Aisee pole sana mkuu kwa mkasa huu..
Hapa kuna somo kubwa sana la kujifunza...
Mimi ni mwenyeji wa Chaga, mataa wa December naufahamu vizuri..
Wale jamaa sijui wana mtandao gani..? Ukishaulizia kitu duka moja mkashindwa bei, maduka yote utakutana na the same story..
Kuna madalali sijawahi kuona, hata bolt namba 12 ukitaka, inadalaliwa...

Ule mtaa nimejenga urafiki na fundi mmoja tu, tena huyu fundi nilitafutiwa na mzee mmoja mwenye duka pale December..huyu mzee nilinunua kifaa kwake used, akaniambia atanipa kijana mzuri anifungie, kwa sababu yeye ndiyo fundi wake hata akinunua gari za kichinja ,ndiyo mvhinjaji wake..
Jamaa ni fundi mzuri na tunaelewana sana..
December, punguzeni madalali ni kero kwa wateja..

