Waziri anapozindua choo cha matundu nane!

Waziri anapozindua choo cha matundu nane!

Joined
Sep 26, 2013
Posts
33
Reaction score
10
Heshima kwenu wana JF

Hili ni jambo linaloweza kuwa la kuchekesha lakini ndipo CCM ilipotufikisha
Ndugu wadau siku chache zilizopita kulikuwa na shamra shamra,hoi hoi na nderemo hapa jimboni Mwanga kwa Profesa maghembe. Kulikuwa na tukio la ajabu kidogo kufanywa na kiongozi wa Kitaifa hasa level ya Uwaziri

Naam! ni kuzindua choo cha wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwanga ambapo Mheshimiwa Wazir Profesa Maghembe ndie alikuwa mgeni Rasmi! Gharama za ujenzi wa choo hicho zimegharamikiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi na wafadhili wa Ahsante Tours ya Moshi. Mfuko wa jimbo ulichangia Tsh 600,000/= kwenye ujenzi huo ambao umegharimu jumla ya fedha za kitanzani tsh 9,000,000/=

Kioja ni kuwa choo hicho ni cha kawaida sana na wala hapakuhitajika sherehe ya gharama kubwa kukizindua huku shule hiyo ikiwa haina vitabu vya kutosha , walimu kununua chaki kwa pesa zao wenyewe.

All in All Cheo cha Uwaziri ni Cheo kikubwa sana kufanya shughuli hiyo ya Uzinduzi wa Choo. Hii ni kudhalilisha kabisa serikali kwani fedha/ Muda huo uliotumika kwa watumishi na watendaji wa Halmashauri plus mafuta ya magari vingetosha kabisa kufanya kitu kingine cha maana kama kuwanunulia watoto hao vitabu na mahitaji mengine ya kuendesha shule.

Hiyo ndio serikali ya CCM ya miaka hii sasa sijui tukiwaongezea 2015 itakuwaje! maana kwa upuuzi huu mdogo tu sijui

Source: mimi mwenyewe na kamera niliopigia picha imechukuliwa na wasaidizi wa Waziri!
 
ngoja kwanza lumumba waje nitarudi.
cc simiyu yetu
 
NANGERA ECHUNGUKE
===>Kama ulipigia kura jembe na myundo jikanye mwenyewe,kama ndugu zako walipigia jembe na nyundo na wao pia wakanye,ukisipowakanya usije kulalamika hapa tena,hasa Desemba 2015.
 
Ha ha ha jf mpaka chooni,nadunda nayo sahv huku nakuny*
 
we ulitaka kizinduliwe na nani?

Sio level yake Waziri kuzindua choo tena cha kienyeji na ukizingatia na umbali wa safari yenyewe.Hizo ni kazi za madiwani wa sehemu husika.Inaonyesha ni jinsi gani viongozi wa chama kilichochoka na wao wamechoka hata mawazo na hawawezi hata kubuni kazi za kututoa hapa alipotuachia nyerere!
 
Hiyo kamera wamesema watakurudishia? Pole kamanda.
 
Heshima kwenu wana JF

Hili ni jambo linaloweza kuwa la kuchekesha lakini ndipo CCM ilipotufikisha
Ndugu wadau siku chache zilizopita kulikuwa na shamra shamra,hoi hoi na nderemo hapa jimboni Mwanga kwa Profesa maghembe. Kulikuwa na tukio la ajabu kidogo kufanywa na kiongozi wa Kitaifa hasa level ya Uwaziri

Naam! ni kuzindua choo cha wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwanga ambapo Mheshimiwa Wazir Profesa Maghembe ndie alikuwa mgeni Rasmi! Gharama za ujenzi wa choo hicho zimegharamikiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi na wafadhili wa Ahsante Tours ya Moshi. Mfuko wa jimbo ulichangia Tsh 600,000/= kwenye ujenzi huo ambao umegharimu jumla ya fedha za kitanzani tsh 9,000,000/=

Kioja ni kuwa choo hicho ni cha kawaida sana na wala hapakuhitajika sherehe ya gharama kubwa kukizindua huku shule hiyo ikiwa haina vitabu vya kutosha , walimu kununua chaki kwa pesa zao wenyewe.

All in All Cheo cha Uwaziri ni Cheo kikubwa sana kufanya shughuli hiyo ya Uzinduzi wa Choo. Hii ni kudhalilisha kabisa serikali kwani fedha/ Muda huo uliotumika kwa watumishi na watendaji wa Halmashauri plus mafuta ya magari vingetosha kabisa kufanya kitu kingine cha maana kama kuwanunulia watoto hao vitabu na mahitaji mengine ya kuendesha shule.

Hiyo ndio serikali ya CCM ya miaka hii sasa sijui tukiwaongezea 2015 itakuwaje! maana kwa upuuzi huu mdogo tu sijui

Source: mimi mwenyewe na kamera niliopigia picha imechukuliwa na wasaidizi wa Waziri!

NANGERA!

Ukishaona hivyo, ndio ujue mi-CCM imeshaishiwa hoja za maendeleo. Hivi nyumba ya kuhifadhi M.A.V.I. ndio inasherehekewa kiasi hicho? Kwamba choo ni suala la ziada na si sehemu ya maisha ya kila siku kwa wanafunzi wawapo shuleni??

Kweli watu wameweka u-Prof wao mifukoni ili wajiaminishe kula yao ya kesho.
 
Mkuu embu tujuze zaidi,profesa alizindua kwa kunya umo chooni au alikojoa!

Sasa nafasi ya viongozi wetu kama Madiwani, Wabunge watafanya kazi gani jamani??? Yaani Profesor ameshindwa kazi wizarani kwake anakwenda kujikomba kwa wananchi kwa choo cha msaada. Duh aibu!!!
 
MaCCM yanatuona misukule kiasi kwamba hata choo wanaona kama sio haki ya watoto wa shule kuwa nacho bali Ni fadhila za mbunge. CCM standards are very poor, ndio akili zao zilipoishia hapo. Waziri kuzindua choo
 
Mkuu weka picha ya choo hicho,may ni flush toilet(ya kizungu au arabic)
Mkuu Ucjali nitakuwekea mda ukifika nivumilie kwanza nihudhurie Mkutano wa M4C si unajua wapo kwa siku 16 hapa jimboni kunyorosha magamba!
 
alitakiwa azindue kwa kutupia kidogo angalau hata kojo, ila gharama pamoja maudhulio ya prof. hapo kuna shaka
 
Hiyo ndo Chukua Chako Mapema....chezea hicho chama wewe? Usipokuwa makini hata ukikamilisha ujenzi wa nyumba yako wanaweza kuja kuzindua wao....
 
Kama uwezi kufurahia kidogo hata kikubwa uwezi hata kidogo
 
Back
Top Bottom