Huyo ni mbunge wa wananchi kupitia CHADEMA, anatetea maslahi ya wananchi. Wabunge hawa ni wachache lakini wananchi tunatambua kazi yao . Wabunge wangine ni wa mafisadi, ambao hata uteuzi wao ndani ya chama chao ili kugombea ubunge ni wa mashaka ya kifisadi. Kazi yao pia tunaijua, kusinzia, kuomba miongozo ya kuwabughudhi wabunge wa wananchi, wanachoweza sana ni kujifanya wanapinga hoja kwa povu jingi na kasha kusema wanaunga mkono hoja 100% na /au kuitikia ndiooooo! hata kama hajasikia nini kimeongelewa. Tuamke wananchi wote, tuongeze wabunge wa wananchi na kuwaondoa wabunge wa kusinzia na kuunga mkono hoja.