Waziri ataka wapiga debe waondolewe Dar

Waziri ataka wapiga debe waondolewe Dar

wanaudhi sana wapiga debe. ving'ang'anizi hadi basi haaaa
 
SIKU moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuwaagiza wakuu wa mikoa wapya kuwakamata vijana wote ambao wanacheza (poolTable) nyakati za asubuhi,kwa madai kuwa wajiingize kwenye shughuli za ufanyaji kazi,

Naye,Waziri nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhakikisha anawaaondoa wapiga “debe” wote kwenye vituo vya mabasi kwa madai kuwa wanafanya vitendo vya kihalifu. Waziri Simbachawene ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam,wakati wa semina kwa wakuu wa mikoa wote nchini ambao waliapishwa jana na Rais Magufuli,

Ambapo alitumia nafasi hiyo kwa kusema kazi ya kupiga debe sio rasmi na aina kipato kitachoweza kumkwamua kijana kuondokana na tatizo la umasikini,

“Yaani hata hapa Dar es salaam namuomba mkuu wa mkoa ahakikishe anawondoa hawa wapiga debe kwenye vituo vya mabasi kwani wamekuwa wakichangia kutokea kwa uharifu,kipato cha mpiga debe kwa siku hakiwezi kumkwamua kimaisha sana sana wanatumia nafasi hiyo kufanya uharifu wanatakiwa kuondolewa haraka waende kwenye kazi hata za kilimo”amesema Simbachawene.

Hata Hivyo Waziri Simbachane ametumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa mikoa kufanya kazi kwa ufasaha na kuwatumikia wananchi ikiwemo kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
Angeyasema haya wakati wa uchaguzi ingependeza sana!
 
Kuwafukuza wapiga debe sioni kama ni sawa, inapaswa kwanza kukaa nao na kuona changamoto zinazowakabili na kujua namna ya kulimaliza tatizo, kwanza hakuna mtu anayetoka kilosa au sikonge kwenda dar kupiga debe, wapiga debe ni madaiwaka, jamaa zao madereva na makonda wa daladala badala ya kushinda nyumbani wakizozana na shemeji zao huchukuliwa na kaka zao kuwasaidia kazi mfano kuangalia gari wakati dereva kaenda msalani.

wapo wapiga debe wanatumika kulipa visasi kwa abiria wakorofi mfano mtu anakataa kutoa nauli makusudi kwa kujiona wao ni mabaunsa au maboxer hawa husakiziwa kwa mateja kwa ujira wa pesa kidogo ya ngada.

Njia nzuri ya kumaliza tatizo la wapiga debe ni kuwajengea uwezo wakaunda umoja wao ukasajiriwa wakatambulika rasmi hivyo wakawa na uongozi na kamati zao zitakazosaidia kushughulikiana wao kwa wao badala ya kuhusisha dola. Wao wapiga debe wanamjua kibaka ni nani na teja ni lipi. Hata likitokea tukio la wizi basi nirahisi kwa kushirikiana na viongozi wao ni rahisi kumpata mhalifu.
 
huwezi kuishi kutegemea kutafuniwa kila kitu, wanaolima wametafutiwa na nani maeneo?
Aisee hizo sio kauri za kizalendo. Hujui matatizo tunayoyapata tuliozaliwa kwenye familia masikini ambazo hata tukikua hatuna referees. Fikilia kwa makini hapo ulipo wewe kwa sasa ni nani alikushika mkono mpaka upo hivyo. Siwatetei wapiga debe ila pia serikali iliahidi kuzalisha ajira nyingi kwakua inajua ni tatizo kubwa. Alafu kama ni kuhusu kipato hata vijana walioko vijijini vipato huwatosha kula tu na familia zao. Wenye uwezo ni wale ambao familia zao zina historia ya utajiri na waliwekeza kwenye ardhi. Tusishabikie kila kitu itatukost
 
