ichumu lya
JF-Expert Member
- Aug 11, 2016
- 2,605
- 2,729
Kumbe Mwijage alikua ni mlango sasa ulitolewa mlango wa debe ikawekwa pazia, Tanzania yangu jamanii.
Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amewataka raia wa China nchini wakitaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wa Watanzania wafuate taratibu.
Kakunda ametoa kauli hiyo jana jioni Desemba 7, 2018 wakati akizindua kituo cha maonyesho ya bidhaa za Kichina kilichopo Keko jijini Dar es Salaam.
Amesema nafasi za uwekezaji Tanzania na kuwakaribisha Wachina kuwekeza, kuwataka pale wanapotaka wanawake wanapaswa kufuata sheria na taratibu na kuachana na tabia ya kusimama na mabinti vichochoroni na kuwaachia watoto.
“Huku kwetu huwa tunakwenda kwa wazazi kujitambulisha kwa kutoa posa na kuoa kwa sherehe kubwa na mdundiko unapigwa,” amesema Kakunda.
“Fuateni taratibu hizo acheni kusimama simama vichochoroni na wasichana wa watu, hii nchi ya amani mkifanya hivyo mnawakera wazazi wao.”
Kakunda amewataka Wachina hao kuendeleza urafiki wa nchi hizo mbili kwa kuishi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi.
“Njooni muwekeze lakini dumisheni urafiki ulioanzishwa na waasisi wa nchi yetu na China kwa kufuata mila, tamaduni za nchi, mziheshimu.
Ameongeza, “Mkienda Arusha kuna Wamasai wana taratibu zao wakati mwingine wanavaa shuka pekee bila kitu kingine ndani msistuke ndiyo tamaduni zao, hivyo mnapaswa kuziheshimu.”
Wakati akizungumza alikuwa na mkalimani aliyekuwa akitafsiri kwa Kichina na kuwafanya raia wa nchi hiyo waliokuwa eneo hilo kuangua kicheko.
Chanzo: Mwananchi