elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
WAZIRI wa Ardhi William Lukuvi ameagiza Wakazi wa Sinoni mkoani Arusha kumlipa Bibi Nasi Muruo (98) kiasi cha Sh. milioni 519 kwa kosa la kuvamia eneo lake na kujenga baada ya kushinda kesi ya kudhulumiwa ardhi yake tangu mwaka 1979 na kuzungushwa.
atimaye kaya 109 zimetakiwa kumlipa fidia jumla ya Sh519.3 milioni kikongwe Nasi Muruo(98) mkazi wa eneo la Sinoni, katika jiji la Arusha, baada ya kurejeshwa ardhi yake aliyokuwa anaidai kwa miaka 42 .Waziri Lukuvi ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na kaya 109 zilizovamia eneo la bibi huyo katika viwanja vya shule ya msingi Sinoni.
Amesema kila kaya italipa kiasi cha Sh20,000 kwa mita moja ya mraba katika eneo la bibi huyo, lakini italipia pia fedha za kupimwa ardhi ili kupewa hati ndani ya miezi mitatu "Kila manachi aliyopo hapa ili zoezi la uvamizi na majina yenu ya uvamizi yaweze kubadilika na muitwe wamiliki ni lazima utaratibu ufuatwe ili nikija siku nyingine hapa nizungumze na wamiliki wa ardhi sio wavamizi wa ardhi kwa sababu mtakuwa na hati zenu," amesema Lukuvi na kuongeza kuwa; "Sasa hili zoezi la kubadilisha majina yenu kutoka wavamizi kuwa wamiliki ni lazima utaratibu ufanyike na muwe wazalendo mlipe kodi ya kila mwaka lakini lazima huyu mama alipwe na kiwango atakacholipwa mtamchangia wote nyinyi, haipungui milioni 500 kwa uchache kwa sababu tumepunguza tumewapaneni kiwango cha chini kabisa cha shilingi elfu 20,000 mtachanga na kuingiza kwenye akaunti yake," amesema Kikongwe huyu alirejeshewa ardhi yake, Julai 8, 2019 na Waziri Lukuvi, kutokana na maelekezo ya Rais John Magufuli wa Tanzania, alipomtaka kushughulikia mgogoro huo, hasa baada ya kuripotiwa malalamiko ya Kikongwe huyo, kunayanyang’anywa ardhi yake tangu mwaka 1977 na ndugu wa ukoo wao, Edward Lenjeshi