Inauma sana!
Kulipa Kodi ni wajibu wa kila mtu aliyeko ktk dunia hii
Wananchi hasa walalahoi wamekuwa kama ni shamba la Bibi, walaji wa mavuno hayo ni hao wanaowapangia wananchi kulipa Kodi za ajabu ajabu,
Bajeti hii, inapokuja na Kodi ya nyumba kuingizwa kwenye mfumo wa Luku, aliyelengwa hapo si mwingine, ni mlala hoi huyuhyu anayelipa Kodi Kwa mijeredi ya police, wenye nyumba na matajiri wakiendelea kuneemeka.
Wananchi walalahoi hukamuliwa kama sweta, mbali na kuendelea kuwa waaminifu katika kulipa Kodi, ajabu ni pale Kodi nyingi zinapoishia mikononi mwa waliojuu, wenye kuwapangia maisha Yao yaweje
Kodi nyingi zinazokuwa zinapangwa, utadhani mtu huwa anakelekwa Sana na uwepo wa watu wa chini, na pengine huwa wanajiambia hawa watu ni wa kukamua haswaa, na kwa sababu hiyo, wananchi wa kawaida ndio haswaa, hufunga mikanda Kwa kukamliwa ili mambo ya nchi Yao yaende, ni Jambo jema.
Kinachouma sana ni pale walipa kodi wamefanya wajibu wao, halafu wasimamizi wa fedha hizo, wanazigawana ju kwa juu.
Hivi majuzi, kumetokea uotevu wa mabilioni ya fedha katika wizara ya fedha, Fedha hizi, hakuna aliyewajibika, na fedha zimepotea
Inauma sana pale mlalahoi anapotoa kodi yake akiamini huduma za kijamii atazipata, kumbe kuna genge la watu wachache waliojifanya mchwa, wakula pesa za walala Hoi na hawawajibishwi.
Kitendo cha kupotea mabilioni ya fedha katika wizara husika, waziri kuendelea kuwepo, ni kuruhusu wanyonge na walipa kodi waendelee kuishi maisha magumu katika hali ya kukosa miundombinu ya uhakika na kukosa huduma mhimu, mbaya zaidi, kitendo hiki kinaweza kutafsiliwa kwamba, ni kuendelea kuwanyonga walala Hoi walipa kodi na wao kufurahia kugawana jasho lao bila ya kuchukuliwa hatua.
Ni vyema sasa, kila mtu anapobainika amekula fedha za walipa kodi, awajibishwe kama mlalahoi anapofuatiliwa kiasi cha kufikishwa police akidaiwa Kodi ya Tsh 20000.
Inakuwaje kwa hao wanaoiba mabilioni ya fedha wakiachwa bila kuchukuliwa hatua, upotevu wa mabilioni ya juzi, waziri na katibu wake wanafanya nini ofisini?
Wananchi, hawajawahi kukataa kulipa Kodi kwa kuwa Kodi ndiyo inayowasogezea wananchi huduma
Tuwajibishane bila kuoneana aibu.