Kutokana na kupungua kwa maji katika Mto Ruvu ambao unatumika kusambaza maji katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Pwani na mkoa wa Dar es Salaam, Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameiagiza DAWASA kushirikiana na wenye visima vya maji kutoa huduma hiyo ili kupunguza madhira yanayowapata wakazi wa mikoa hiyo.
Agizo hilo linatengua amri ya DAWASA iliyokuwa inawazuia wenye visima kusambaza maji.
=======
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kushirikiana na wadau wengine wenye visima vikubwa vya maji kutoa huduma ya maji kwa kipindi chote cha ukame.
Akikagua zoezi la uunganishaji wa mabomba ya maji eneo la Wazo mkoani Dar es Salaam, Waziri Aweso amesema wizara yake itashirikiana na DAWASA kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji katika kipindi chote cha ukame.
Pia ameielekeza DAWASA kuzingatia vema ratiba ya mgao wa maji na kugawa maji bila ya upendeo.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA mhandisi Cyprian Luhemeja amesema, mradi wa maji ya visima wa Kigamboni utakamilika siku ya Jumapili na hivyo kuwawezesha wananchi kupata huduma ya maji.
Tarehe 25 mwezi huu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla alitangaza kuanza rasmi kwa mgao wa maji mkoani humo na katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Pwani, kufuatia kupungua kwa kina cha maji katika mto Ruvu.
TBC Online