Hapa nilipo naishi kibishi kama maskini wengine ktk nchi hii wanaojitahidi kujikwamua kila kuchwao, nilichotaka kusema ni kuwa, hii dhana ya kila kitu uiangalie serikali huwa kwa kiasi kikubwa haisaidii na mwishowe watu wanaishia kulalamika na kujenga chuki zisizo za msingi wakati uki fight mwenyewe uwezekano upo kabisa kujikwamua, wangapi wamefanikiwa bila kubebwa, dhana ya kujitegemea raia wengi wa tz hawajaielewa kwa mapana yake, hakuna ushabiki huu ni uhalisia, epuka excuses kwenye maisha, hazijengi!
 
SIKU moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuwaagiza wakuu wa mikoa wapya kuwakamata vijana wote ambao wanacheza (poolTable) nyakati za asubuhi,kwa madai kuwa wajiingize kwenye shughuli za ufanyaji kazi,

Naye,Waziri nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhakikisha anawaaondoa wapiga “debe” wote kwenye vituo vya mabasi kwa madai kuwa wanafanya vitendo vya kihalifu. Waziri Simbachawene ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam,wakati wa semina kwa wakuu wa mikoa wote nchini ambao waliapishwa jana na Rais Magufuli,

Ambapo alitumia nafasi hiyo kwa kusema kazi ya kupiga debe sio rasmi na aina kipato kitachoweza kumkwamua kijana kuondokana na tatizo la umasikini,

“Yaani hata hapa Dar es salaam namuomba mkuu wa mkoa ahakikishe anawondoa hawa wapiga debe kwenye vituo vya mabasi kwani wamekuwa wakichangia kutokea kwa uharifu,kipato cha mpiga debe kwa siku hakiwezi kumkwamua kimaisha sana sana wanatumia nafasi hiyo kufanya uharifu wanatakiwa kuondolewa haraka waende kwenye kazi hata za kilimo”amesema Simbachawene.

Hata Hivyo Waziri Simbachane ametumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa mikoa kufanya kazi kwa ufasaha na kuwatumikia wananchi ikiwemo kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.[/QUOTE Akiweza kufungua vichochoro vyote ambavyo watu wameviziba ambapo hakuna gari la taka wala fire linaweza pita na wengine wamevifanya garages bubu nitajua Dar tumepata Kandoro mwingine hacheki na nyani
 
K
Mbona yeye alikuwa mpiga debe stand ya mabasi dodoma?
Kweli aisee!, mbona wapiga debe wa magari ya champion wanawaliza sana wagogo(abiria) kwa kulipa nauli kubwa zisizo halali, inamaana kwao dodoma hajawaona? Kwanini aseme dar tu?, anakazana kusifia mke wa jirani wakati hata wakwake kapendeza!
 
Halafu ipitishwe sheria mtaa ukikutwa na teja mwenyekiti wa serikali ya mtaa na mjumbe wa nyumba kumi wachukuliwe hatua. Tutanyooka tu na hata tukipita kwa mtogole saa nane usiku hatufungi madirisha na tutaperuzi kama kawa
 
Hapa nilipo naishi kibishi kama maskini wengine ktk nchi hii wanaojitahidi kujikwamua kila kuchwao, nilichotaka kusema ni kuwa, hii dhana ya kila kitu uiangalie serikali huwa kwa kiasi kikubwa haisaidii na mwishowe watu wanaishia kulalamika na kujenga chuki zisizo za msingi wakati uki fight mwenyewe uwezekano upo kabisa kujikwamua, wangapi wamefanikiwa bila kubebwa, dhana ya kujitegemea raia wengi wa tz hawajaielewa kwa mapana yake, hakuna ushabiki huu ni uhalisia, epuka excuses kwenye maisha, hazijengi!
Hata hao wapiga debe ndo wameona wanajikwamua hapo mkuu. Kwahiyo kuwafukuza ni kuwaathiri kisaikolojia. Kumbuka hii nchi ina serikali. Si uungwana kuwatimua watu hovyo bila kujua unawapeleka wapi na kufanya nini? Kama wameweza kutambua vipato vyao havitoshi, je wamefikilia nn kiwaongezea kipato? Au hata hicho kidogo wananyang'anywa. Sio poa mkuu. Liangalie kwa jicho la tatu hili suala
 
