Waziri amuumbua Salva wa Ikulu

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
* Ni kuhusu ziara za mawaziri mikoani kutetea serikali awamu ya nne

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), Philip Marmo amesema kuwa mawaziri watazunguka mikoani kwa wiki mbili kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya nne maelezo ambayo yanapingana na yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, Salva Rweyemamu.

Mwananchi iliripoti wiki iliyopita kuwa serikali imetoa waraka unaowazuia mawaziri kusafiri nje na badala yake kuwataka kuzunguka mikoani kuelezea mafanikio ya serikali hiyo iliyoingia madarakani mwaka 2005, ikiwa ni mkakati uliopewa jina la "mlitutuma, tumetekeleza, tumerudi kuwaelezeni tulivyotekeleza na kuwasikiliza" ambao unaonekana ni kujipanga kabla ya uchaguzi mkuu.

Waraka huo pia unawataka mawaziri kukutana na watu wa aina mbalimbali kwenye ziara hizo, wakiwemo viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini msemaji huyo wa Ikulu alikimbilia kukanusha habari hizo akielezea habari hizo kuwa taarifa iliyochapishwa na gazeti hili ni za uongo, lakini hakufafanua sababu ya taarifa hizo kuwa za uongo.

Lakini jana, Waziri Marmo alikuwa mtulivu wakati alipotoa maelezo ya kina ya jinsi mawaziri hao watakavyotekeleza mpango huo ambao alisema safari hii utakuwa na mafanikio tofauti na ilivyokuwa mwaka 2007 wakati wananchi walipowazomea wasaidizi hao wa rais kiasi cha kuamua kufanya mikutano ya ndani.
Waziri Philip Marmo aliwaita wahariri wa vyombo vya habari ofisini kwake na kuwaelezea kuwa ziara hizo zinafanywa na mawaziri wote wa serikali hiyo katika mikoa 21 ya Tanzania Bara.

Hii inakuwa ni mara ya tatu kwa Ikulu kutoa maagizo kama hayo baada ya ziara ya kwanza iliyofanywa mwaka 2007 ya kutetea na kuelezea bajeti ya mwaka 2007/08, ambayo ilikuwa ya kwanza kwa serikali ya awamu ya nne.
Waziri Marmo aliwaambia wahariri hao kuwa lengo la safari hizo ni kuelezea utakelezaji wa serikali ya awamu ya nne, ambayo imekumbwa na matatizo ya aina tofauti, ikiwa ni pamoja na kupoteza mawaziri wanne, akiwemo Edward Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu.

Kama mnavyofahamu serikali ya awamu ya nne iliingia madarakani mwezi Desemba 2005. Wakati wa kuingia madarakani tulitoa ahadi mbalimbali kwa wananchi wetu, Tumeona kuwa ni busara kuwapa mrejesho wa jinsi tulivyotekeleza ahadi hizo katika kipindi cha miaka mitano," alisema Waziri Marmo.

"Ni haki yao kufahamu tumetekeleza nini na nini tumeshindwa kukitekeleza na kwa sababu gani," aliongeza Waziri Marmo.

Hata hivyo, Marmo ambaye alisema kuwa suala hilo si jambo geni kufanywa kwa serikali ya awamu hiyo na kwamba mawaziri wametakiwa kumaliza ziara zao kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano uliopangwa kuanza mapema wiki ijayo.

Akiongea kwa kujigamba, Waziri Marmo alisema kuwa safari hii hawatarajii kuzomewa tena na wananchi na badala yake wanatarajia kushangiliwa na wananchi wa mikoa ambayo mawaziri hao watazungukia kwa kuwa serikali hiyo imejipanga na imefanya kazi nzuri katika kipindi chake.

"Safari hii hatutarajii kuzomewa tena, tunatajaria kushangiliwa kwa sababu serikali imefanyakazi yake kama ilivyotajariwa," alisema Waziri Marmo.

Tayari mawaziri waliopangiwa tarehe za mwanzo wameshafanya ziara zao, akiwemo Waziri Mary Nagu, ambaye alikutana na wakati mgumu mjini Mbeya ambako alirushiwa maswali magumu huku viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) mkoani humo wakisusia kikao hicho.

Alipoulizwa sababu za serikali kuwatumia mawaziri wake kuzunguka mikoani kueleza mafanikio hayo, Waziri Marmo alisema: "Mawaziri si makatibu wakuu ambao wao wanatakiwa kukaa ofisini kufanya kazi za utendaji na si kwenda kwa wananchi kwa kuwa wao si wanasiasa," alisisitiza.

Alisema ni busara kupeleka mrejesho wilayani na mikoni kwa kuwa Dar es Salaam ni kitovu cha utekelezaji wa sera na wananchi wa mikoani hawajui hivyo inabidi wakaelezwe na mawaziri hao.

