Waziri ataka wapiga debe waondolewe Dar

ilo nalo neno,, na haMna saBaBu ya Msingi wao kuwepo zaidi ya kipiga kelele na kutengeneza Magenge ya uhalifu,, Big up Mwsh. SiMBachawene.
wateja wakuu wa unga ni hao majamaa nashangaa wanakaa vituoni wengi ni vibaka wana afya za kutisha nadhani hao ndo wangekuwa wa1 kukusanywa wakapelekwa kwenye kambi za kulima haiingii akilini wenzao yaani konda na dereva wanapigika wao wanakusanya ushuru gari zote zimeanzzikwa zinapoelekea wao makelele na kuvizia abiriawawa
 
Njia rahisi ni kuhakikisha mradi wa mabasi yaendayo kasi unaanza kazi, mabasi yapo barabara tayari sielewi ni nini kinachokwamisha.
Tanzania ni kubwa jamaa yangu, usifikiri ameongelea wapiga debe wa Dar pekee, wapo mpaka Liwale na Nachingwea
 
hawa jamaa ndo shughuri zao kila siku kuna wapiga debe wana maisha mazuri,ambao awali unga wanajua nini wanachokitafuta mi nadhani waandaliwe utaratibu maalum hata ikitokea uhalifu eneo lao LA kazi wao ndo wakujua nani kafanya,lakini kuwaondoa ni kuongeza vibaka loba na kabari zitakua nyingi mitaani
 
SIKU moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuwaagiza wakuu wa mikoa wapya kuwakamata vijana wote ambao wanacheza (poolTable) nyakati za asubuhi,kwa madai kuwa wajiingize kwenye shughuli za ufanyaji kazi,

Naye,Waziri nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhakikisha anawaaondoa wapiga “debe” wote kwenye vituo vya mabasi kwa madai kuwa wanafanya vitendo vya kihalifu. Waziri Simbachawene ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam,wakati wa semina kwa wakuu wa mikoa wote nchini ambao waliapishwa jana na Rais Magufuli,

Ambapo alitumia nafasi hiyo kwa kusema kazi ya kupiga debe sio rasmi na aina kipato kitachoweza kumkwamua kijana kuondokana na tatizo la umasikini,

“Yaani hata hapa Dar es salaam namuomba mkuu wa mkoa ahakikishe anawondoa hawa wapiga debe kwenye vituo vya mabasi kwani wamekuwa wakichangia kutokea kwa uharifu,kipato cha mpiga debe kwa siku hakiwezi kumkwamua kimaisha sana sana wanatumia nafasi hiyo kufanya uharifu wanatakiwa kuondolewa haraka waende kwenye kazi hata za kilimo”amesema Simbachawene.

Hata Hivyo Waziri Simbachane ametumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa mikoa kufanya kazi kwa ufasaha na kuwatumikia wananchi ikiwemo kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
Hili jambo si rahisi,,yaani halihusiani na siasa kabisa....Litaleta balaaaa.....ni vyema kuwashirikisha wataalamu wa masuala ya uchumi...afya....ustawi wa jamiii na wawekezaji.....SI KITU RAHISI KAMWE.
 
Back
Top Bottom