Wazee wampongeza Lembeli kuteuliwa taasisi ya kimataifa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Kahama. Siku chache baada ya mbunge wa zamani wa Kahama, James Lembeli kuteuliwa kuwa mwenyekiti mwenza wa Taasisi ya Kimataifa ya Uhifadhi na Mazingira, wazee wamempongeza, wakisema ni heshima kwa Taifa.
2eba07f2b639887cf535ebdd8de8c604.jpg

Hivi karibuni, Lembeli aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa taasisi ya Jane Goodall yenye makao yake makuu katika Jimbo la Virginia nchini Marekani. Taasisi hiyo hufanya kazi zake katika nchi 140 duniani.

Lembeli pia ni mjumbe wa bodi ya shirika jingine la hifadhi la African Parks Network lenye makao yake makuu jijini Johanessburg, Afrika Kusini.

Katika hafla ya kumpongeza Lembeli juzi, mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wa Kahama (Uwaka), Nathan Homgan alisema wameamua kutumia fursa hiyo kutambua heshima yake kimataifa.

Umaarufu wa Lembeli uliongezeka wakati alipopinga Operesheni Tokomeza iliyotekelezwa vibaya kwa kukiuka haki za binadamu.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu Lembeli huwa anaitumia vizuri akili yake.
 
ok vizuri asijaribu ule mchezo aliotaka kuufanya 2014/15 kuhusu mikataba ya maliasili hususani Hifadhi za Taifa na mbuga za wanyama zetu kwani African Parks Network walidondosha mate hahahaha wakameza mate, yakaambulia mchanga wa kaburi acha waharishe
 
Ameanza hii kazi muda mrefu sana!! Kabla , ubunge wake kupokwa.....muda wote yuko nje!! Njaa sio kivile kama mimi na wewe!!!
Hawa wakubwa hata akiwa na v8,anaweza kuwa ana njaa ni tofauti na wewe njaa yako ya kulala bila kula
 
Nilete hoja kwako unitoe koromeo?
Mmeshazoea kuchinjana sasa mnajipenyeza kwetu kueneza chuki tuchinjane
Hapo kahama mmejaa wengi sana kwa kuwa mnakuja kwa taxi tu
Kachukue buku saba Lumumba.. Maana nahisi njaa ndo inayokusumbua.. Maana huwez tamka kuwa ana njaa mtu ambaye kawahi kuwa mbunge ili hari ww hata ujumbe wa nyumba kumi hujawahi pata. Umasikini ndo chanzo cha roho mbaya
 
Back
Top Bottom