Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Aaaaaah issue huwa ni timing tu mkuu, alafu kawaida kabla haujaamua kushambulia ni lazima ujue idadi ya maadui na wamejipangaje.

Unaweza ukawa na bastola afu wahuni wakawa na SMG na akawa sehemu ambayo labda si visible kwako ,ukajikuta unakula chuma sehemu ambayo ungeweza kuganya nao negotiation ya kawaida kabisa.

Chuma huwa tunatumia pale ambapo unaona kabisa uwezekano wa wewe kuopona haupo ( ile situation ambayo hata uwape nini ni lazima wakuue).Pale mimi niliamua kushambulia bila kujali yote hayo ili kujichukulia point kwa mama watoto wangu😅.Mpaka leo mke wangu huwa ananikumbusha hilo tukio.
Anakuona kama Komando Rambo 😀😀
 
Mwaka 2009 wakati tunatoka babati kuja Singinda tupofika pale Hanang (enzi hizo kuna rough road) majira ya saa saba usiku, tukashangaa kuona malori kama manne hivi yamesimama na tukawa tunasikia kelele ishara ya kwamba hakukuwa na utulivu pale.

Vuuuuup nikala break, ile tunajiuliza kuna nini au madereva wa haya malori wameamua kulala porini hapa? Mara ngongongo kwenye kioo cha gari, ile nafungua tu nikala kelbu moja matata sana.... Woote shuka chini faster faster lile jamaa likawa linakoroma, hatujakaa sawa wakaongozeka wakawa watatu.

Kwenye gari (CRUISER) tulikuwa watu wanne, yani mimi rafiki zangu wawili na mke wangu, sasa ile kutaka kuonekana mwamba mbele ya mke wangu, nikasema liwalo na liwe siwezi kuonekana dhaifu acha nice tu wakati nashuka yule mmoja aliyekuwa upande wangu nikashuka nae mazima na teke la mbupu,wakati hawajakaa sawa nikafyatua mbili juu khoo khoo niaasikia wanapiga kelele "Oyaah wana motooo "

Kuanzia sikuiyo huwa sitembei usiku sehemu zenye mapori.
Maisha ndiyo yanatulazimisha kutembea usiku. Binafsi napenda kusafiri usiku ili asubuhi inikute nshafika mahali na kazi iendelee plus kunipunguzia gharama za lodging.
Huyo jamaa ungembariki chuma ya goti ili akajifunze kulima badala ya kuteka.
 
Maisha ndiyo yanatulazimisha kutembea usiku. Binafsi napenda kusafiri usiku ili asubuhi inikute nshafika mahali na kazi iendelee plus kunipunguzia gharama za lodging.
Huyo jamaa ungembariki chuma ya goti ili akajifunze kulima badala ya kuteka.
Hata mimi baadae niliwaza hivyo, kwamba kwanini sikumpa hata ya mguu?

Ila kufyatua ndio ilikuwa option bora zaidi kiusalama,maana uke mlio unawafanya hata wale wezi wengi ambao walikuwa kwenye nagari mengine kukimbia kulikoni kuanza kuwalenga mmojammoja.

Ile paah paaah, faster tu jamaa wakakimbilia pembezoni mwa barabara kwenye mapori. Hapo nilikuwa natetemeka na moyo unaenda mbio,nawaza labda watarudi kutufanyia ambush😁.
 
Sehemu flani hivi 🤓🤓 code zinasomeka
B07BFE89-6BE3-4313-9DBD-D4217F628862.jpeg
 
Naona upepo wa kisurisuri unapitia kwenye jukwaa letu pendwa 😁😁😁.....sidhani kuwa watu wamekimbia kwa kuwa wanafanyia service machine zao tayari kwa road trip za mwisho wa mwaka
Tupo mkuu....sometimes huwa napenda kutoka kwenye social media kwa a week or two. Ni addiction ya aina fulani so huwa najipa muda kuona kama naweza kuishi bila mitandao ya kijamii(except Whatsapp kwasababu za kibiashara)
 
Back
Top Bottom