Waziri ataka wapiga debe waondolewe Dar

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,186
9,288
SIKU moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuwaagiza wakuu wa mikoa wapya kuwakamata vijana wote ambao wanacheza (poolTable) nyakati za asubuhi,kwa madai kuwa wajiingize kwenye shughuli za ufanyaji kazi,

Naye,Waziri nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhakikisha anawaaondoa wapiga “debe” wote kwenye vituo vya mabasi kwa madai kuwa wanafanya vitendo vya kihalifu. Waziri Simbachawene ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam,wakati wa semina kwa wakuu wa mikoa wote nchini ambao waliapishwa jana na Rais Magufuli,

Ambapo alitumia nafasi hiyo kwa kusema kazi ya kupiga debe sio rasmi na aina kipato kitachoweza kumkwamua kijana kuondokana na tatizo la umasikini,

“Yaani hata hapa Dar es salaam namuomba mkuu wa mkoa ahakikishe anawondoa hawa wapiga debe kwenye vituo vya mabasi kwani wamekuwa wakichangia kutokea kwa uharifu,kipato cha mpiga debe kwa siku hakiwezi kumkwamua kimaisha sana sana wanatumia nafasi hiyo kufanya uharifu wanatakiwa kuondolewa haraka waende kwenye kazi hata za kilimo”amesema Simbachawene.

Hata Hivyo Waziri Simbachane ametumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa mikoa kufanya kazi kwa ufasaha na kuwatumikia wananchi ikiwemo kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
 
SIKU moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuwaagiza wakuu wa mikoa wapya kuwakamata vijana wote ambao wanacheza (poolTable) nyakati za asubuhi,kwa madai kuwa wajiingize kwenye shughuli za ufanyaji kazi,

Naye,Waziri nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhakikisha anawaaondoa wapiga “debe” wote kwenye vituo vya mabasi kwa madai kuwa wanafanya vitendo vya kiharifu. Waziri Simbachawene ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam,wakati wa semina kwa wakuu wa mikoa wote nchini ambao waliapishwa jana na Rais Magufuli,

Ambapo alitumia nafasi hiyo kwa kusema kazi ya kupiga debe sio rasmi na aina kipato kitachoweza kumkwamua kijana kuondokana na tatizo la umasikini,
,
“Yaani hata hapa Dar es salaam namuomba mkuu wa mkoa ahakikishe anawondoa hawa wapiga debe kwenye vituo vya mabasi kwani wamekuwa wakichangia kutokea kwa uharifu,kipato cha mpiga debe kwa siku hakiwezi kumkwamua kimaisha sana sana wanatumia nafasi hiyo kufanya uharifu wanatakiwa kuondolewa haraka waende kwenye kazi hata za kilimo”amesema Simbachawene.

Hata Hivyo Waziri Simbachane ametumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa mikoa kufanya kazi kwa ufasaha na kuwatumikia wananchi ikiwemo kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
Wapiga debe ni kama Mungiki wa kenya wanahodhi taratibu za kisheria kwa kujidai wao ndio wenye maamuzi kwenye vituo vya mabasi/dalalala hufunga milango hadi gari lijae ,hukusanya fedha isiyoenda serikalini ,hukaa tu wakisubiri migao bandia ya vipato kutoka kwa madereva wa mabasi/daladala.Hao wacha waondolewe tu ni sawa na wacheza pool,kama daladala zina majina ya route na kama mabasi yana ofisi za kukatia tiketi
 
Wengi wao ni wavuta unga cocaine bangi milungi nk hawa jamaa hawafai kabisa makonda na madereva hawapumui, kila kituo unawakuta wamejazanani wezi ajabu mnapanda nae gari akishuka ujue mtu keshalizwa , wako wengi sana sura tu akikuangalia unakimbia mwenyewe, hata tukiwapeleka wakalime sina uhakika kama wataweza maana mda wote wamelewa
 
Atupe pembejeo na mashamba bil kusahau kutututafutia soko. N a sio kulangua mazao yetu halafu wao wanakwenda kuuza Nje ya nchi kwa dola Tumeshtuka maana rizimoko alifanya hivyo akenda kuuza Un kwa kutumia magari ya sekta nyeti tz
 
Hawa jamaa huwa wanaingiza zaid ya buku 10 kwa siku .. Mi naona watafutiwe utaratibu , sabab hii haitapunguza uhalifu , bali itaongeza mara dufu , awa jamaa wengi wao ni watu walioadhirika na unga / weed .. Serikali isikurupuke hapa , hawa watu sio wacheza pooltable , hii ni kazi yao , inayowaingizia kipato chao cha kila siku , though inawezekana kuwa ni kweli wanafanya uhalifu ,lakin lets admit , in the past few years vitendo vingi vya upakuaji vimepungua kwa asilimia kubwa sana , hata wezi kuchomwa moto siku Dar hatusikii sana . kuna uwezekano wa kuzika vijana wengi sana kama serikali itakurupuka na kuziba hata hii mianya michache wanaotumia hawa vijana kujipatia ulaji wao .
 
Back
Top Bottom