafanyiwa uchunguzi na Mamlaka za Kiusalama, lakini utaratibu umefanyika na tayari Waziri Aweso ameshatoa maelekezo ya matengenezo ambayo yatafanyika ndani ya wiki moja.

Pia soma ~ Kijiji cha Mayonje (Sumbawanga), tangu Novemba 2025 hatuna maji baada ya bomba kupasuka
 
Back
Top Bottom