Mpaka leo hujaona kuwa kipato cha mpiga debe hakijitoshelezi? ni aibu mwanaume mzima mwenye nguvu kufikiria inatosha kuishi kwa kazi kama hiyo, ni tatizo lingine la mwafrika, tunaridhika kizembe mno, ni muda sasa kulazimishwa kutumia ubongo kama wenywe tumeshindwa kufikiri!
 
Mkuu sikatai hakiwatoshi. Je waache kabisa ili wakose vyote? Kumbuka tumetofautiana elimu na maarifa. Alafu lazima ujue kuwa kuna mtu akipata chakula tu, kwake anaona ni sawa. Je tutumie nguvu kumnyang'anya chakula ili apate na hela ya ziada au tumpe elimu ya kuongeza kipato? Na je unajiuliza ni wangapi hawafanyi hata hiyo kazi wapo tu wanamaliza visigino kutafuta ujira. Tutumie busara badala ya nguvu kutatua matatizo ya nchi yetu. Nani hajui ajira ni tatizo. Je huko mnakowasukumia wakalime. Je, mmewapa mitaji na elimu ya kutosha? Tuache ushabiki. Nyie wasomi ndo mnapaswa kuwa mstari wa mbele kuielimisha jamii
 
Duh tunarudi kule kule, sio kwamba waache na wasifanye kitu, la hasha, na sio lazima uwe umesoma....na sio lazima ukalime, yapo mengi ya kufanya
 
Hao wapiga debe Ubungo wengi wao ni wezi. Mwaka Jana nilishuhidia mama mmoja kutoka safari ya akilia majira ya saa 2 usiku eti alirmbebea begi hamuoni. Kwa hyo waondolewe tu. Pili wanatudalalia nauli kwenye mabasi ilihali magari sie tunayajua.Ila sina uhakika kama wakuu watafanikiwa kwa hili wazo
 
Wengi wao ni wavuta unga cocaine bangi milungi nk hawa jamaa hawafai kabisa makonda na madereva hawapumui, kila kituo unawakuta wamejazanani wezi ajabu mnapanda nae gari akishuka ujue mtu keshalizwa , wako wengi sana sura tu akikuangalia unakimbia mwenyewe, hata tukiwapeleka wakalime sina uhakika kama wataweza maana mda wote wamelewa

Hayo uliyosema umesahau na hili la hawa jamaa kuwa kiwanda cha matusi. Kuna siku nilikuwa na mama yangu na mtoto wangu, daa ile siku sintokaa niisahau, yalimwaga matusi ya nguoni mpaka kila mtu ilibidi aombe dereva aondoe gari. Nilikuwa namuibia jicho mama yangu na mtoto wangu jinsi yale matusi yalivyokuwa yanaghaniwa kila mmoja alitahayari. Jioni mama yangu alinisihi anaomba watoto wangu akiondoka arudi nao kijijini kuogopa watoto wasije kuharibika. Wakati ule mama yangu alikuwa na miaka 55 lakini sidhani kama kwenye maisha yake aliwahi kusikia matusi ya kiwango kile na umri wake wote. Nadhani wasiishie hapo tu, bali wawaondoe na madalali wa mazao, hao ndio kaburi la wakulima. Unatoka na mazao yako kijijini ukifika huuzi mpaka wao wakubali na bei wanayokupa ni ya kukumaliza na ole wako ukatae wakati uko na mazao yanayoharibika kama nyanya, papai nk hakuna rangi utaacha kuona.
 
Back
Top Bottom