Hii si mara ya kwanza kwa msemaji huyo wa Ikulu kukanusha habari bila ya kutoa ufafanuzi wa kina. Mwaka juzi alikanusha habari iliyochapishwa na Mwananchi kuwa Rais Jakaya Kikwete amejitosa sakata la umeme, lakini baadaye gazeti hili lilichapisha habari taarifa ambayo msemaji huyo aliituma ikionyesha kuwa mkuu huyo wa nchi alijadiliana na Wizara ya Nishati na Madini kuhusu tatizo la umeme na kuagiza kuwa Sheria ya Manunuzi ya Umma isiwe kikwazo.

Pia mwaka juzi, msafara wa Rais Kikwete ulishambuliwa na wananchi mkoani Mbeya, lakini Salva akakanusha akidai kuwa wakazi hao walikuwa wanataka rais awahutubie na kuwaelezea kuwa ni walevi. Hata hivyo, miezi kadhaa baadaye, kiongozi wa kundi hilo alikamatwa baada ya kufuatiliwa na maofisa wa serikali.

Marmo alisema yeye amepangia mkoa wa Singida na kwamba fedha zitakazotumika katika ziara hizo hazitatoka nje ya bajeti za wizara zao.

Imekuwa ni kawaida kwa msemaji huyo wa rais

Akielezea mafanikio yaliyopatikana katika awamu hiyo, Waziri Marmo alisema serikali imeweza kuvuka lengo la kutoa ajira milioni moja kwa wananchi wake kama ilani ya uchaguzi ya CCM ilivyoahidi.
Alisema ajira hizo zimepatikana kwa sababu ya mazingira mazuri ya uwekezaji, shughuli za ujenzi, sekta ya madini na mawasiliano.

Kwa upande wa wizara yake Waziri Marmo alisema katika kipindi cha miaka mitano ofisi yake imeweza kuimarisha utawala bora, kujenga mfumo wa demokrasia imara wenye kuheshimu haki za wananchi katika ngazi zote, kutekeleza sera ya menejimenti ya maafa ya mwaka 2004 kwa kujenga uwezo wa kukabilana na majanga na kuchapa nyaraka za serikali.

Aidha, mambo mengine ni kuratibu udhibiti wa dawa za kulevya, kuimarisha vita dhidi ya ukimwi, kuendeleza Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma, Kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuendeleza sekta binafsi, kuboresha huduma za watumishi wake na wananchi pamoja na kuimarisha masoko ya mazao ya wakulima na huduma za kifedha vijijini.

Chanzo: Mwananchi
 
Jk anaogopa kumtimua Salva kwa sababu moja tu -- alilazimishwa na Rostam kumpa hiyo kazi. Narudia alilazimishwa na JK ilibidi akubali kwani anajua fika RA ndiye aliyemuingiza ikulu kutokana na hela za wizi za Kagoda. Siku JK akijitutumua na kumfukuza tu, basi RA ataweka hadharani siri yote ya kagoda pamoja na vimemo vya jinsi vigogo wa CCM walivyokuwa wanasainishwa wakati alipokuwa anawagawia mamilioni yale kule Mindu Street.

Hivi ndivyo Ikulu yeti inavyoendeshwa na mdosi wa kutoka Igunga -- kiasi kwamba hadi akina Makamba na Pinda wanazungumza madudu tu,m linapokuja suala la kingmaker wao -- au tuseme Small God wao. Wanaona ni bora waongee pumba kuliko kukaa kimya!!!
 
Jk anaogopa kumtimua Salva kwa sababu moja tu -- alilazimishwa na Rostam kumpa hiyo kazi. Narudia alilazimishwa na JK ilibidi akubali kwani anajua fika RA ndiye aliyemuingiza ikulu kutokana na hela za wizi za Kagoda. Siku JK akijitutumua na kumfukuza tu, basi RA ataweka hadharani siri yote ya kagoda pamoja na vimemo vya jinsi vigogo wa CCM walivyokuwa wanasainishwa wakati alipokuwa anawagawia mamilioni yale kule Mindu Street.

Hivi ndivyo Ikulu yeti inavyoendeshwa na mdosi wa kutoka Igunga -- kiasi kwamba hadi akina Makamba na Pinda wanazungumza madudu tu,m linapokuja suala la kingmaker wao -- au tuseme Small God wao. Wanaona ni bora waongee pumba kuliko kukaa kimya!!!

That is exactly counter punch.
 
hii ajira ya Rweyemamu pale magogoni ilishaongolewa sana,wengi tunaifahamu! huyu jamaa kiazi hakuna mfano!! yeye ni kukanusha tu hata akiambiwa 2+2=4..atabisha ili mradi amfurahishe RA wake.
 
Back
Top Bottom